Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Vidokezi kutoka kwa wenyeji wa Airbnb Plus: Jinsi ya kuwa na makaribisho yenye uchangamfu zaidi

  Fahamu jinsi wenyeji wenye mafanikio wa Airbnb Plus hufanyiza mvuto mara ya kwanza.
  Na Airbnb tarehe 21 Apr 2021
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 21 Apr 2021

  Vidokezi

  • Tazamia mahitaji ya wageni kwa kuwasiliana nao kabla ya kuwasili

   • Hakikisha uingiaji shwari kwa kuandaa kabla ya wakati

   • Fanya maandalizi kwa kuzingatia hisia na kuhakikisha kuwa wageni wanahisi kustareheka

   • Toa vifaa muhimu na uweke vya ziada panapofikika

   • Fanya kuondoka kuwe rahisi na ufuatilie baada ya saa 24

   Wenyeji wa Airbnb Plus ni jumuiya ya watu wa kipekee ambao huchukua kukaribisha wageni kama ufundi na wanachangamana tangu wakati wa kuwasili. Hapa kuna vidokezi vyao muhimu vya kuunda mtazamo mzuri toka mwanzo na makaribisho machangamfu:

   Hakikisha una vifaa wanavyohitaji wageni tayari

   Si lazima usubiri hadi wageni wako wafike ili kuwafanya wahisi kukaribishwa. Siku moja kabla ya kuingia, waulize wageni ikiwa wana maombi yoyote maalumu. Wanasafiri na mnyama kipenzi? Acha vitu vya kuchangamsha au kuchezea. Ikiwa ni kuondoa mzio wa chakula kutoka kwenye stoo ya vyakula au kuacha maelekezo ya jinsi ya kufika eneo ambalo unajua wageni wangependa kutembelea, kufanya mambo mahususi husaidia sana.

   Hakikisha uingiaji shwari

   Wape wageni maelekezo ya wazi wazi jinsi ya kuingia ili kuwaandaa kwa kuwasili kwao, ukijumuisha picha za wapi pa kupata funguo na mlango. Wenyeji wengi wanapenda kutuma maelekezo ya kuingia kupitia programu ya Airbnb. Ikiwezekana, kuwa mwepesi kubadilisha ombi kuhusu kuingia mapema au kutoka kuchelewa

   Jitolee kuwasalimu wageni ana kwa ana, au weka njia rahisi ya mgeni kuingia mwenyewe pamoja na kufuli janja, kisanduku cha funguo cha kicharazio, au mlango ulio na kicharazio cha kuingilia. Zifanye salamu za ana kwa ana kuwa changamfu, fupi na zenye umakini—taarifa yoyote unayoshiriki katika mwongozo wa nyumba, labda huhitaji kuijumuisha kwenye ziara hiyo. Kama wageni watatumia njia ya kuingia wenyewe, wasiliana nao ili kuhakikisha wana kila kitu wanachohitaji.

   Fanya maandalizi

   Wasaidie wageni kujisikia raha kwa kuweka nyuzijoto zinazofaa, kuwasha taa za kuingia na kuweka ujumbe wa kibinafsi wa kuwakaribisha kwa majina yao. Hakikisha sehemu ina harufu nzuri au haina harufu yoyote (kusiwe na harufu ya manukato, kemikali au harufu kali). Manukato yoyote yanahitajika kuwa ya kiasi na ya asili, kama harufu ya mikaratusi, lavenda na machungwa—jaribu chombo cha kueneza harufu au mafuta asili.

   Fanya iwe rahisi kwa wageni kupata kile wanachohitaji, katika nyumba yako na katika eneo lako. Weka barua fupi za kirafiki na vidokezo vinavyosaidia, ikiwemo makumbusho kuhusu kile kinachopatikana au kilichopigwa marufuku. (Ni sawa kuweka barua hizo hizo kwa muda mrefu, ilimradi hazijachanika au kuchafuka.) Hakikisha unatoa mwongozo wa nyumba ambao ni rahisi kutumia ulio na vidokezi vya ndani kuhusu eneo lako, mambo ya kufanya kitongojini na vivutio vya eneo husika.

   “Mke wangu huwasalimu wageni kwa chupa ya mvinyo; ninawasalimu kwa mayai nusu dazeni. Tunajaribu kuungana na kila mgeni kwa njia fulani,” anasema Darrel, mwenyeji wa Airbnb Plus kutoka Atlanta. Ukarimu wake unalipa: "Darrel alikuwa mkarimu sana tulipofika kwenye nyumba yake," anasema Harrison, mgeni. "Maelekezo yake yalikuwa wazi kabisa, kwa hivyo hakukuwa na mkanganyiko wakati wa kuingia au kutoka."

   Toa vifaa muhimu na vya ziada

   Ruhusu wageni wafurahie mara moja kwa kuandaa vistawishi vya kutosha kwa muda wote wa ukaaji. Kwa mfano, wakati wote uwe na karatasi za chooni za kutosha na viungo vya jikoni kama pilipili nyeusi, chumvi na mafuta ya kupikia. Ili kuifanya safari kuwa nyepesi kwa wageni, jiandae kutoa vitu vinavyoombwa mara nyingi, kama taulo za ziada na blanketi.

   Kidokezi cha bonasi: Kununua mahitaji kwa wingi (kama sabuni za maji au chai na kahawa) kunaweza kukusaidia kuokoa pesa. Aidha, kujaza tena maji kwenye chupa na vyombo ni bora kwa mazingira na inavutia pia.

   Fanya kuondoka kuwe laini na rahisi

   Kuagana kirafiki kunapendeza kama vile makaribisho machangamfu. Kadiri inavyowezekana, kubaliana na maombi yoyote ya kutoka kwa kuchelewa. Wasaidie wageni kupanga safari zao kwa kutuma barua ikionyesha njia ya haraka zaidi kufika uwanja wa ndege au kituo cha treni.

   Ruhusu kutoka kuwe rahisi kama vile kufunga mlango au kuacha ufunguo—wageni hawapaswi kuombwa kutupa takataka au kuosha vyombo au vitambaa. Ndani ya saa 24 baada ya kutoka, watumie wageni ujumbe, ukiwashukuru na kuwauliza ikiwa mambo yalienda vizuri wakati wa ukaaji wao.

   Usisahau kuwa mawasiliano ya wazi ni muhimu, tangu wakati kabla ya kuingia hadi baada ya kutoka. Unapokaribisha wageni zaidi kwenye sehemu yako, utapata njia yako ya kipekee ya kuwafanya wahisi kama wao ni sehemu ya eneo lako.

   Vidokezi

   • Tazamia mahitaji ya wageni kwa kuwasiliana nao kabla ya kuwasili

    • Hakikisha uingiaji shwari kwa kuandaa kabla ya wakati

    • Fanya maandalizi kwa kuzingatia hisia na kuhakikisha kuwa wageni wanahisi kustareheka

    • Toa vifaa muhimu na uweke vya ziada panapofikika

    • Fanya kuondoka kuwe rahisi na ufuatilie baada ya saa 24

    Airbnb
    21 Apr 2021
    Ilikuwa na manufaa?