Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Kuunda mpango wa biashara ya kukaribisha wageni

Badilisha nyumba yako ili ikufaidi kwa msaada wa hivi vidokezi vitano vya Mwenyeji Bingwa.
Na Airbnb tarehe 19 Jul 2019
Inachukua dakika 9 kusoma
Imesasishwa tarehe 7 Jun 2021

Vidokezi

  • Andaa kauli ya dhamira ili uanze

    • Angalia matangazo ya mahali ulipo ili upate kichocheo

    • Tengeneza bajeti ili uendelee kufuata malengo yako ya kukaribisha wageni

    • Mruhusu rafiki akae katika sehemu yako ili akupe maoni kabla ya mgeni wako wa kwanza kufika

    • Jaribu teknolojia, kama vile programu na makufuli janja, ili zikusaidia unapokaribisha wageni

    Nick na Sarah Roussos-Karakaian ni timu ya mume na mke ambao ni Wenyeji Bingwa (@nestrs) ambao wamefanya ukaribishaji wa wageni kuwa biashara ya wakati wote mjini Columbus, Ohio. Baada ya kutangaza chumba chao cha chini Jiji la New York kwenye Airbnb mnamo 2012, hawajaacha. Tangu wakati huo, wameifanya kuwa kazi yao kuu. Sarah pia ni mtangazaji mwenza katika podikasti "Thanks for Visiting,” ushauri kwa wenyeji gwiji na wanaoanza. Hapa, wanashiriki maarifa na vidokezi vya jinsi ya kuanzisha biashara ya Airbnb.

    Sarah: “Kwetu, ilianzia Queens, New York. Nilikuwa mwigizaji. Pia nilikuwa nikifanya kazi kwenye baa mara nyingi.”

    Nick: “Na mimi nilikuwa nikifanya mazoezi ya kazi kwa vitendo mwenye shahada ya uzamili katika usanifu na hata sikuwa na uwezo wa kutosha kujikimu…”

    Sarah: “Na sote tulitaka sana kumiliki nyumba lakini hatukujua namna ya kufanya hivyo. Siku moja, niliona nyumba ndogo—ilikuwa ndogo zaidi katika eneo ilipokuwa na ilikuwa ghali kwetu—lakini nilikuwa nimeamua kutafuta njia ya kuipata.”

    Nick: “Kutokana na elimu sahihi ya kifedha, akiba na msaada kutoka kwa familia, tuliweza kupata mkopo.”

    Sarah: “Na wakati haya yote yakiendelea, nilikuja kufahamu kwamba rafiki yangu alikuwa akitangaza chumba katika nyumba yake kwenye Airbnb. Hali iliyokuwa ikimsaidia kulipia kodi yake Jijini New York—yaani nilishangaa sana. Si watu wengi walikuwa wanajua kuhusu Airbnb wakati huo. Nilimwambia Nick kuhusu uwezekano wa sisi kutangaza nyumba yetu na akawa anasita—lakini mimi nikawa ninavutiwa. Tukaamua kujaribu na huo ukawa ndio mwanzo.”

    Nick: “Nakumbuka nilikuwa nikiosha vyoo na nilifurahia sana kufanya hivyo. Kazi hiyo ilikuwa ikilipa rehani yetu ya nyumba kwa hivyo nilijiambia: ‘Bila shaka, inapendeza! Inawezekana kufanya hivi hata zaidi?’”

    Sarah: “Niliweza kuleta uzoefu wangu mwingi wa ukarimu nilioupata nilipofanya kazi katika hoteli za kifahari—na ilinipendeza. Baada ya miaka minne ya kuwa mwenyeji na kumiliki nyumba jijini New York, tulibahatika kubishiwa mlango na mwekezaji ambaye alitaka kununua nyumba yetu, pamoja na vyote vilivyokuwemo.”

    Nick: “Baada ya kujishauri na kuangalia karatasi ndefu ya maeneo ambayo tungeweza kwenda, pamoja na safari za kuzunguka nchi nzima tukiongea na wenyeji, tulijikuta tukiwa Columbus, Ohio.”

    Sarah: “Kuweza kuchanganya usanifu, ukarimu na kuwa na nyumba—pamoja na kuwa na uhuru wa kujifanyia uamuzi wetu wenyewe wa ubunifu—ni kutimia kwa ndoto. Ndiyo sababu tuna shauku kubwa ya kuwasaidia wengine kujifunza jinsi ya kuwa wenyeji.”

    1. Anza kwa kauli ya dhamira

    Sarah: “Kabla ya kuanza, tunapendekeza ujiandalie kauli ya dhamira. Itaongoza maadili na nyendo zako, jambo ambalo husaidia sana wakati ambapo huenda huna uhakika kuhusu mwelekeo au uamuzi. Kauli yako ya dhamira inaweza kukusaidia uelekee sehemu sahihi. Pia itabaini jinsi unavyounda na kusanifu sehemu yako.”

    Nick: “Wakati unaunda kauli ya dhamira, chukua muda ujiulize maswali kadhaa:

    • Ni nini kinachokupa motisha?
    • Je, maadili yako ni nini?
    • Je, unataka kufanya kazi vipi?
    • Una maono gani?
    • Una malengo gani?”

    Sarah: “Sisi maono yetu ni kubadili sehemu za kukaa ili tuweze kubadili maisha. Tunajaribu kukumbuka hilo katika kila kitu tunayofanya.”

    2. Tafiti soko

    Nick: “Kabla ya kuanza, ni muhimu kufanya utafiti wako na kuangalia ushindani katika eneo lako. Utafiti huu wa awali utabainisha jinsi unavyosanifu, kujiweka na kuuza sehemu yako.

    • Zingatia watu unaowalenga. Je, ni nani anayeweza kuweka nafasi ya kukaa katika sehemu yako? Kwa mfano, kwe upande wetu, Columbus ni mji wa vyuo vikuu kwa hivyo tumefanya sehemu zetu kuwajali wazazi wanaowatembelea watoto wao.
    • Tathmini vistawishi vyako. Je, unaruhusu wanyama vipenzi? Je, una eneo la kuegesha magari au bwawa la kuogelea? Je, sehemu yako imepambwa kwa upekee? Chochote kinachoinua sehemu yako japo kwa udogo, pia kinakupa uwezekano wa kutoza zaidi.
    • Tafuta mtandaoni uone matangazo mengine ya Airbnb, hoteli na ukodishaji wa muda mfupi karibu nawe. Je, ni vitu gani vinapatikana? Wanatoza kiasi gani cha pesa? Je, kuna njia ambayo unaweza kutumia kujitofautisha?
    • Unda mkakati wa bei. Ili kusaidia kuongeza viwango vyako vya ukaaji wakati unapoanza, tumia nyenzo ya Airbnb ya Upangaji Bei Kiotomatiki, ambayo hukuruhusu kubadilisha bei zako kiotomatiki kati ya siku za wiki na wikendi.”

    3. Panga bei ili kupata faida

    Sarah: “Kuunda bajeti, ingawa kunaweza kuwa hakupendezi sana, ni muhimu sana. Tunapendekeza utumie programu ya excell na upange gharama zako katika vikundi vitatu:

    Gharama za kabla: Huu ndio uwekezaji wa kwanza unaofanya katika sehemu yako kabla ya mtu yeyote kuitembelea, kama vile ukarabati, mapambo, samani na upigaji picha.

    • Inashauriwa kuwekeza katika mapambo. Si lazima ununue kutoka kwa wanaouza ghali au kuwa na kila kitu cha fahari zaidi. Fanya tu sehemu yako iwe ya kuvutia. Tafuta vitu katika magulio au kuwa mbunifu na ufanye jambo tofauti kwa rangi au mandhari—ni haya ndiyo yatakayovutia macho ya watu katika tangazo lako.
    • Huwa tunawashauri wenyeji wanaokaribisha wageni kwa mara ya kwanza wawekeze katika magodoro, makochi na mashuka mazuri. Kila mtu hujiangusha kwenye kitanda mara tu wanapoingia kwenye chumba cha hoteli—kwa hivyo hakikisha kitanda chako ni kizuri. Wakati mwingine huwa tunapata tathmini ya nyota 5 kutokana na kitandani pekee, tathmini hiyo itakusaidia kuongeza kiwango cha ukaaji.

    Gharama zinazojirudia: Vitu vya msingi vinavyotumiwa na wageni vinavyopaswa kuongezwa tena, vikiwemo bidhaa za bafuni, shashi, taulo za karatasi, betri na balbu.

    • Je, huwa unajumuisha nyongeza yoyote kama vile chupa za maji au kahawa?
    • Andaa orodha ya huduma zote unazohitaji na uhakikishe kuwa unaweza kumudu bei unazopata
    • Nunua kwa wingi kiasi kinachotosha miezi sita kwa wakati mmoja na ufuatilie matumizi yako katika programu ya excell
    • Kwa vitu kama mashuka, kumbuka kuzingatia ni mara ngapi ungependa kuyanunua katika mwaka mzima. Unashauriwa kuwa na mashuka mazuri na safi kwa ajili ya wageni wako kila wakati.

    Gharama za matengenezo na usimamizi: Hushughulikia kila kitu kinachohitajika ili kuhakikisha kwamba sehemu yako ni salama, yenye joto linalofaa na inafaa kwa ajili ya kuishi. Pia inajumuisha gharama za bustani na mwonekano wa nje. Je, utakuwa ukimlipa mtu wa kusafisha ili akusaidie kufanya mabadiliko au utamtegemea mwenyeji mwenza?

    Jumlisha takwimu hizi na uhakikishe kuwa unamudu gharama na kwamba malengo yako yanaweza kutumilika. Ikiwa hasabu hazilingiani, basi huenda itakupasa kuweka akiba zaidi kabla ili uweze kuandaa sehemu utakayoonea fahari.”

    4. Fikiria kama mgeni

    Sarah: “Hiki ni mojawapo ya vidokezi ambavyo huwa ninapenda kuwapa wanaokaribisha wageni, kwamba tafuta rafiki mwaminifu na mkweli aje akae katika sehemu yako. Unajua unaona nyumba yako siku baada ya siku na hata unaweza kusahau vitu ambavyo msafiri anaweza kuvihitaji—kama vile mswaki au dawa ya kupiga mswaki—au kasoro ya ubunifu ambayo imekupita. Rafiki anaweza akakusaidia kwa kukupa maoni kuhusu vitu hivyo vidogo lakini muhimu. Haitakuwa vyema kwa mgeni anayelipa kukuonyesha.”

    Nick: “Tunapenda kujumuisha kikapu cha ‘Je, umesahau kitu?’ ambamo huwa tunaweka bidhaa na vitu ambavyo wageni wanaweza kuhitaji dakika za mwisho. Kuwa na mawazo ya ukarimu ndio msingi wa biashara yako kufanikiwa. Ndiyo sababu watu huenda kwenye hoteli tofauti wanazopenda—kwa sababu wanajua cha kutarajia: sehemu inayohisi kana kwamba wao ndio wa kwanza kufika, taulo zilizokunjwa kwa uangalifu na wanajua wanaweza kutegemea kupata hata vitu vidogo kama vile chaja ya simu karibu na meza ya kitandani. Unashauriwa kuwa na kiwango sawa cha huduma kwa wageni wako ili watake kurudi tena na tena.”

    5. Ifanye kuwa ya Kiotomatiki

    Nick: “Kuwa mwenyeji kuna changamoto, lakini pia ni tofauti sasa ukilinganisha na ilivyokuwa Airbnb ilipoanza. Kuna teknolojia zaidi, zana, rasilimali na msaada wa kukuwezesha kupanga mchakato na kufanya maisha yako ya kuwa mwenyeji yawe rahisi kidogo.”

    Sarah: “Wenyeji wanapoanza, tunapendekeza wajifanyie mchakato wote wa kukaribisha kuanzia mwanzo hadi mwisho kwa kila ukaaji: kuanzia ujumbe wa mwanzo wa kuweka nafasi, kuwapokea wageni, kufanya usafi na mabadiliko. Baada ya kuelewa juu chini zake, basi unaweza kutumia mifumo mbalimbali otomatiki, kwa mfano:

    • Programu za kwenye wavuti: Kuna programu ambazo unaweza kutumia (kama vile IFTTT) ili kuratibu vianzisha matukio na kuunganisha zana dijiti. Kwa mfano, unapopata uthibitisho wa kuweka nafasi katika kikasha chako cha barua pepe, inaweza kutuma kikumbusho cha kalenda kiotomatiki kwako, kwa mwenzako, au kwa mtu anayesafisha.
    • Makufuli janja ni nguvu mpya. Wageni wanaweza kutumiwa nambari ya kipekee ambayo hufanya kazi tu kwa muda wa safari yao. Huruhusu wageni kuingia wenyewe, kwa hivyo huhituitaji kuratibu wakati wa kuwaruhusu waingie nyumbani. Tunaweza tu kushauriana nao katikati ya kipindi chao cha kukaa.
    • Kujiundia orodha kama zamani: Nina orodha ya mambo ya kufanya kila robo mwaka katika kila nyumba iliyo na vitu ninavyohitaji kufanya kwa ajili ya usalama na matengenezo, vitu kama vile kuangalia vichungi vya tanuru, kuhakikisha kuwa betri kwenye ving'ora vya moto zinafanya kazi, kufagia mivungu. Huwa ninachapisha orodha hiyo na kuitundika kwenye kabati la kando—kwa hivyo wakati ninatembelea nyumba fulani, ninaweza kujua hali yake katika mwaka.”

    Nick: “Kuwa na biashara ya Airbnb kunahitaji bidii. Lakini tunatamani sana kuwaonyesha watu kuwa kumiliki nyumba na kufanya biashara hii wakati wote kunawezekana—na kwamba kuna zaidi ya njia moja ya kufanya hivyo.”

    Sarah: “Unajua kwa upande wangu kulikuwa na badiliko la kazi na nilihofia kwamba nisingalipata chochote ambacho ningalipenda jinsi nilivyopenda kuigiza. Lakini Airbnb imebadili maisha yetu. Tunaweza kufanya maamuzi yetu wenyewe ya ubunifu, kuwa wamiliki wa biashara—yaani mambo yanazidi kunoga hata zaidi.”

    Nick: “Inaturuhusu kuendelea kuwa na uhuru na kufurahia maisha yetu hata zaidi. Tunataraji kuwa unaweza kupata njia ya kuanzisha biashara ya Airbnb na kuifanya iwe upendavyo. Ikiwa unahitaji ushauri zaidi, unaweza kuwasiliana nasi.”

    Furahia kuwa mwenyeji!
    Nick + Sarah, Nestrs

    Vidokezi

    • Andaa kauli ya dhamira ili uanze

      • Angalia matangazo ya mahali ulipo ili upate kichocheo

      • Tengeneza bajeti ili uendelee kufuata malengo yako ya kukaribisha wageni

      • Mruhusu rafiki akae katika sehemu yako ili akupe maoni kabla ya mgeni wako wa kwanza kufika

      • Jaribu teknolojia, kama vile programu na makufuli janja, ili zikusaidia unapokaribisha wageni

      Airbnb
      19 Jul 2019
      Ilikuwa na manufaa?