Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Ushauri wa Mwenyeji Bingwa wa kukaribisha wageni wa LGBTQ+

Habari ya hivi karibuni ya mwezi Juni ya Bodi ya Ushauri ya Wenyeji inatoa vidokezi vya kuwa Mwenyeji mwenye kujumuisha.
Na Airbnb tarehe 21 Jun 2021
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 14 Jun 2022

Vidokezi

Kila mwezi tunashiriki habari za hivi karibuni kutoka Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na kukusaidia kuwajua wanachama wa bodi.

Habari za kila mtu,

Jina langu ni Peter Kwan, Mwenyeji Bingwa huko San Francisco na mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji. Tangu nilipokuwa Mwenyeji takribani miaka 10 iliyopita, nimekuwa nikiitetea jumuiya ya kukaribisha wageni—ikijumuisha makundi ambayo mara nyingi hupuuzwa katika jamii, kama vile wazee na wanajumuiya wa jumuiya ya LGBTQ+.

Kwa heshima ya Pride, nilishiriki katika hafla ya Airbnb ya "Inayowezeshwa na Wenyeji (Mashoga)" mapema mwezi huu. Yalikuwa mazungumzo mazuri na kundi la viongozi wa Wenyeji mashoga kuhusu jinsi sisi kama Wenyeji wa LGBTQ+ tunavyochangia mafanikio ya Airbnb katika kufanya kujisikia nyumbani kuwe halisi.

Hapa chini unaweza kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasaidia wageni wa LGBTQ+ kujisikia salama katika sehemu yako, pamoja na faida ambayo nimepata kwa kujihusisha na jumuiya ya kukaribisha wageni katika eneo langu.

Kuwa Mwenyeji aliyejumuisha zaidi

Ninawahimiza Wenyeji, kwa njia yoyote wanayoona kuwa inafaa, kusema kwamba nyumba yao ni sehemu salama kwa ajili ya wageni wa LGBTQ+ katika maelezo ya tangazo lao. Huko San Francisco, si ajabu kwa wenzi wa jinsia moja kutembea barabarani wakiwa wameshikana mikono. Lakini kwa wageni wengi wanaotoka nchi zilizo na desturi au sheria tofauti, kutoa maelezo kuhusu hali hii ya eneo husika kunaweza kuondoa wasiwasi.

Ikiwa Mwenyeji atawajulisha wageni kwamba hawaji tu kwenye jiji salama, bali wanakuja pia kwenye nyumba salama, hiyo inaweza kubadlisha kwa njia kubwa amani ya akili ya mgeni. Wageni wanapaswa kujua kabla ya kupiga kengele ya mlango kwamba watapokewa kwa mikono miwili pamoja na wenzi wao wa jinsia moja, kulingana na dhamira ya Airbnb ya kuwasaidia watu "kujisikia nyumbani mahali popote."

Ninawajua Wenyeji wa LGBTQ+ huko San Francisco ambao wana picha kwenye tangazo lao yenye bendera ya upinde wa mvua kwenye kona na maelezo yao yanazungumza kuhusu utambulisho wao na aina ya uanaharakati wanaojihusisha nao.

Unaweza pia kufanya mambo ya kimkakati ili kusaidia kufanya wageni wa LGBTQ+ wajihisi starehe zaidi mara wanapowasili, kama vile kutoa miongozo ya mashoga kwenye jiji na vitabu kuhusu historia ya LGBTQ+. Hiyo huleta tofauti kubwa katika kuwasaidia wageni kujisikia kukaribishwa.

Kupata usaidizi katika jumuiya yako

Baada ya kuwa Mwenyeji, niligundua kwamba hapakuwa na maeneo mengi ya kupata majibu kwa maswali yangu yote.

Nilianzisha kundi la usaidizi wa jumuiya ya Wenyeji mwaka 2012 na tumekuwa tukikutana kila mwezi tangu wakati huo.

Kukaribisha wageni kunaweza kuwa jambo la upweke sana, kwa hivyo ushauri wangu kwa Wenyeji wapya ni kujiunga na Kilabu cha Wenyeji cha eneo husika—au uanzishe ikiwa hakipo. Badala ya kujifunza jinsi ya kuwa Mwenyeji mzuri kupitia majaribio na makosa, unaweza kujifunza kupitia uzoefu wa watu wengine—na unaweza kutengeneza urafiki mzuri.

Inafurahisha sana kuwasaidia Wenyeji wengine, kuhusiana na mambo ya msingi ya kukaribisha wageni—kama vile jinsi ya kuvinjari tovuti—na kuwaalika wanatimu wa Airbnb kuelezea bidhaa mpya na kujadili mabadiliko ya kisheria kwenye mikutano yetu ya Kilabu cha Wenyeji.

Kwa nini mimi pia ni mtetezi wa Wenyeji wazee

Kwa kawaida wazee si kundi linalozingatiwa sana wakati watu wanazungumza kuhusu ujumuishaji na uanuwai katika jumuiya inayokaribisha wageni—nao kwa kweli wanahitaji umakinifu wetu.

Nilijifunza kwamba kwenye Airbnb, wazee ni mojawapo ya makundi yanayoongezeka kwa kasi zaidi ya Wenyeji wapya nchini Marekani na wazee wa kike nchini Marekani wana tathmini thabiti zilizo bora.*

Mojawapo ya mambo ninayotaka kufanya kama mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji ni kuongeza uzingatiaji wa wazee na kusaidia kuhakikisha kwamba Airbnb inapotengeneza bidhaa, wanatufikiria.

Mojawapo ya mambo yanayonifurahisha sana ni kundi dogo nililoanzisha kwa ajili ya Wenyeji wazee wanaoitwa Wenyeji wa Dhahabu. Mimi ni mwanachama kamili wa Chama cha Wastaafu wa Marekani (AARP), kwa hivyo maadamu una sifa za kuwa mwanachama wa AARP, unaweza kujiunga na Wenyeji wa Dhahabu.

Kundi la Wenyeji wa Dhahabu linaongezeka nao ni baadhi ya wanachama ninaowapenda wa jumuiya ya wenyeji siku hizi. Kabla ya COVID, tulikuwa tukienda kwenye nyumba ya mwanachama kila mwezi ili kula pamoja chakula cha jioni cha kuchangia. Lilikuwa jambo zuri sana.

Kwenye kilabu, wazee hufundishana kuhusu kukaribisha wageni. Kama kundi lingine lolote, wazee wanaweza kuwa wepesi wa kujifunza teknolojia na maendeleo mengi ya kidijitali yanayobadilisha maisha yetu, au wanaweza kuhitaji mafunzo maalamu au usaidizi ambao unaweza kutoa elimu yenye matokeo zaidi.

Yale ambayo Bodi ya Ushauri ya Wenyeji imekuwa ikifanya hivi karibuni

Pata maelezo zaidi kuhusu yale ambayo Bodi ya Ushauri ya Wenyeji imekuwa ikifanya na usubiri habari za hivi karibuni na vidokezi vya kila mwezi kutoka kwa wanabodi.

*Kulingana na ripoti ya Airbnb ya "Jumuiya Inayokua ya Airbnb ya Wenyeji Wanawake 60 na Zaidi"
Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

Airbnb
21 Jun 2021
Ilikuwa na manufaa?