Siri kutoka kwa Mwenyeji Bingwa wa muda mrefu

Mwenyeji Bingwa Nikki anashiriki vidokezi vyake, kuanzia kuweka mpangilio mpaka kuonekana.
Na Airbnb tarehe 3 Mac 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 3 Mac 2020

Vidokezi

  • Mawasiliano ni kanuni ya 1 ya ukaribisho mzuri

  • Onekana kupitia picha nzuri, maelezo ya kina na matarajio ya wazi kwa ajili ya wageni

  • Anza na bei ya chini ili kupata nafasi zinazowekwa na uondoe maongezeko yoyote makubwa ya bei ili kuchochea tathmini nzuri

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

Nikki alikuwa mmoja wa wenyeji wa kwanza kwenye Airbnb kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa mpango huo ulipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2014. Amedumisha hadhi hiyo kwa zaidi ya robo 16 mfululizo.

Nikki hufanyaje? Alijifunza kukaribisha wageni kuanzia mwanzo hadi juu, akianza na nyumba ndogo ya shambani katika ua wake wa nyuma huko San Francisco. Tangazo hilo moja lilifanya vizuri sana kiasi kwamba akasukumwa kupanua na kuanza kupangisha nyumba yake nzima yenye vyumba vitatu vya kulala wakati wa likizo za familia.

Hapa, Nikki anashiriki siri za mafanikio yake ya Mwenyeji Bingwa.

Kuanza kama mwenyeji

"Miaka sita iliyopita, nilikaa katika nyumba yangu ya kwanza kwenye Airbnb huko Provence, Ufaransa na niliipenda. Ilikuwa studio ndogo sana katika mji wa kale wa Aix. Ilitimiza mahitaji yetu vizuri sana, lakini wenyeji hawakuwa wamejitahidi kuifanya iwe ya kupendeza au kufanya chochote. Niligundua kwamba ikiwa ningaliweka kiasi fulani cha pesa ndani yake, ningaliweza kutengeneza kitu maalumu kwa kutumia nyumba ndogo ya wageni ya futi 200 za mraba katika ua wangu. Nilidhani ingewekewa nafasi mara chache tu, lakini nilishangaa wakati iliwekewa nafasi mara moja kwa wiki nzima."

Kuwekewa nafasi haraka

"Kila ninapoweka tangazo mtandaoni, naanza na bei ya awali ya tangazo ambayo ni asilimia 50-70 tu ya kiwango cha soko, hadi nitakapokuwa na angalau tathmini tatu (au hadi nitakapopata maombi mengi mno ya kuweka nafasi kiasi cha kuweza kuongeza bei ifikie viwango vya soko). Ninafanya hivyo ili niweze kuondoa maongezeko bila kuharibu tathmini nzuri na kwa sababu ni muhimu kupata tathmini kadhaa haraka iwezekanavyo ili tangazo liweze kuonekana juu katika viwango vya utafutaji."

Kuandaa sehemu yenye makaribisho

"Yote huanza na sehemu nzuri. Lazima iwe safi. Ninapenda sehemu zangu ziwe wazi na zenye hewa ya kutosha. Isiwe na mparaganyo, lakini iwe na sehemu za ubunifu wa kuzingatiwa ambazo zinatoa maeneo ya kupumzisha macho yako. Pia lazima iwe yenye starehe, hasa vitanda. Ninawekeza katika magodoro ya sponji ya kukumbukwa na watu wanayapenda. Kwa kweli hiyo ni fadhili. Unatembea kwenye sehemu hiyo na kufikiria jinsi ambavyo watu wataitumia, kisha uweke dhana ya ubunifu kwenye sehemu hiyo."

Kuonekana kwenye Airbnb

"Kuwa na picha nzuri huleta tofauti. Picha za kitaalamu ni lazima. Ninafikiria kuhusu sehemu hiyo, kama ni sehemu ya familia au inafaa zaidi aina fulani ya msafiri nami huweka hayo katika kichwa. Andika maelezo mazuri sana ambayo ni ya kina na ya kukaribisha, ili umvutie mtu aingie kwenye tangazo. Eleza vitanda, vitambaa, majina ya chapa ya aina maalumu ya sabuni au vistawishi unavyotoa."

Kuweka matarajio ya wageni

"Katika tangazo lako, hakikisha umejumuisha maelezo ya vitu vya kipekee vya nyumba yako. Elezea vitu hivyo kwa njia ambayo ni ya uaminifu na wazi, bila kuvunja moyo. Unahitaji kuonyesha uwazi wa kutosha ili kuwasaidia wageni wako wachague nyumba wanayoitaka."

Kuwa mtu unayewasiliana vizuri

"Kwangu, mawasiliano ni kanuni ya 1 ya kukaribisha wageni vizuri. Mawasiliano yako ya moja kwa moja na mgeni huanza na maulizo ya kwanza. Siku zote mimi huwauliza wageni watarajiwa maswali machache ya ufuatiliaji baada ya kila ombi la kuweka nafasi, lengo si kuwa mkorofi au mdadisi, lakini ili kuhakikisha tu kwamba nyumba hiyo inawafaa. Kiukweli, unaanza mchakato wa kupata tathmini ya nyota 5 wakati huo."

Kwangu, mawasiliano ni kanuni ya 1 ya kukaribisha wageni vizuri.
Nikki,
San Francisco

Faida za kushangaza za kuwa mwenyeji

"Cha kushangaza sana kwangu ni jinsi ambavyo wageni wamekuwa wazuri. Watu wamekuwa waaminifu sana na wema na wenye kuelewa. Na kwa upande wa uchumi, nilishangazwa na mapato. Sikuingia katika hili nikitarajia kufanya vizuri sana, sembuse kuigeuza kuwa kazi. Nimezingatia mambo ninayopenda sana kuhusu kukaribisha wageni na kufuatilia fursa nilipoziona na matokeo yake yamekuwa mazuri sana."

Vidokezi

  • Mawasiliano ni kanuni ya 1 ya ukaribisho mzuri

  • Onekana kupitia picha nzuri, maelezo ya kina na matarajio ya wazi kwa ajili ya wageni

  • Anza na bei ya chini ili kupata nafasi zinazowekwa na uondoe maongezeko yoyote makubwa ya bei ili kuchochea tathmini nzuri

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni
Airbnb
3 Mac 2020
Ilikuwa na manufaa?