Kwa nini bei yako ya kila usiku inaweza kuonekana tofauti
Vidokezi
Tunajaribu njia mpya za kuonyesha bei katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb
Lengo ni kutambua ikiwa miundo mingine inaweza kuongeza nafasi zinazowekwa
Jaribio haliathiri kiasi cha malipo ya wageni au malipo ya Mwenyeji kwa njia yoyote ile
Kuanzia mwishoni mwa mwezi Septemba, tunajaribu njia tofauti za kuonyesha bei ya sehemu za kukaa, ikiwemo ada zote, katika matokeo ya utafutaji ya tangazo. Lengo ni kuunda uzoefu wa kuweka nafasi ambao ni rahisi, wa haraka na ulio wazi zaidi kwa wageni. Hapa kuna kile unachohitaji kujua kuhusu jaribio hili la bei—na jinsi ya kutoa maoni.
Jaribio hili la bei hufanya kazi vipi?
Jaribio huchagua kinasibu jinsi ya kuwasilisha taarifa za bei kwa wageni katika miundo tofauti. Miundo hiyo inaonyesha bei za kila usiku au jumla ya gharama za safari, pamoja na ada za usafi naada za huduma za Airbnb, katika matokeo ya utafutaji. Kodi zinaonekana kama kipengele tofauti cha ingizo kwenye ukurasa wa malipo.
Jaribio linatumika kwa wageni wanaotafuta sehemu za kukaa katika maeneo fulani ulimwenguni kote. Wakati wa jaribio, mabango yenye ukubwa tofauti yanaweza kuonekana kwenye matangazo, yakiwatangazia wageni mabadiliko hayo.
Je, jaribio hili la bei linaathiri malipo yangu?
Hapana. Kiasi ambacho mgeni analipa na malipo ya Mwenyeji hayaathiriwi kwa njia yoyote ile.
Daima unadhibiti bei uliyoweka kwa ajili ya sehemu yako. Wakati wa jaribio hili, bado unaweza kurekebisha bei yako ya kila usiku katika sehemu ya Bei na Upatikanaji ya maelezo ya tangazo lako.
Kwa nini bei za kila usiku zinahitaji kuonekana tofauti?
Tulibuni huduma yetu iliyopo ili kutoa mchanganuo wa ada na kodi tofauti ili wageni waelewe kikamilifu matozo yanayoweza kuwapo kabla ya kulipa. Katika mwaka uliopita, tumeona kiwango kikubwa cha kurudi kwa usafiri kwenye Airbnb na ingawa tunaamini muundo wetu wa sasa unafanya kazi vizuri, daima tunajitahidi kuboresha uzoefu wa kila mtu.
Kwa kujaribu njia tofauti za kuonyesha bei katika matangazo, tunatarajia kutambua iwapo muundo mpya unaweza kuongeza idadi ya nafasi zinazowekwa za Wenyeji na kuitumikia vyema zaidi jumuiya yetu ya kimataifa.
Ninaweza kufanya nini ili kuunga mkono jaribio hili?
Iwe tangazo lako liko au haliko katika eneo linalohusika katika jaribio, unaweza kubadilisha maelezo ya tangazo lako wakati wowote ili kuonyesha kile kilicho maalumu kukuhusu wewe na sehemu yako—na kuonyesha thamani unayotoa.
Tunakaribisha maoni yako kuhusu kila kitu tunachofanya, ikiwemo jinsi bei zinavyojitokeza katika matokeo ya utafutaji ya tangazo.
Vidokezi
Tunajaribu njia mpya za kuonyesha bei katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb
Lengo ni kutambua ikiwa miundo mingine inaweza kuongeza nafasi zinazowekwa
Jaribio haliathiri kiasi cha malipo ya wageni au malipo ya Mwenyeji kwa njia yoyote ile