Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Majibu ya Airbnb: Vidokezi vya kuwekewa nafasi zaidi

  Wageni wanajali kuhusu picha—hivi ndivyo unavyoweza kuboresha zako.
  Na Airbnb tarehe 21 Sep 2018
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 5 Okt 2021

  Uliuliza: Ninaweza kufanya nini ili kuwekewa nafasi zaidi?

  Tulienda moja kwa moja hadi kwenye chanzo kwa ajili ya jibu hili: Tuliwauliza wageni kile wanachotafuta katika sehemu za kukaa za Airbnb na tukachambua tabia yao ya kuweka nafasi ili kujua ni nini kinachowatoa kwenye kuvinjari hadi kwenye kuweka nafasi.

  Imebainika kwamba, baada ya bei na tathmini, upigaji picha ndilo jambo muhimu zaidi. Kwa kweli, asilimia 60 ya mwonekano wa tangazo huanza kwa mgeni kubofya picha na zaidi ya asilimia 40 ya wakati ambapo mgeni anachagua kutowekea nafasi tangazo, kitu cha mwisho ambacho alibofya kilikuwa picha. Kwa hivyo picha ni muhimu na zinapaswa kuwa nzuri kadiri iwezekanavyo.

  Anza kwa kupiga picha nzuri ukitumia simu yako au kamera au ikiwa uko tayari kuboresha tangazo lako (na mafanikio katika kuwekewa nafasi), fikiria kupiga picha za kitaalamu.

  Tumegundua kuwa kupiga picha za kitaalamu kunaweza kusaidia tangazo lako kuonekana na kufanya vizuri zaidi kuliko jinsi ambavyo ingekuwa vinginevyo. Hasa, unaweza kutarajia:

  • Uwezekano wa asilimia 16 zaidi wa kuwekewa nafasi
  • Kiasi cha jumla kwa nafasi zilizowekwa kuongezeka kwa asilimia 39 (inamaanisha kuwa wageni huwekea nafasi sehemu za kukaa za muda mrefu)
  • Idadi ya usiku uliowekewa nafasi kuongezeka kwa asilimia 28
  • Bei ya wastani ya kila usiku kuongezeka kwa asilimia 26

  Kama wengi wenu mnavyojua, Airbnb inaweza kuwaunganisha na wapiga picha wa kitaalamu katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni. Unaweza kuomba picha za kitaalamu bila kutozwa gharama ya awali; ada ya huduma itatolewa kutoka kwenye nafasi utakazowekewa katika siku zijazo.

  Ikiwa huduma ya Airbanb ya kupiga picha za kitaalamu haipatikani katika eneo lako, fikiria kuajiri mpiga picha ambaye ana utaalamu katika sehemu za ndani.

  Mara tu unapokuwa na picha ambazo zinaonyesha eneo lako vizuri, ni wakati wa kuwapa wageni watarajiwa muktadha zaidi. Picha nzuri zinahitaji maelezo mafupi mazuri. Na wageni huyasoma. Maelezo mafupi ni fursa yako ya kufanya vitu viwili vikubwa: kuelekeza umakini wa wageni watarajiwa kwenye vitu vya kipekee na vya kuvutia vya eneo lako na kusaidia kuweka matarajio. Kwa hivyo usiwaonyeshe tu kitanda kizuri, bali waambie jinsi kinavyostarehesha. Elezea kile ambacho hawawezi kujionea—kwa mfano, kwamba vigae kwenye sakafu ya bafu vinaweza kupashwa joto. Hii ni nafasi yako ya kuwasaidia wageni kuwazia wakiwa kwenye sehemu yako.

  Kwa kutenga wakati ili kuonyesha na kuwaambia wasafiri jinsi eneo lako lilivyo zuri, watu watavutiwa zaidi. Uangalifu wako kwa mambo madogo-madogo kwenye tangazo lako la mtandaoni unaonyesha kuwa utakuwa mwenyeji anayejali vitu vidogo ambavyo vinaleta utofauti.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Airbnb
  21 Sep 2018
  Ilikuwa na manufaa?