Kuunda mchakato rahisi wa kuingia

Toa maelekezo ya hatua kwa hatua na ukaribisho mzuri.
Na Airbnb tarehe 3 Jan 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 4 Jun 2024

Uzoefu wa kuingia huanza na mawasiliano dhahiri na huishia kwa kuwasaidia wageni kujisikia kukaribishwa na kutulia katika sehemu yako. Hivi ndivyo jinsi ya kuunda mchakato wa kuwasili kwa urahisi.

Unda mchakato wako wa kuingia

Nenda kwenye mwongozo wa kuwasili wa tangazo lako ili uweke mchakato wa kuingia ambao ni rahisi na wa kuaminika.

  • Chagua muda wa kuingia. Fikiria ni muda gani utahitaji kabla wageni wengine hawajaingia. Wenyeji wengi wanapendelea kuingia mchana kwa hivyo kuna muda wa kutosha wa kufanya usafi kabla ya wageni wanaofuata kuwasili.

  • Andika maelekezo dhahiri ya kufika kwenye sehemu yako. Jumuisha maelezo muhimu ikiwa ni vigumu kupata au huduma ya simu si thabiti katika eneo hilo.

  • Chagua njia ya kuingia.Wageni wengi wanapendelea urahisi wa kuingia mwenyewe, ambao unawaruhusu waongie ndani bila wewe kuwepo.

  • Toa maelekezo ya kuingia. Baada ya kuchagua njia ya kuingia na kuweka maelezo, kama vile mahali ambapo kisanduku chako cha funguo kipo, unaweza kuweka maelekezo ya hatua kwa hatua yenye picha katika sehemu hiyo hiyo.

  • Unda mwongozo wa nyumba na kitabu cha mwongozo. Shiriki taarifa muhimu kuhusu eneo lako, kama vile jinsi ya kuunganisha kwenye Wi-Fi na vidokezi vya mahali ulipo, ikiwemo maeneo ya kula chakula.

Wageni wanaweza kufikia maelekezo yako ya kuingia kwenye maelezo ya safari yao saa 48 kabla ya muda wa kuingia au saa 24 kabla ikiwa una sera ya kughairi inayoweza kubadilika.

Fikiria kuratibu ujumbe kwa siku moja au mbili kabla ya kuingia. Ni fursa kutuma maelekezo yako ya kuingia kwa wageni wote kwenye nafasi iliyowekwa na uwaombe wawasiliane nawe ikiwa wana maswali yoyote.

Andaa eneo lako

Jinsi wageni wanavyohisi wanapofungua mlango ni sehemu muhimu ya mchakato wa kuingia.

  • Hakikisha eneo lako halina doa. Unda utaratibu unaojumuisha kusafisha sehemu zote, sakafu na nguo na uhakiki mara mbili kwamba madoa yoyote, uchafu na nywele zimeondolewa.

  • Onyesha taarifa muhimu. Weka matoleo yaliyochapishwa ya mwongozo wa nyumba yako na kitabu cha mwongozo katika sehemu inayoonekana wazi.

  • Toa zawadi ya ukaribisho. Hiki kinaweza kuwa kitu rahisi kama vile ujumbe ulioandikwa kwa mkono au zawadi kutoka mahali ulipo.

  • Kuwa na njia mbadala ya kuingia. Fikiria kuweka ufunguo wa ziada kwenye kisanduku cha funguo karibu na mlango ikitokea njia ya msingi ya kuingia haifanyi kazi.

Vyovyote vile ulivyochagua kuwakaribisha wageni, wewe au Mwenyeji Mwenza mnapaswa kupatikana wakati wa kuingia ili kutatua haraka matatizo yoyote ambayo yanaweza kutokea. Kuitikia haraka wageni wanapowasili pia kunaweza kuweka mwelekeo mzuri katika mchakato uliosalia wa ukaaji wao.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
3 Jan 2020
Ilikuwa na manufaa?