Mpango mpya na ulioboreshwa wa AirCover kwa ajili ya Wenyeji

Ulinzi kamili. Unajumuishwa kila wakati, bila malipo. Kwenye Airbnb pekee.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2022
Inachukua dakika 5 kusoma
Imesasishwa tarehe 21 Jul 2023

Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Airbnb 2022 Toleo la Novemba. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu toleo letu la hivi karibuni.

AirCover kwa ajili ya Wenyeji hutoa ulinzi kamili kila wakati unapoweka eneo lako kwenye Airbnb. Sasa inajumuisha ulinzi zaidi, pamoja na uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni, ukaguzi wa nafasi iliyowekwa, ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3, ulinzi kwa ajili ya vitu vyako vya thamani na ulinzi kwa ajili ya magari na boti zilizoegeshwa kwenye nyumba yako.

Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni

Uaminifu wa jumuiya yetu unatokana na kujua kwamba Wenyeji na wageni wako jinsi wanavyodai kuwa. Tunapanua uthibitishaji wa utambulisho kwa wageni wote wanaoweka nafasi ya kusafiri kwenda katika nchi na maeneo 35 maarufu ya Airbnb, yakiwakilisha asilimia 90 ya nafasi zote zilizowekwa. Tutapanua uthibitishaji wa utambulisho duniani kote mapema mwaka 2023, ikijumuisha asilimia 100 ya nafasi zetu zilizowekwa.

Tutaendelea kufanya uchunguzi wa historia ya wageni wote nchini Marekani kabla ya ukaaji wao wa kwanza na tutaangalia ikiwa wageni wote wanaoweka nafasi wako kwenye orodha fulani za uangalizi au orodha za vikwazo.

Kama sehemu ya uthibitishaji wetu uliopanuliwa wa utambulisho wa wageni, tumefanya pia mabadiliko kadhaa kwenye matakwa ya Kuweka Nafasi Papo Hapo. Pata maelezo zaidi

Pata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni

Teknolojia ya ukaguzi wa nafasi iliyowekwa

Tunazindua teknolojia inayomilikiwa ya ukaguzi wa nafasi iliyowekwa, ambayo husaidia kupunguza uwezekano wa sherehe zenye kuvuruga na uharibifu wa nyumba, nchini Marekani na Kanada. Tulijaribu ukaguzi wa nafasi zilizowekwa nchini Australia na tukapata sherehe zisizoidhinishwa zilishuka kwa takribani asilimia 35 wakati wa majaribio hayo.

Teknolojia yetu ya ukaguzi inatathmini takribani mambo 100 ya nafasi iliyowekwa na inazuia baadhi ya nafasi zilizowekwa ili kusaidia kupunguza uwezekano wa sherehe zenye kuvuruga na uharibifu wa nyumba. Tunapanga kupanua hii kwa nafasi zote zilizowekwa kote ulimwenguni mapema mwaka 2023.

Pata maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya ukaguzi wa nafasi zilizowekwa

Ulinzi zaidi wa uharibifu

Kwa zaidi ya muongo mmoja, Airbnb imetoa ulinzi dhidi ya uharibifu unaoongoza kwenye tasnia kwa Wenyeji wetu. Leo, tunaongeza ulinzi huu kwenye AirCover kwa ajili ya Wenyeji:

  • Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3: Tunaongeza ulinzi dhidi ya uharibifu mara tatu kutoka USD milioni 1 hadi USD milioni 3, unaolinda nyumba yako pamoja na vitu vilivyomo.
  • Ulinzi wa sanaa na vitu vya thamani: Tunalinda aina mbalimbali za sanaa, vito na vitu vya kukusanywa, ambavyo vinaweza kurekebishwa au kubadilishwa kwa thamani iliyokadiriwa ikiwa vimeharibiwa.
  • Ulinzi wa magari na boti: Tunatoa ulinzi dhidi ya uharibifu wa magari, boti na vyombo vingine vya majini ambavyo unaegesha au kuhifadhi kwenye nyumba yako.

Ulinzi mpya ni kuongezea kwenye vipengele hivi ambavyo tayari vimejumuishwa kwenye AirCover kwa ajili ya Wenyeji:

  • Mawasiliano ya usalama saa 24: Endapo utajihisi kwamba hauko salama, programu yetu inakupa ufikiaji wa mbofyo mmoja kwa maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.
  • Ulinzi dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi: Tunalipia uharibifu unaofanywa na wanyama vipenzi
  • Kufanya usafi wa kina : Tunafidia kwa ajili ya huduma za kufanya usafi wa ziada zinazohitajika ili kuondoa madoa na harufu ya moshi.
  • Ulinzi dhidi ya hasara ya mapato: Tunakufidia mapato yaliyopotea iwapo utaghairi nafasi zilizowekwa za Airbnb ambazo zimethibitishwa kwa sababu ya uharibifu wa mgeni.
Pata maelezo zaidi kuhusu ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji

Mchakato rahisi wa kufidia

Ulituambia mchakato wa kufidiwa ulikuwa mgumu sana. Kulingana na maoni yako, tumerahisisha mchakato wetu wa kutoa fidia.

Ikiwa mgeni ataharibu eneo au mali zako, unaweza kutembelea Kituo chetu cha Usuluhishi ili kuwasilisha ombi la kufidiwa kwa hatua chache tu, kisha ufuatilie kwa urahisi mchakato huo kuanzia kuwasilisha hadi kupokea malipo. Ombi lako litatumwa kwanza kwa mgeni. Mgeni asipojibu au kulipa ndani ya saa 24, utaweza kuihusisha Airbnb.

Wenyeji Bingwa (walio na matangazo nje ya jimbo la Washington nchini Marekani) pia hupata uelekezaji uliopewa kipaumbele na urejeshaji wa fedha wa haraka.

Bima ya dhima ya Mwenyeji ya USD milioni 1

Bima ya dhima ya Mwenyeji, ambayo ni sehemu ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji, hukulinda katika tukio nadra ambapo mgeni atajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa akiwa anakaa kwenye eneo lako. Watu wanaokusaidia kukaribisha wageni, kama vile Wenyeji Wenza na wafanya usafi, pia wamejumuishwa katika bima hii.

Bima ya dhima ya Mwenyeji hukufidia ikiwa utapatikana kuwa na wajibu kisheria kwa:

  • Jeraha la mwili kwa mgeni (au wengine)
  • Uharibifu au wizi wa mali ya mgeni (au wengine)
  • Uharibifu unaosababishwa na mgeni (au wengine) kwenye maeneo ya pamoja, kama vile kumbi za majengo na nyumba zilizo karibu

Ikiwa unahitaji kuwasilisha madai, tumia tu fomu yetu ya kujiunga na bima ya dhima. Tutatuma taarifa unayotoa kwa kampuni ya nje ya bima inayoaminika, ambayo itampa mwakilishi ashughulikie madai yako. Atatatua madai yako kulingana na masharti ya sera ya bima.

Ikiwa wewe ni Mwenyeji wa Tukio, unalindwa na bima yetu ya dhima ya Matukio.

Pata maelezo zaidi kuhusu bima ya dhima ya Mwenyeji

AirCover kwa ajili ya Wenyeji ya Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, Bima ya dhima ya Mwenyeji na Bima ya dhima ya Matukio haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini Japani, ambapo Bima ya Mwenyeji ya Japani na Bima ya Ulinzi ya Tukio ya Japani zinatumika au Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel LLC. Kwa Wenyeji waliotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini China Bara, Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China unatumika. Kumbuka kwamba vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD.

Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio inadhaminiwa na watoa bima wengine. Ikiwa unakaribisha wageni nchini Uingereza, sera za bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Tukio zinatolewa na Zurich Insurance Company Ltd. na zinapangwa na kutekelezwa bila gharama ya ziada kwa Wenyeji wa Uingereza na Airbnb UK Services Limited, mwakilishi aliyeteuliwa wa Aon UK Limited, ambao wameidhinishwa na kudhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha. Nambari ya usajili ya Aon katika FCA ni 310451. Unaweza kuangalia maelezo haya kwa kutembelea Rejesta ya Huduma za Fedha au uwasiliane na FCA kupitia nambari 0800 111 6768. Sera za dhima ya Mwenyeji na Matukio ndani ya Aircover kwa ajili ya Wenyeji zinadhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Fedha, bidhaa na huduma zilizosalia si huduma zinazodhibitiwa zilizopangwa na Airbnb UK Services Limited. FPAFF609LC

Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si bima na hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji. Kwa matangazo katika Jimbo la Washington, wajibu wa kimkataba wa Airbnb chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unalindwa na sera ya bima iliyonunuliwa na Airbnb. Kwa Wenyeji ambao nchi yao ya makazi ni tofuati na Australia, Masharti haya ya Ulinzi dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji yanatumika. Kwa Wenyeji ambao nchi yao makazi ni nchini Australia, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na Masharti ya Ulinzi Dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji kwa Watumiaji wa Australia.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
11 Mei 2022
Ilikuwa na manufaa?