Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Jinsi ya kuweka sheria za nyumba zinazofaa

  Saidia kulinda nyumba yako na kuunda huduma bora kwa wageni.
  Na Airbnb tarehe 1 Des 2020
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 21 Nov 2022

  Vidokezi

  • Sheria za nyumba zinaonekana kwenye ukurasa wa tangazo lako na wageni lazima wakubaliane nazo ili waweke nafasi kwenye eneo lako

  • Unaweza kuongeza sheria za ziada ili kushughulikia desturi za mahali ulipo au wasiwasi wa afya na usalama

  Sheria za nyumba yako zinaweka maratajio kwa wageni na kuwadokezea mtindo wako wa kukaribisha wageni. Pia huwasaidia wageni watathmini iwapo sehemu yako inawafaa kabla ya kuiwekea nafasi.

  Kuchagua sheria za kawaida za nyumba yako

  Wenyeji wanaweza kuchagua kutoka katika seti ya sheria za kawaida za nyumba katika maeneo yafuatayo:

  • Wanyama vipenzi
  • Matukio
  • Uvutaji sigara, uvutaji wa mvuke wa sigara za kielektroniki na sigara za kielektroniki
  • Saa za utulivu
  • Nyakati za kuingia na kutoka
  • Idadi ya juu ya wageni
  • Kupiga picha na kurekodi video za kibiashara

  Sheria za nyumba yako zinaangaziwa katika maeneo manne: kwenye ukurasa wa tangazo lako, kwenye skrini wakati wageni wanaweka nafasi kwenye sehemu yako na kwenye barua pepe ya Fungasha Mizigo Yako pamoja na Mwongozo wa Kuwasili ambao wageni hupokea kabla ya safari yao.

  Kuandika sheria za ziada

  Ikiwa una matakwa maalumu ambayo hayajajumuishwa kwenye seti ya sheria za kawaida za nyumba, kama vile ikiwa sehemu yako ni eneo lisiloruhusu uvaaji wa viatu, unaweza kuyaandika chini ya sheria za ziada.

  Ni jambo la busara kuepuka kuwachosha wageni kwa kuwapa sheria nyingi kupita kiasi, lakini unaweza kuongeza chochote muhimu kuhusu desturi za mahali ulipo au afya na usalama. Hii ni mifano michache kutoka kwa Wenyeji:

  • "Tunaomba uwe kimya na mwenye busara, hasa usiku au wakati wa usingizi wa mchana." —Beatriz Elena, Medellin, Kolombia
  • "Tafadhali funga na uweke kufuli kwenye madirisha na milango yote unapoondoka chumbani." —Dave na Deb, Edmonton, Kanada
  • “Tafadhali usiweke chakula chochote kwenye chumba cha kulala.” —Momi, Honolulu.

  Sheria za nyumba husaidia kukulinda

  Ukiwa na sheria za msingi, sheria yoyote unayochagua kutoka kwenye orodha ya sheria za kawaida za nyumba inaweza kutekelezwa. Ikiwa mgeni atakiuka sheria ya nyumba, hatua yako ya kwanza inapaswa kuwa kuwasiliana na mgeni huyo kisha ujaribu kutatua tatizo hilo moja kwa moja. Ikiwa utashindwa kutatua tatizo hilo, wasiliana na kituo cha Usaidizi wa Jumuiya ili upate usaidizi.

  Sheria zote za nyumba lazima zipatane na sera na masharti ya Airbnb, ikiwemo masharti yetu ya huduma na sera ya kutobagua.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Sheria za nyumba zinaonekana kwenye ukurasa wa tangazo lako na wageni lazima wakubaliane nazo ili waweke nafasi kwenye eneo lako

  • Unaweza kuongeza sheria za ziada ili kushughulikia desturi za mahali ulipo au wasiwasi wa afya na usalama

  Airbnb
  1 Des 2020
  Ilikuwa na manufaa?