Vistawishi ambavyo wageni wanavitaka

Fanya tangazo lako lionekane kupitia vipengele na vistawishi hivi maarufu.
Na Airbnb tarehe 19 Nov 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 21 Nov 2023

Wageni mara nyingi wanachuja matokeo ya utafutaji ya Airbnb ili kupata maeneo yenye vipengele na vistawishi mahususi. Unaweza kusaidia tangazo lako lionekane zaidi kwa kujumuisha kila kitu ambacho nyumba yako onato.

Vistawishi maarufu

Hivi ni vistawishi ambavyo wageni watafuta mara nyingi.*

  1. Bwawa

  2. Wi-Fi

  3. Jiko

  4. Maegesho ya bila malipo

  5. Beseni la maji moto

  6. Kiyoyozi au kipasha joto

  7. Mashine ya kufua au kukausha

  8. Huduma ya kuingia mwenyewe

  9. Televisheni au televisheni ya kebo

  10. Meko

Ni rahisi kuweka vistawishi katika kichupo cha Matangazo cha akaunti yako ya kukaribisha wageni. Nenda tu kwenye Sehemu yako na Vistawishi, kisha uguse alama ya jumlisha. Chagua Weka mbele ya kipengele chochote ambacho nyumba yako inacho. Unaweza pia Kuunda ziara ya picha na kuweka maelezo kulingana na chumba, ikiwemo vistawishi, taarifa za faragha, na mipangilio ya kulala.

    Vitu muhimu

    Wageni wanatarajia sehemu yako iwe na vitu hivi muhimu kwa ajili ya ukaaji wa kustarehesha:

    • Karatasi ya choo

    • Sabuni ya mkono na mwili

    • Taulo moja kwa kila mgeni

    • Mto mmoja kwa kila mgeni

    • Mashuka kwa kila kitanda cha mgeni

    Fikiria kutoa kiasi kikubwa kwa ajili ya makundi makubwa na sehemu za kukaa za muda mrefu. Unaweza kuwatumia wageni wako ujumbe ili kuwauliza wanachohitaji.

    Usalama wa wageni

    Tahadhari chache za msingi zinaweza kusaidia kupunguza hatari nyumbani kwako.

    Tunawahimiza sana Wenyeji wote waweke ving'ora vya moshi na kaboni monoksidi katika sehemu zinazotumia vifaa vya kuchoma mafuta. Unaweza pia kutoa kizima moto na sanduku la huduma ya kwanza.

    Pata maelezo zaidi kuhusu kuandaa nyumba yako

    Vipengele vya ufikiaji

    Wageni walio na mahitaji ya ufikiaji mara nyingi wanatafuta vipengele kama vile mlango wa kuingia usiokuwa na ngazi, vyuma vya kujishikia bafuni vilivyofungwa na maegesho yanayofikika. Kujumuisha vipengele hivi katika tangazo lako huwasaidia wageni kujua ikiwa eneo lako linawafaa.

    Soma miongozo yetu ya vipengele vya ufikiaji

    Sehemu za kufanyia kazi mbali na ofisini

    Wageni wanaofanya kazi wakiwa mbali wakiwa safarini wanathamini vipengele na vistawishi kama vile:

    • Wi-Fi ya kasi na ya kuaminika
    • Sehemu mahususi ya kufanyia kazi
    • Vifaa vya kujali afya ya mgongo, kama vile stendi ya kompyuta mpakato
    • Mwangaza mzuri
    • Vifaa vya ofisi, pamoja na kalamu, karatasi na chaja ya jumla

    Pata maelezo zaidi kuhusu kuwezesha kufanyia kazi mbali na ofisi

    Vipengele vinavyowafaa watoto na wanyama vipenzi

    Karibisha wageni zaidi wenye watoto au wanyama vipenzi kwa kutoa vitu muhimu kama vile:

    • Kiti cha watoto kukalia wanapokula
    • Kitanda cha mtoto cha safari
    • Milango ya usalama wa watoto
    • Vifuniko vya fanicha
    • Mabakuli ya chakula na maji kwa ajili ya wanyama vipenzi
    • Taulo za kufuta miguu ya wanyama vipenzi mlangoni
    • Vifaa vya ziada vya kufanyia usafi

    Hakikisha unaonyesha mabadiliko ambayo umefanya kwa kusasisha vistawishi vyako, maelezo ya tangazo na picha. Kuweka vitu vichache tu vinavyotafutwa sana kunaweza kusaidia katika kuwafanya wageni wahisi wamestareheka zaidi katika sehemu yako na kunaweza kusababisha tathmini nzuri.

    *Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb ambazo zilipima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi ulimwenguni kote kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba, 2022.

    Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
    Airbnb
    19 Nov 2020
    Ilikuwa na manufaa?