Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi kughairi na kurejeshewa fedha kunavyoathiri malipo yako

  Haya ndiyo mambo ya kutarajia wakati mipango ya safari inabadilika.
  Na Airbnb tarehe 19 Jul 2021
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 21 Jul 2021

  Vidokezi

  • Wakati nafasi iliyowekwa imeghairiwa au kubadilishwa, malipo yako yanaweza kurekebishwa

  • Hii inaweza kutokea wakati wa malipo—au kuathiri jinsi unavyolipwa kwa ajili ya nafasi zinazowekwa za wakati ujao

  • Jifunze cha kutarajia na upate vidokezi vya kuzuia kughairi

  Hata mipango iliyowekwa vizuri inaweza kubadilika na hiyo ni pamoja na safari kwenye Airbnb. Kwa mfano, mgeni anaweza kulazimika kughairi nafasi aliyoweka kwako au abadilishe tarehe za ukaaji wake na tunataka kuhakikisha unajua nini cha kutarajia ikiwa jambo hilo litatokea—hasa kwa kuwa linaweza kuathiri malipo yako.

  Habari njema ni kwamba tumefanya mchakato wa kurejeshewa fedha kiotomatiki uwe rahisi zaidi kwako kama Mwenyeji. Endelea kusoma ili ujue jinsi mabadiliko ya safari, kughairi na kurejeshewa fedha kunavyoweza kuathiri malipo yako na uzoefu wa wageni wako—na upate vidokezi vya kuzuia kughairi safari siku zijazo.

  Je, nini kimetokea?

  Kuna njia kadhaa ambazo mabadiliko ya safari yanaweza kuathiri malipo yako. Hizi ni sababu tatu kuu zinazoweza kufanya uone tofauti katika fedha:

  1. Mabadiliko: Mgeni alibadilisha urefu wa ukaaji wake kwako.
  2. Kughairi: Mgeni alighairi ukaaji wake kwako.
  3. Usuluhishi: Jambo fulani kuhusu sehemu ya kukaa ya mgeni wako halikukidhi matarajio na akaomba kurejeshewa fedha.

  Wageni wako: Airbnb hushughulikia fedha wanazorejeshewa

  Kwa hivyo, ni nini hufanyika ikiwa mgeni wako anaweka nafasi ya safari ambayo baadaye haendi? Hiyo inalingana na sera yako ya kughairi. Na itakuwa vipi ikiwa beseni la maji moto ambalo lilitangazwa kwenye tangazo lako linavunjika bila kutarajiwa? Mgeni wako anaweza kuwasiliana nawe moja kwa moja au kuwasiliana na usaidizi kwa wateja wa Airbnb ili kuomba kurejeshewa sehemu ya fedha.

  Wakati ambapo kurejesha fedha zote au sehemu yake kunahakikishwa , ni rahisi sana: Airbnb humrudishia pesa mgeni wako. Ni ya kiotomatiki, kama ilivyo kwa mfumo wetu mwingine wa malipo.

  Malipo yako: kupima wakati ni muhimu sana

  Jinsi hii inavyoathiri fedha zako inategemea lini mgeni wako amerudishiwa pesa.

  • Ikiwa amerejeshewa fedha kabla hujapokea malipo kwa ajili ya safari yake: Malipo yako yataghairiwa au kubadilishwa kulingana na sera yako ya kughairi au maelezo mapya ya safari.
  • Ikiwa amerejeshewa fedha baada yako kupokea malipo kwa ajili ya safari yake: Malipo yako ya siku zijazo yatabadilishwa kiotomatiki ili kulipia gharama ya fedha zilizorejeshwa. Kama tulivyosema, Airbnb humrudishia mgeni pesa mara moja kisha Wenyeji wanawajibika kuirudishia Airbnb pesa. Kimsingi, tunalipia gharama kabla ili safari ya wageni iwe nzuri, kisha tunarudisha fedha hizo kutoka kwenye mapato yako ya siku zijazo. Hii ndiyo sababu huenda usipokee malipo kwa ajili ya nafasi zako zilizowekwa zijazo au kwa nini malipo yako yajayo yanaweza kuonekana kuwa chini kuliko unavyotarajia. Utaona hii ikiwa imeorodheshwa kama kiasi hasi kwenye barua pepe wakati malipo yako yanatolewa na vile vile kwenye historia yako ya muamala.

  Kuzuia kughairi

  Kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili kuhakikisha marekebisho ya kiotomatiki hayakushtui:

  Vidokezi

  • Wakati nafasi iliyowekwa imeghairiwa au kubadilishwa, malipo yako yanaweza kurekebishwa

  • Hii inaweza kutokea wakati wa malipo—au kuathiri jinsi unavyolipwa kwa ajili ya nafasi zinazowekwa za wakati ujao

  • Jifunze cha kutarajia na upate vidokezi vya kuzuia kughairi

  Airbnb
  19 Jul 2021
  Ilikuwa na manufaa?