Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Jinsi Airbnb inavyowalinda Wenyeji

Pata maelezo kuhusu ulinzi wa ndani wa Airbnb.
Na Airbnb tarehe 4 Feb 2020
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 26 Mac 2024

Vidokezi

Iwe wewe ni Mwenyeji mpya au unafikiria tu wazo la kukaribisha wageni, unaweza kuwa na maswali kuhusu kulinda sehemu na mali zako wakati wasafiri wanakaa nyumbani kwako. Visa vya uharibifu na usalama ni nadra sana, lakini Airbnb imeweka ulinzi mwingi kwa ajili ya Wenyeji na wageni.

Wasifu na tathmini

Airbnb inakusaidia kuwajua wageni. Ikiwa unatumia kipengele cha Kushika Nafasi Papo Hapo, unaweza kubadilisha mipangilio yako ili kuongeza matakwa ya ziada ya wageni zaidi ya matakwa yetu ya kuweka nafasi kwa ajili ya wageni wote. Na ikiwa unapendelea maombi ya kuweka nafasi mwenyewe, unaweza kuangalia wasifu wa wageni na kusoma tathmini kutoka kwa Wenyeji wa zamani kabla ya kukubali nafasi iliyowekwa.

Kwa kuwa Wenyeji na wageni wanaweza tukuandikiana tathmini baada ya nafasi iliyowekwa kukamilika, unaweza kuwa na uhakika kwamba maoni unayosoma yanategemea hali halisi waliyopitia. Unaweza pia kutumia zana salama ya kutuma ujumbe ya Airbnb kuuliza maswali na kuweka matarajio wakati wowote kabla ya ukaaji wa mgeni.

AirCover kwa ajili ya Wenyeji

AirCover kwa ajili ya Wenyeji ni ulinzi kamili kwa ajili ya kila Mwenyeji kwenye Airbnb. Hii hutoa ulinzi kabla ya safari ili kusaidia kuhakikisha wageni wanaoweka nafasi wako jinsi wanavyodai kwenye uthibitisho wa utambulisho wa mgeni na husaidia kupunguza uwezekano wa sherehe zenye vurugu na uharibifu wa nyumba kupitia teknolojia ya uchunguzi wa nafasi iliyowekwa.

AirCover kwa ajili ya Wenyeji inajumuisha USD milioni 1 ya bima ya dhima ya Mwenyeji na USD milioni 3 ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, pamoja na ulinzi wa kazi za sanaa, vitu vya thamani, magari yaliyoegeshwa, boti na magari mengine na kadhalika.

Pata maelezo zaidi kuhusu AirCover kwa ajili ya Wenyeji

Sheria za msingi

Sheria za msingi kwa ajili ya wageni ni seti mpya ya viwango vinavyoweza kutekelezwa ambavyo wageni wote wanapaswa kufuata. Sheria za msingi zinahitaji wageni waheshimu sehemu yako, wafuate sheria za nyumba yako, wawasiliane mara moja ikiwa matatizo yatatokea na waache nyumba yako katika hali ambayo haihitaji kufanyiwa usafi kupita kiasi. Kila mgeni anayeweka nafasi atakubaliana na sheria hizi kabla ya kuweka nafasi.

Usalama wa akaunti

Airbnb huchukua hatua kadhaa za kulinda akaunti yako, kama vile kuhitaji uthibitisho wa ziada wakati mtu anajaribu kuingia kwa kutumia simu mpya au kompyuta nayo inakutumia arifa za akaunti mabadiliko yanapofanywa. Maadamu unatumia Airbnb katika mchakato mzima, kwa mawasiliano, kuweka nafasi na malipo, unalindwa na sera na ulinzi wa Airbnb.

Usaidizi wa saa 24

Huduma ya usaidizi kwa wateja wa kimataifa ya Airbnb inatoa huduma kwa lugha 62 ili kukupa msaada kuhusu:

  • Usaidizi wa kuweka tena nafasi
  • Kurejesha fedha
  • Upatanishi

Pata taarifa zaidi kuhusu sera na ulinzi wetu

Ukiwa na ulinzi huu uliowekwa, unaweza kukaribisha wageni ukiwa na uhakika. Kwa maelezo zaidi kuhusu njia muhimu ambazo Airbnb hutumia kuwaweka Wenyeji salama, angalia AirCover kwa ajili ya Wenyeji.

AirCover ya Wenyeji kwa ajili ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji,Bima ya dhima ya Mwenyeji na Bima ya dhima ya Matukio haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini Japani, ambapo Bima ya Mwenyeji ya Japani na Bima ya Ulinzi ya Tukio ya Japani zinatumika au Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel LLC. Kwa Wenyeji waliotoa sehemu za kukaa au matukio nchini China Bara, Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China unatumika. Kumbuka kwamba vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD.

Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio inadhaminiwa na watoa bima wengine. Ikiwa unakaribisha wageni nchini Uingereza, sera ya bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio zinatolewa na Zurich Insurance Company Ltd. na zinapangwa na kutekelezwa bila gharama ya ziada kwa Wenyeji wa Uingereza na Airbnb UK Services Limited, mwakilishi aliyeteuliwa wa Aon UK Limited, ambayo imeidhinishwa na kudhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha. Nambari ya usajili ya Aon katika FCA ni 310451. Unaweza kuangalia maelezo haya kwa kutembelea Rejesta ya Huduma za Fedha au uwasiliane na FCA kwa nambari 0800 111 6768. Sera za dhima ya Mwenyeji na dhima ya Matukio ndani ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji zinadhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Fedha. Bidhaa na huduma zilizosalia si huduma zinazodhibitiwa zilizopangwa na Airbnb UK Services Limited. FPAFF405LC

Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si bima na hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji. Chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, utarejeshewa fedha kwa ajili ya uharibifu fulani uliosababishwa na wageni kwenye nyumba na mali yako ikiwa mgeni hatalipia uharibifu huo. Kwa matangazo katika Jimbo la Washington, majukumu ya mikataba ya Airbnb chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji yanalindwa na sera ya bima iliyonunuliwa na Airbnb. Kwa Wenyeji ambao nchi yao ya makazi ni tofuati na Australia, Masharti haya ya Ulinzi dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji yanatumika. Kwa Wenyeji ambao nchi yao makazi ni nchini Australia, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na Masharti ya Ulinzi Dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji kwa Watumiaji wa Australia.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

Airbnb
4 Feb 2020
Ilikuwa na manufaa?