Tunakuletea kichupo cha Matangazo

Seti ya nyenzo mpya za kusimamia tangazo lako na kuonyesha maelezo ya nyumba yako.
Na Airbnb tarehe 8 Nov 2023
video ya dakika 5
Imesasishwa tarehe 11 Mac 2024

Kusimamia tangazo ni mojawapo ya sehemu muhimu zaidi za kukaribisha wageni kwa sababu ndivyo wageni wanavyoielewa nyumba yako. Tumeona kwamba matangazo yenye maelezo zaidi yanaweza kupata uwekaji nafasi wa hadi asilimia 20 zaidi. Lakini matangazo mengi yanakosa maelezo ambayo wageni wanajali kwa sababu kuyaweka limekuwa jambo gumu sana.

Ndiyo sababu tunawaletea kichupo cha Matangazo, seti ya nyenzo mpya ambazo hukuruhusu kudhibiti tangazo lako kwa urahisi na kuonyesha maelezo ya nyumba yako.

Hapa kuna vipengele muhimu vya kichupo kipya cha Matangazo:

  • Kihariri cha tangazo hufanya iwe rahisi kuweka maelezo kuhusu tangazo lako, ikiwemo vistawishi, mipangilio ya kulala na kadhalika. Kiolesura kilichobuniwa upya pia hufanya iwe rahisi kuhariri taarifa ya kuwasili ambayo wageni wanahitaji kabla ya kuingia.
  • Ziara ya picha inayowezeshwa na AI inakusaidia uunde ziara ya picha ya tangazo lapo papo kwa hapo. Hupanga picha kulingana na chumba ili kuwasaidia wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako. Unaweza kuhariri ziara yako ya picha wakati wowote na uweke vistawishi kwenye kila chumba.
  • Uunganishaji wa kufuli janja unakuwezesha kuunganisha kufuli janja linalolandana kwenye akaunti yako ya Airbnb na kutengeneza kiotomatiki msimbo wa kipekee kwa kila nafasi inayowekwa.

Kuanza kutumia kichupo cha Matangazo

Bofya kichupo cha Matangazo katikati ya upau wako wa maelekezo. Sasa uko kwenye Kihariri cha tangazo. Zana hii iliyosanifiwa upya hurahisisha jinsi unavyoweka taarifa kwenye tangazo lako na hutoa vidokezi kuhusu njia bora za kuonyesha maelezo.

Kihariri cha tangazo kimegawanywa katika sehemu mbili:

  • Sehemu yako ni mahali ambapo unasimamia ukurasa wa tangazo lako na kuweka maelezo kuhusu nyumba yako.

  • Mwongozo wa kuwasili ni pale unapoweka maelezo ambayo wageni wanahitaji kabla ya kuingia.

Sehemu yako

Hapa ndipo utaweka maelezo kuhusu nyumba yako, kama vile kichwa cha tangazo lako, maelezo, na vistawishi.

Kuweka vistawishi
Sasa ni rahisi zaidi kuweka vistawishi kwenye tangazo lako. Nenda kwenye Vistawishi kisha ubofye ishara ya kujumlisha. Unaweza kuona vistawishi karibu 150 kulingana na herufi au kwa kategoria, ikiwemo Burudani, Familia na Nje. Unaweza pia kutafuta kistawishi kulingana na jina, hakuna kusogeza kunahitajika. Chagua Weka mbele ya kipengele chochote ambacho nyumba yako inacho.

Kuunda ziara ya picha
Picha zenye ubora wa juu ni mojawapo ya sehemu muhimu zaidi za tangazo zuri. Zinawavutia wageni na zinaweza kusaidia kuvutia uwekaji nafasi zaidi.

Unaweza kutumia ziara ya picha mpya inayowezeshwa na Akili Bandia (AI) ili kupanga picha za tangazo lako papo hapo katika ziara ya picha ili kuwasaidia wageni kuelewa mpangilio wa nyumba yako. Unachohitaji kufanya ni kubofya tu Unda ziara yako ya picha. Ni hivyo tu.

Injini mahususi ya Akili Bandia (AI) inatambua picha za ndani na nje na inapanga kila picha kiotomatiki kwenye mojawapo ya aina 19 za vyumba na sehemu.

Kisha, unaweza kuweka maelezo kwenye kila chumba. Kwa mfano, unaweza kuongeza kwamba chumba cha kulala kina kitanda cha ukubwa wa juu au sebule ina TV. Unaweza pia kujumuisha taarifa kuhusu vipengele vya ufikiaji, ukifuata miongozo hii.

Unaweza kuhariri ziara yako ya picha wakati wowote kwa kuondoa, kusogeza au kuweka picha. Baada ya kumaliza kuhariri, hakiki tangazo lako kwa kubofya kitufe cha Angalia.

Mwongozo wa kuwasili

Hapa ndipo utaweka maelezo ambayo wageni wanahitaji baada ya kuweka nafasi na kabla ya kuwasili, kama vile wakati wa kuingia na maelekezo yoyote maalumu au maelekezo ya maegesho. Na kwa mara ya kwanza, utaweza kuona taarifa yako ya kuwasili kama wageni wako wanavyofanya. Bofya tu kitufe cha Angalia.

Kutoa maelezo ya kuingia
Ukitumia mwongozo wa Kuwasili, unaweza kushiriki maelezo ya kuingia kwa urahisi na wageni baada ya kuweka nafasi. Unaweza kuweka au kurekebisha njia yako ya kuingia na muda, maelekezo, mwongozo wa nyumba, nenosiri la Wi-Fi na kadhalika, yote katika sehemu moja.

Kuunganisha kufuli janja lako
Hivi karibuni utaweza kuunganisha kufuli janja lako kwenye akaunti yako ya Airbnb na kutengeneza kiotomatiki msimbo wa kipekee wa mlango kwa kila nafasi inayowekwa. Hakuna misimbo ya kubadilisha mwenyewe tena kati ya nafasi zinazowekwa.

Wageni watapata msimbo katika maelezo yao ya kuweka nafasi kwenye Airbnb, pamoja na maelezo kuhusu jinsi ya kuiweka. Pia watapokea msimbo wao wa mlango katika barua pepe mara tu baada ya kuweka nafasi na watapata arifa wakati wa kuingia. Kila msimbo unafanya kazi tu wakati wa ukaaji wa mgeni. Misimbo inaisha muda dakika 30 baada ya kutoka isipokuwa urekebishe mwenyewe muda huu kwa ajili ya wageni wako.

Uunganishaji wa kufuli janja utaanza kutekelezwa mapema mwaka 2024 kwa wageni wenye nyumba nchini Marekani na Kanada na makufuli mahususi kutoka Schlage. Linapopatikana mahali ulipo, utaliona chini ya Njia ya kuingia. Fuata tu maelekezo ya kuunganisha kufuli janja la nyumba yako kwenye tangazo lako kwenye Airbnb.

Kichupo cha Matangazo ni sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Novemba. Kwa sasa inapatikana kwa Wenyeji wenye matangazo sita au machache. Anza kutumia vipengele vipya leo unapojisajili kwenye Ufikiaji wa Mapema.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
8 Nov 2023
Ilikuwa na manufaa?