Kuweka mkakati wako wa kupanga bei
Kurekebisha bei yako na upatikanaji mara kwa mara kunaweza kukusaidia kuendelea kuwa na ushindani na kufikia malengo yako ya mapato. Hizi hapa ni baadhi ya njia ambazo unaweza kuendeleza mkakati wako wa kupanga bei.
Tathmini mara kwa mara
Kuna mambo machache ya kuweka kipaumbele unapoweka bei yako na upatikanaji.
- Fungua usiku zaidi: Hatua hii husaidia tangazo lako lionekane katika matokeo zaidi ya utafutaji. Ikiwa mipangilio yako inazuia tarehe, utapata vidokezi vya kuzifungua. Kwa mfano, ikiwa muda wako wa chini wa kukaa ni usiku 5 na una usiku 4 ambao haujawekewa nafasi kati ya nafasi zilizowekwa, utaona kidokezi cha kupunguza kima cha chini cha safari yako kwa usiku huo.
- Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji: Hatua hii inakusaidia kukaribisha wageni kwenye ratiba inayokufaa. Rekebisha muda wa safari yako, ilani ya mapema, muda wa maandalizi na kadhalika kwa urahisi.
- Angalia vidokezi vya bei na matangazo sawia: Nyenzo hizi zinakusaidia kuweka bei zenye ushindani kwa siku tofauti, misimu na matukio maalumu. Hutaona vidokezi vya bei au matangazo sawia ikiwa unatumia kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki.
“Ninapenda kuangalia matangazo sawia ili niweze kulinganisha bei zangu, kuhakikisha kwamba bei yangu si ya juu sana au ya chini sana na kutafuta bei iliyo bora,” anasema Karen, Mwenyeji Bingwa jijini Nelson, Kanada.
Unaporekebisha bei yako, kumbuka jumla ya bei ambayo wageni wanalipa, ambayo inajumuisha ada zozote unazoweka.
Jitayarishe kwa nyakati zenye wageni wachache
Hata matangazo maarufu zaidi yanaweza kuwa na vipindi vya ukimya vyenye nafasi chache zinazowekwa. Hizi ni njia chache za kusaidia tangazo lako lionekane.
- Toa mapunguzo: Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi yanaweza kusaidia kujaza kalenda yako na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka. Punguzo la dakika za mwisho linaweza kuwavutia wageni wanaoweka nafasi siku 1 hadi 28 kabla ya kuingia.
- Fupisha ilani ya mapema: Kuwaruhusu wageni waweke nafasi karibu na wakati wa kuingia kunaweza kukusaidia kuvutia nafasi zaidi zinazowekwa. Chagua muda wa mapema ambao ni mfupi kama siku hiyo hiyo, kulingana na maandalizi unayohitaji.
- Ruhusu ukaaji wa muda mfupi: Kupunguza muda wa chini wa safari yako huwavutia wageni wanaotafuta likizo ya haraka. Unaweza kuweka idadi ya chini ya usiku kulingana na siku ya kuingia.
"Kwa kweli ninapata sehemu zaidi za kukaa ambazo ni za muda mfupi," anasema Jimmy, Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Ni sehemu za kukaa za dakika za mwisho ambazo watu hawajapanga, kwa hivyo siku 2 zinaonekana kama likizo nzuri. Urahisi ni wa kuvutia."
Ongeza muda wenye shughuli nyingi
Nyenzo kadhaa za Airbnb zinaweza kukusaidia ufaidike zaidi na nyakati ambazo mahitaji ya wageni ni makubwa. Hizi ni mbinu chache za kuzingatia.
- Zingatia sikukuu na matukio maalumu: Sasisha upatikanaji wako na bei kabla ya matamasha makubwa, sherehe, matukio ya michezo na kadhalika ili kusaidia kuongeza nafasi unazowekewa na mapato yako. Kalenda yako inaangazia sikukuu nyingi na matukio makuu katika eneo lako.
- Weka punguzo kwa watakaowahi: Punguza bei yako kwa nafasi zinazowekwa mwezi 1 hadi 24 mapema ili kuwavutia wageni wanaopanga mapema.
- Panua kipindi chako cha upatikanaji: Kupita muda wa chini wa miezi 3 kunamaanisha tangazo lako litaonekana katika matokeo zaidi ya utafutaji. Unaweza kufungua kalenda yako hadi miaka 2 mapema.
"Wakati mwingine ninapata watu wanaoweka nafasi mwaka mmoja mapema kwa ajili ya likizo za majira ya kiangazi au kwa ajili ya Krismasi miezi 6 mapema," anasema Anne, Mwenyeji Bingwa jijini Tarragona, Uhispania. "Watu ambao huwa wanaweka nafasi mapema kwa kawaida hawaghairi. Ni muhimu pia kwa sababu utajua mapema kinachokuja."
Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.
Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.