Faida za kukaa usiku mzima katika eneo lako

Wewe mwenyewe kuwa mgeni kunaweza kukusaidia kuona maeneo unayopaswa kuyaboresha.
Na Airbnb tarehe 20 Nov 2019
video ya dakika 2
Imesasishwa tarehe 14 Mei 2021

Vidokezi

  • Inasaidia kukaa katika eneo lako kana kwamba wewe ni mgeni

  • Kupata uzoefu wa sehemu yako kutoka kwa mtazamo wa mgeni hukuruhusu kujua iwapo kuna kitu chochote unachotaka kuongeza au kurekebisha

  • Baada ya ukaaji wako, kwa mfano, unaweza kuamua kusafisha njia ya kuingia au kuongeza uchaga wa mizigo kwenye chumba cha kulala

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni

Njia moja ya kuhakikisha kuwa sehemu yako iko tayari kwa wageni ni kulala hapo usiku kucha (au mwombe rafiki yako). Anza kutoka mwanzo kabisa kana kwamba unawasili kwa mara ya kwanza: Je, maelekezo ya maegesho yako ni wazi? Je, unaweza kujua njia hadi kwenye mlango wakati wa usiku kwa urahisi? Je, kuna mahali pa kuweka mizigo yako? Kuoga na kulala katika sehemu yako kunaweza kukusaidia kuangalia mara mbili ikiwa shinikizo la maji ni sawa na kitanda ni kizuri. Usisahau kupitia mchakato wa kutoka—ikiwa kuna ufunguo, je, unajua wapi pa kuuacha? Ikiwa kasoro zozote zinatokea, ni wazo zuri kutenga muda ili kurekebisha sehemu yako au kuongeza ubainifu kwa maelezo ya tangazo lako, mwongozo wa nyumba na maelekezo ya kuingia.

Vidokezi

  • Inasaidia kukaa katika eneo lako kana kwamba wewe ni mgeni

  • Kupata uzoefu wa sehemu yako kutoka kwa mtazamo wa mgeni hukuruhusu kujua iwapo kuna kitu chochote unachotaka kuongeza au kurekebisha

  • Baada ya ukaaji wako, kwa mfano, unaweza kuamua kusafisha njia ya kuingia au kuongeza uchaga wa mizigo kwenye chumba cha kulala

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni
Airbnb
20 Nov 2019
Ilikuwa na manufaa?