Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Tunawaletea AirCover

  Ulinzi kamili. Bila malipo kwa kila Mwenyeji. Kwenye Airbnb pekee.
  Na Airbnb tarehe 9 Nov 2021
  video ya dakika 5
  Imesasishwa tarehe 10 Nov 2021

  Vidokezi

  • AirCover inajumuisha USD milioni 1 za ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji na USD milioni 1 za bima ya dhima ya Mwenyeji

  • Ulinzi dhidi ya uharibifu unajumuisha ulinzi wa upotezaji wa mapato, pamoja na ulinzi mpya dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi, kufanya usafi wa kina na kadhalika

  • AirCover inajumuishwa kila wakati na haina malipo kila wakati—kwenye Airbnb pekee

  Wenyeji wetu ndio kiini cha Airbnb. Kukusikiliza ni muhimu kwenye kazi yetu na ni maoni ndiyo yaliyotuelekeza kusasisha mipango yetu ya ulinzi wa Mwenyeji na kuunda AirCover—ulinzi kamili, bila malipo kwa kila Mwenyeji, kwenye Airbnb pekee.

  Umetuambia katika vikao vya kusikiliza, katika warsha, kwenye Kituo cha Jumuiya na kupitia Bodi ya Ushauri ya Wenyeji kwamba unahitaji ulinzi zaidi: Je, itakuwaje ikiwa mgeni anavuta sigara katika sehemu yako na unahitaji kufanya usafi maalumu? Je, itakuwaje ikiwa mbwa wa mgeni ametafuna sehemu ya sofa yako na unahitaji kuirekebisha?

  Umetuambia pia kwamba mchakato wa kulipa si wa moja kwa moja kila wakati na kwamba lilikuwa jambo la kuhangaisha kuwasilisha maombi yako ya kulipwa kabla ya mgeni wako aliyefuata kuingia.

  Tumekusikia na tunafurahi kushiriki AirCover. Kando na USD milioni 1 za ulinzi wa dhima, AirCover inaongeza USD milioni 1 za ulinzi dhidi ya uharibifu ambao Wenyeji wanapata, pamoja na ulinzi mpya dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi, kufanya usafi wa kina na kadhalika.

  Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 1

  Ikiwa eneo au mali yako itawahi kuharibiwa na mgeni wakati wa ukaaji wa Airbnb, AirCover itakupa ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 1. Tayari tumekulinda ikiwa mgeni ataharibu zulia lako kwa kumwaga mvinyo mwekundu na sasa, kupitia ulinzi ulioongezwa, tutagharamia iwapo paka wa mgeni atakwaruza mapazia yako.

  Ulinzi ulioongezwa unajumuisha:

  • Ulinzi dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi: Usijali—uharibifu unaofanywa na wanyama vipenzi umelindwa
  • Ulinzi dhidi ya kufanya usafi wa kina: Tunakufidia gharama za kufanya usafi usiotarajiwa, kama vile kuondoa harufu ya sigara ikiwa mgeni anavuta sigara nyumbani kwako.
  • Ulinzi dhidi ya hasara ya mapato: AirCover hufidia upotezaji wa mapato iwapo utaghairi nafasi zilizowekwa ambazo zimethibitishwa za Airbnb kwa sababu ya uharibifu wa mgeni
  • Kipindi cha siku 14 za kuwasilisha maombi: Ikiwa wageni watasababisha uharibifu, una siku 14 za kuomba kufidiwa baada ya wao kutoka—haijalishi ikiwa wageni wapya tayari wameingia.
  • Malipo ya haraka zaidi: Wenyeji hupokea malipo ya haraka zaidi kwa ajili ya uharibifu wa wageni (siku 9 kwa wastani)
  • Ufuatiliaji wa haraka zaidi kwa Wenyeji Bingwa: Sasa unapata uelekezaji uliopewa kipaumbele na malipo ya haraka zaidi

  Iwapo unahitaji kuomba kulipwa, tuma tu ombi la AirCover kwenye Kituo chetu cha Usuluhishi. Ukishatuma ombi lako, tutamjulisha mgeni wako kuhusu kilichoharibika au kukosekana. Mgeni wako basi ana saa 72 za kulipa kiasi unachoomba. Iwapo atakataa kulipa kiasi kamili au hatajibu, utaweza kuhusisha Airbnb Usaidizi.

  Pata maelezo zaidi kuhusu ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji

  Bima ya dhima ya Mwenyeji ya USD milioni 1

  Bima ya dhima hutumika kwa Wenyeji katika tukio nadra ambapo mgeni atajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa akiwa anakaa kwenye eneo lako. Watu wanaokusaidia kukaribisha wageni, kama vile Wenyeji Wenza na wasafishaji, pia wamejumuishwa, kwa hivyo unaweza kuwa na uhakika unapokaribisha wageni kwenye Airbnb.

  Bima ya dhima ya Mwenyeji hukufidia ikiwa utapatikana kuwa na wajibu kisheria kwa:

  • Jeraha la mwili kwa mgeni (au wengine)
  • Uharibifu au wizi wa mali ya mgeni (au wengine)
  • Uharibifu unaosababishwa na mgeni (au wengine) kwenye maeneo ya pamoja, kama vile kumbi za majengo na nyumba zilizo karibu

  Ikiwa unahitaji kuwasilisha madai, nenda tu kwenye fomu yetu ya usajili wa bima ya dhima. Taarifa hiyo itatumwa kwa kampuni inayotupa huduma ya bima inayoaminika ya ulinzi dhidi ya uharibifu unaosababishwa na mhusika mwingine, ambayo itampa mwakilishi ashughulikie madai yako. Atatatua madai yako kulingana na masharti ya sera ya bima.

  Ikiwa wewe ni Mwenyeji wa Tukio, unalindwa chini ya bima yetu ya dhima ya Matukio.

  Pata maelezo zaidi kuhusu bima ya dhima ya Mwenyeji

  AirCover imehamasishwa na maoni yako—lakini bado hatujamaliza. Tumejizatiti kutenda kulingana na maoni yako na tunakuhimiza uendelee kutupa mawazo yako.

  Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel, LLC au Wenyeji katika China Bara na nchini Japani, ambapo Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China, Bima ya Mwenyeji ya Japani na Bima ya Ulinzi ya Tukio ya Japani hutumika. Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji.

  Kumbuka kwamba vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD na kwamba kuna vigezo, masharti na vighairi vingine.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • AirCover inajumuisha USD milioni 1 za ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji na USD milioni 1 za bima ya dhima ya Mwenyeji

  • Ulinzi dhidi ya uharibifu unajumuisha ulinzi wa upotezaji wa mapato, pamoja na ulinzi mpya dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi, kufanya usafi wa kina na kadhalika

  • AirCover inajumuishwa kila wakati na haina malipo kila wakati—kwenye Airbnb pekee

  Airbnb
  9 Nov 2021
  Ilikuwa na manufaa?