Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi ya kukaribisha wageni wako wa kwanza

  Hii ndiyo namna ya kuunda tukio zuri kwa wageni—mara ya kwanza na kila wakati.
  Na Airbnb tarehe 20 Nov 2019
  Inachukua dakika 7 kusoma
  Imesasishwa tarehe 9 Jun 2021

  Vidokezi

  • Maelekezo ya kuingia ya kisasa zaidi yanaweza kufanya kuwasili kwa wageni kuwa rahisi

  • Kuhakikisha sehemu yako ni safi kunasaidia wageni kuwa na ukaaji mzuri

  • Kupatikana kwa ajili ya wageni kunaweza kuwasaidia kujihisi kusaidiwa

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuwafurahisha wageni wako wa kwanza

  Unaweza kuhisi wasiwasi kidogo unapotarajia kuwasili kwa wageni wako wa kwanza. “Nilifurahi sana lakini pia nilikuwa na wasiwasi mwingi,” anasema Mwenyeji Colleen kutoka Richmond, Kanada. Lakini kwa haraka aligundua jinsi kuwa mwenyeji kunaweza kufurahisha na kuwa na tija. “Tulipendezwa sana na hali nzima! Mgeni huyo amerudi kila mwaka na amekuwa rafiki wa karibu sana.”

  Unataka kuunda hali nzuri kwa ajili ya wageni wako wa kwanza na wa siku zijazo? Angalia mwongozo huu wa hatua tano.

  Hatua ya 1: Wasiliana mapema na mara kwa mara

  Kuwakaribisha wageni huanza hata kabla hawajafika mlangoni pako. Kwa kujibu haraka ujumbe wa wageni, unawajulisha kwamba unajali mahitaji yao. Mazungumzo haya ya mapema pia ni fursa nzuri ya kujenga matarajio. Vidokezi kadhaa vya kusaidia:

  • Kuwa mkweli. Wageni wanaweza kuwa wamesahau maelezo muhimu katika tangazo lako. Je, unahitaji kuwakumbusha kwamba kutakuwa na wanyama vipenzi, wageni wengine, au wanafamilia katika sehemu zinazotumiwa pamoja katika nyumba yako?
  • Jibu kwa urahisi. Unaweza kutumia ujumbe wa Airbnb au programu kujibu wageni ukiwa nyumbani na unapofanya shughuli zako.
  • Fikiria mbele. Ikiwa unatarajia kutuma taarifa zile zile kwa wageni kadhaa, okoa muda kwa kutumia kipengele cha majibu ya haraka (awali kilijulikana kama ujumbe uliohifadhiwa).

  Hatua ya 2: Rahisisha kuwasili na kuingia

  Unaweza kujibu maswali yanayoulizwa sana na kuwawezesha wageni kuingia kwa namna shwari kwa kujaza sehemu zote zilizoko chini ya sehemu ya "taarifa kwa ajili ya wageni" ya kichupo chako cha Matangazo, pamoja na maelekezo ya kwenda kwenye sehemu yako, maelekezo ya kuingia na Wi-Fi. Taarifa hii itasaidia wageni wako kuwa na mchakato shwari wa kuingia. Itatumika pia kujaza Mwongozo wako wa Kuwasili, ambayo itaonekana upande wa juu wa vichupo vya Safari za wageni saa 48 kabla ya kuingia.

  Hatua ya 3: Hakikisha vitu ni safi na maridadi

  Sehemu safi huvutia. Wageni wakipata vumbi kwenye chumba cha kulala au madoa ya chakula jikoni, inawezekana kuwa hayo tu ndiyo watayokumbuka kuhusu sehemu yako. Nywele zikiwa pasipotarajiwa hukera sana, pia kukiwa na vitu vingi vya binafsi vitafanya sehemu kuonekana kuwa imejaa. Hakikisha unayapa uangalifu wa ziada mashuka, taulo, sakafu na bafu.

  Hatua ya 4: Bashiri mahitaji ya wageni

  Kila mgeni ni tofauti, lakini wengi watatarajia kuweza kufikia vitu na taarifa fulani mara moja. Fikiria:

  • Kuhakikisha sehemu yako ina vistawishi muhimu vya kutosha, ikiwemo taulo, mashuka, sabuni na karatasi ya choo
  • Kufanya mabadiliko kwenye mwongozo wako wa nyumba ili kuwapa wageni taarifa muhimu kuhusu sehemu zilizopigwa marufuku, maelekezo kwa ajili ya vifaa, Wi-Fi, n.k.
  • Kuunda kitabu cha mwongozo kilicho na mikahawa unayopenda, maduka ya vyakula, maduka ya kahawa na kadhalika
  • Kuhakikisha unaweza kupatikana kupitia arafa, simu au barua pepe iwapo chochote kitaenda mrama
  • Kuwa na nambari za simu za watu muhimu, kama vile fundi bomba, mtu anayefanya kazi ndogo ndogo, wakala wa mtandao na usaidizi wa kebo au majirani wanaoweza kupatikana kwa urahisi ikiwa utakuwa mbali

  Hatua ya 5: Toa na upate tathmini

  Tathmini zako kadhaa za kwanza ni muhimu katika ufanisi wako kwenye Airbnb—wastani wa ukadiriaji wako wa nyota utaonekana kwenye tangazo lako baada ya kupokea tathmini tatu na unaweza kuathiri jinsi unavyoorodheshwa katika matokeo ya utafutaji.

  Pia utapata fursa ya kuwatathmini wageni. Kuwa mwaminifu na mwenye heshima.

  "Kuwaandikia wageni maoni kuna umuhimu sawa na kuandaa chumba kwa ajili yao," Beverlee na Suzie wa Oakland, California, wanasema. “Unamruhusu Mwenyeji mwingine mtarajiwa kuamua ikiwa anataka kumkaribisha mgeni huyo au la.” Mchakato wa kutathmini husaidia kujenga uaminifu miongoni mwa wageni na Wenyeji, hivyo kujenga hali bora kwa jumuiya nzima ya Airbnb.

  Vidokezi

  • Maelekezo ya kuingia ya kisasa zaidi yanaweza kufanya kuwasili kwa wageni kuwa rahisi

  • Kuhakikisha sehemu yako ni safi kunasaidia wageni kuwa na ukaaji mzuri

  • Kupatikana kwa ajili ya wageni kunaweza kuwasaidia kujihisi kusaidiwa

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuwafurahisha wageni wako wa kwanza
  Airbnb
  20 Nov 2019
  Ilikuwa na manufaa?