Kuunda sehemu inayovutia na yenye starehe

Weka akiba ya vitu vya msingi, ifanye iwe safi na acha haiba yako iangaze.
Na Airbnb tarehe 18 Des 2019
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 18 Des 2019

Vidokezi

  • Wasaidie wageni wajisikie wamekaribishwa kwa kutoa nafasi kwa ajili ya mizigo yao

  • Weka vitu zingativu kama vile maua na chaja za simu

  • Toa taulo za ziada, karatasi ya choo na bidhaa kuu kama vile kahawa na chai

Haijalishi ni sehemu ya aina gani unayopangisha kwenye Airbnb, kuna mambo kadhaa rahisi unayoweza kufanya ili kuifanya iwe ya kuvutia na yenye starehe unapojitayarisha kuwakaribisha wageni wako wa kwanza.

Jizoeze ubunifu zingativu

Vipengele vya ubunifu vinavyojali wengine vinaweza kuisaidia sehemu yako ihisi kama nyumbani na yenye kuvutia na si lazima viwe tata au vya bei ghali.

Hivi ni vidokezi vichache vya ubunifu zingativu:

  • Onyesha vitu vinavyoonyesha haiba yako, kama vile kumbukumbu kutoka kwenye safari zako
  • Epuka kuacha nafasi nyingi tupu, ambazo zinaweza kuonekana chushi na zisizoonyesha hisia
  • Chagua rangi anuwai na upange michoro yako, nguo na maelezo mengine
  • Fikiria kuweka kitu cha kuvutia, kama vile taa yenye mapambo mengi au kiti kikubwa cha starehe
  • Pamba kwa kuweka mimea au maua ili kuongeza uchangamfu

Weka vistawishi vya kutosha

Ni lazima utoe angalau karatasi ya choo, sabuni, taulo moja na mto mmoja kwa kila mgeni na mashuka kwa kila kitanda cha mgeni.

Wageni pia huthamini sana:

  • Taulo, mablanketi na mito ya ziada
  • Shampuu na mafuta ya kulainisha nywele
  • Kikausha nywele
  • Bidhaa kuu kama vile kahawa, chai na birika
  • Vifaa vya msingi vya kufanyia usafi

Pata taarifa zaidi kuhusu vistawishi

Unda chumba cha kulala chenye starehe

Chumba cha kulala ni mahali ambapo wageni wako watalala na kuweka mizigo yao, kwa hivyo ni muhimu kukifanya kiwe chenye starehe. Fikiria kuhusu kile kinachoweza kukusaidia ujisikie nyumbani katika sehemu ya mtu mwingine.

Kwa mfano, unaweza:

  • Kutengeneza nafasi kwa ajili ya vitu vya kibinafsi kwa kutoa kabati la kujipambia lililo na droo tupu, kabati lililo na viango tupu au uchaga wa kuweka mizigo
  • Kuweka meza kando ya kitanda iliyo na taa, ili wageni waweze kuweka miwani yao, simu au kitabu karibu na kitanda
  • Kuweka godoro bora, mito michache ya ziada na mablanketi laini ili kuegemeza viwango tofauti vya starehe
  • Kuweka mimea, kioo, chupa na glasi ya maji, adapta ya umeme inayotumika kwenye vifaa vingi vya kielektroniki na chaja ya simu nyingi ili kukipa chumba cha kulala hisia ya makaribisho

Weka marekebisho madogo-madogo ya mwisho

Unaweza kuwasaidia wageni wako wafurahie ukaaji wao kwa kufanya mambo kadhaa zaidi ili utimize ukarimu wako mzuri.

1. Ondoa mparaganyo. Ikiwa unaishi katika sehemu unayoshiriki na wageni, ni muhimu kuzingatia vitu unavyoweka nje na vile ambavyo unaondoa. Kuondoa mparaganyo na kuhifadhi mali yako kwa njia ya kupendeza kunaweza kusaidia kufanya sehemu yako ionekane wazi zaidi na yenye kuvutia.

2. Toa maelekezo. Wasaidie wageni kuelewa jinsi ya kutumia vifaa na vipengele vyote (kama vile meko ya gesi, kiyoyozi au mlango wa gereji) vinavyopatikana kwa ajili ya matumizi yao. Unaweza kujumuisha maelekezo haya kwenye mwongozo wa nyumba yako.

3. Lala usiku kucha. Kukaa usiku kucha katika sehemu yako mara chache hufanya iwe rahisi kujua kinachokosekana au kinachohitaji kuboreshwa. Je, sehemu hiyo inaonekana kuwa changamfu na yenye kuvutia? Je, una kila kitu unachohitaji ili kuhisi umestareheka na kukaribishwa? Badilisha mambo hadi uweze kujibu “ndiyo” kwa maswali haya mawili.

4. Dumisha usafi. Iwe unasafisha sehemu yako mwenyewe au unaajiri mtaalamu, ni muhimu kuweka nyumba yako ikiwa nadhifu na ufuate mchakato wa hatua tano wa kufanya usafi kabla na baada ya kila mgeni. Unaweza kuweka ada ya usafi ili kulipia gharama ya wakati wako au wa msafishaji wako. Ili kukusaidia kutayarisha sehemu yako kwa ajili ya wageni, tumeunda orodha kaguzi unayoweza kutumia.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Wasaidie wageni wajisikie wamekaribishwa kwa kutoa nafasi kwa ajili ya mizigo yao

  • Weka vitu zingativu kama vile maua na chaja za simu

  • Toa taulo za ziada, karatasi ya choo na bidhaa kuu kama vile kahawa na chai

Airbnb
18 Des 2019
Ilikuwa na manufaa?