Ni nini hufanyika wageni wanapoghairi au kubadilisha nafasi iliyowekwa?
Vidokezi
Ikiwa mgeni ataghairi nafasi iliyowekwa, sera yako ya kughairi itatumika
Ikiwa utaidhinisha mabadiliko katika nafasi iliyowekwa na mgeni, utalipwa saa 24 baada ya wakati wake mpya wa kuingia
Chagua sera ya kughairi inayokufaa
Maisha hayana uhakika na wakati mwingine wageni hulazimika kughairi au kubadilisha nafasi walizoweka. Bado unaweza kupokea malipo hata ikiwa mgeni ataghairi, kulingana na sera yako ya kughairi na muda wa mapema ambao wageni wanaghairi.
Haya ndiyo mambo unayoweza kutarajia ikiwa wageni wako wataghairi au kubadilisha nafasi waliyoweka au ikiwa wataomba warejeshewe sehemu ya fedha.
Mgeni anapoghairi nafasi aliyoweka
Ikiwa mgeni ataghairi nafasi aliyoweka, sera yako ya kughairi itatumika. Ikiwa unapaswa kulipwa, pesa hizo kwa kawaida zitatumwa kwako saa 24 baada ya wakati ulioratibiwa wa mgeni wako kuingia.
Kwa mfano, ikiwa una sera thabiti ya kughairi na mgeni wako anaghairi chini ya siku saba kabla ya kuingia, utalipwa asilimia 100 ya bei yako ya kila usiku kwa ajili ya usiku wote, bila kujumuisha kodi na ada zozote. Tutatuma hii saa 24 baada ya muda ulioratibiwa wa mgeni wako kuingia. Hutapokea ada ya usafi, mnyama kipenzi au mgeni wa ziada ikiwa mgeni wako hataingia.
Utaweza kupata rekodi ya malipo yoyote unayopokea au marekebisho katika historia yako ya muamala.
Mgeni anapobadilisha nafasi aliyoweka
Ikiwa mgeni atabadilisha nafasi aliyoweka, kwa kawaida tutatuma malipo saa 24 baada ya wakati wake mpya wa kuingia. Ikiwa unakaribisha wageni wanaokaa muda mrefu, utapokea malipo ya kila mwezi kwa ajili ya nafasi hizi zilizowekwa.
Kwa mfano, ikiwa utaidhinisha ombi la kufanya mabadiliko ili mgeni aje kwa siku 10 mwezi Agosti badala ya siku 10 mwezi Juni na abadilishe kwa muda wa kutosha kiasi kwamba sera yako ya kughairi haitumiki, tutatuma malipo yako saa 24 baada ya wakati mpya wa kuingia wa mgeni wako.
Mgeni akibadilisha nafasi aliyoweka akiwa kwako, malipo utakayopokea katika siku zijazo yanaweza kuathirika.
Kwa mfano, ikiwa mgeni ataingia kwenye eneo lako kwa ajili ya nafasi iliyowekwa ya siku 20, tutatuma malipo yako saa 24 baada ya wakati wake wa kuingia. Lakini ikiwa atalazimika kughairi na kuondoka siku ya 10 na una sera ya kughairi inayoweza kubadilika, utastahili kulipwa kwa kila usiku ambao amekaa, pamoja na usiku mmoja wa ziada.
Katika kisa hiki, kwa kuwa tayari utakuwa umepokea malipo yako kamili, malipo utakayopokea katika siku zijazo yatarekebishwa ili kufidia gharama ya marejesho ya sehemu ya fedha.Mgeni anapoomba arejeshewe fedha
Ikiwa mgeni ataingia kwenye eneo lako akitarajia kupata kistawishi fulani, lakini hakipo au kimeharibika, anaweza kuomba arejeshewe sehemu ya fedha. Kwa mfano, ikiwa beseni lako la maji moto limeharibika bila kutarajia na ni kipengele kikuu cha vila yako, mgeni wako anaweza kuwasiliana nawe ili kuomba arejeshewe sehemu ya fedha.
Kwa mfano huu pia, ukikubali kurejeshewa sehemu ya fedha, malipo utakayopokea katika siku zijazo yatarekebishwa ili kufidia gharama ya marejesho ya sehemu ya fedha, kwa kuwa tayari utakuwa umepokea malipo yako kamili. Unaweza pia kuwafidia wageni kupitia Kituo cha Usuluhishi. Ukituma malipo kwa njia hiyo, malipo utakayopokea katika siku zijazo hayataathiriwa.Kujilinda dhidi ya ughairi
Bila shaka, huwezi kudhibiti iwapo mgeni atalazimika kughairi au kubadilisha nafasi aliyoweka. Lakini unaweza kuwa na uhakika kwamba umeridhika na mipangilio yako kwa kusoma zaidi kuhusu sera zetu za kughairi za mgeni na kuchagua inayokufaa.
Pia ni wazo zuri kufanya matengenezo ya mara kwa mara na kuwasiliana na wageni katika nyakati muhimu, ili uwe na uhakika kwamba eneo lako litakuwa tayari kuwakaribisha wageni, nawe utaweza kuwasaidia ikiwa chochote kitaharibika.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Vidokezi
Ikiwa mgeni ataghairi nafasi iliyowekwa, sera yako ya kughairi itatumika
Ikiwa utaidhinisha mabadiliko katika nafasi iliyowekwa na mgeni, utalipwa saa 24 baada ya wakati wake mpya wa kuingia
Chagua sera ya kughairi inayokufaa