Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Kuelewa mazoea bora ya kukaribisha wageni

  Kuanzia kujibu haraka hadi kuepuka kughairi, hapa kuna mambo ya kuzingatia.
  Na Airbnb tarehe 16 Des 2019
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 12 Okt 2021

  Vidokezi

  • Jibu ujumbe wa wageni na ujibu ujumbe wowote unaohusiana na kuweka nafasi ndani ya saa 24

  • Weka mahitaji ya kuweka nafasi ili uridhike kupokea wageni zaidi

  • Epuka kughairi kwa kuhakikisha unasasisha kalenda yako kila wakati

  • Pata tathmini nzuri kwa kufuata viwango vya ukarimu vya Airbnb

  • Gundua mengi zaidi kwenyemwongozo wetu kamili ili kugundua ulimwengu wa kukaribisha wageni

  Ukiwa mwenyeji wa Airbnb, hutapata tu mapato kwenye nyumba yako, bali utakutana pia na watu wanaovutia kutoka kote ulimwenguni. “Tumekuwa na mtengenezaji wa kamera ya anga, mwimbaji mtunzi mweledi na mwanasarakasi,” wanasema wenyeji Beverlee na Suzie wa Oakland, California. “Imeboresha maisha yetu sote wawili.” Mtu yeyote aliye na sehemu ya kushiriki anaweza kuwa mwenyeji wa Airbnb. Hakikisha uko tayari kutimiza viwango vya msingi vilivyowekwa na Airbnb ili kuhakikisha hali nzuri na wa kuaminika kwa kila mgeni. Haya ni mambo ya msingi ambayo wenyeji bora hufanya:

  Jibu kila ulizo na ombi la kuweka nafasi ndani ya saa 24

  Kujibu haraka wageni wanapowasiliana nawe huonyesha kuwa wewe ni mwenyeji msikivu na mwenye busara. Ni muhimu kujibu ujumbe unaohusiana na kuweka nafasi ndani ya saa 24. Kiwango cha juu cha kutoa majibu si ishara ya ukarimu bora tu, bali ni mojawapo ya vigezo vya kuwa Mwenyeji Bingwa.

  Zingatia kupakua programu ya Airbnb ili uweze kujibu ujumbe ukiwa mahali popote. Na ili kuwa wazi, ingawa kuweza kujibu kila ujumbe wa mgeni ni mazoea mazuri ya kukaribisha wageni, kiwango chako cha kutoa majibu kinategemea hasa majibu yako kwa ujumbe unaohusiana na kuweka nafasi.

  Kubali maombi ya kuweka nafasi

  Data za Airbnb zinaonyesha kuwa wenyeji huwa wanakubali maombi mengi ya kuweka nafasi ambayo wanapokea kwa nyakati wanapopatikana. Unaweza kutumia mipangilio ya upatikanaji kwenye kalenda yako kuzuia siku zozote ambazo huna uhakika kuwa unaweza kukaribisha wageni.

  Ikiwa unaonekana kukataa maombi mengi ya kuweka nafasi, Airbnb inaweza kudhani kuwa hupatikani kwa ajili ya kukaribisha wageni na inaweza kuondoa tangazo lako kwa muda hadi uwe na wakati mwingi zaidi. Ili kuhakikisha kuwa unaweza kukubali maombi mengi kadiri iwezekanavyo wakati bado unaridhika na kila nafasi inayowekwa, zingatia machaguo haya:

  Epuka kughairi

  Airbnb inachukulia kughairi kwa uzito sana. Si kwamba huwavuruga wageni tu, bali mipango yao ya kusafiri hukutegemea wewe!—pia hudhoofisha uhakika kwa jumuiya nzima. Ndiyo sababu, kando na sababu zozote zisizozuilika, kughairi kunapaswa kuepukwa. Ili kupunguza hatari yako ya kughairi:

  • Hakikisha upatikanaji wako na bei zimesasishwa kila wakati
  • Tazamia hafla maalumu au likizo wakati unaweza kutaka kutumia sehemu yako kwa sababu za kibinafsi au kuongeza bei yako ya usiku
  • Ikiwa kwa sababu fulani kalenda yako haiko katika hali bora au unapendelea tu kuidhinisha kila ombi la kuweka nafasi unalopata, zingati kuzima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo
  • Ikiwa utatangaza sehemu yako kwenye tovuti nyingine, washa kipengele cha usawazishaji wa kalenda ili kuzuia wageni wengi kuweka nafasi kwenye tarehe zizo hizo

  Dumisha kiwango cha juu cha ukadiriaji wa jumla

  Mwishoni mwa kila ukaaji, wageni watatathmini hali yao ilivyokuwa wakiwa kwako. Tathmini nzuri zinakusaidia kuwekewa nafasi zaidi na zinaweza kukusaidia kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa. Wenyeji ambao hupata tathmini nzuri huzingatia yafuatayo:

  • Usafi: Wageni watatarajia kupata sehemu safi na nadhifu wanayoona kwenye picha zako za tangazo. Hakikisha unajipa muda wa kutosha kufanya usafi baada ya wageni kuondoka, hasa ikiwa una nafasi zilizowekwa ambazo zinafuatana.
  • Vistawishi muhimu: Wageni wanathamini kuwa na baadhi ya vifaa muhimu panapofikika kwa urahisi. Airbnb inapendekeza kuwa na karatasi ya choo, sabuni ya mkono na mwili, mashuka na angalau taulo na mto mmoja kwa kila mtu.
  • Maelezo sahihi ya tangazo: Wasaidie wasafiri kuamua ikiwa sehemu yako inakidhi mahitaji yao kwa kutoa taarifa wazi na maelezo wanayopaswa kuyajua.
  • Kuingia kwa namna shwari: Mchakato wazi na rahisi wa kuingia utasaidia kuwatuliza wageni wako baada ya mchana-kutwa ya kusafiri.
  • Mawasiliano mahiri: Wageni wanapenda kujua kuwa unapatikana wakati wote wa ukaaji wao. Wasiliana mapema ili uratibu mipango ya kuwasili.

  Kwa vidokezi zaidi kuhusu kudumisha kiwango cha juu ukadiriaji wa jumla, angalia Ukurasa wetu wa ukarimu.

  Zingatia hali kwa ujumla wake

  Airbnb haitarajii kila nafasi inayowekwa kuwa shwari kuanzia mwanzo hadi mwisho—utajifunza mengi na kubadilisha mtindo wako wa kukaribisha wageni kadiri unavyozidi kuwa mzoefu. Kufuata miongozo hii ni hatua nzuri ya kwanza ya kuwa na wageni wenye furaha, tathmini nzuri na safari ya kukaribisha wageni ya kuridhisha.

  Vidokezi

  • Jibu ujumbe wa wageni na ujibu ujumbe wowote unaohusiana na kuweka nafasi ndani ya saa 24

  • Weka mahitaji ya kuweka nafasi ili uridhike kupokea wageni zaidi

  • Epuka kughairi kwa kuhakikisha unasasisha kalenda yako kila wakati

  • Pata tathmini nzuri kwa kufuata viwango vya ukarimu vya Airbnb

  • Gundua mengi zaidi kwenyemwongozo wetu kamili ili kugundua ulimwengu wa kukaribisha wageni

  Airbnb
  16 Des 2019
  Ilikuwa na manufaa?