Jinsi ya kuanzisha tangazo lako la Vyumba
Tangazo lako la Vyumba ni mahali ambapo unawaonyesha wageni vile ilivyo kukaa nyumbani kwako. Unaweza kwenda kwa undani kuhusu sehemu ambazo ni za kujitegemea, ambazo ni za pamoja na jinsi unavyopendelea kuingiliana na wageni.
Unachopaswa kujumuisha katika tangazo lako
Mipangilio hii ya tangazo na uwekaji nafasi hukuruhusu kuweka au kusasisha taarifa ambayo huwasaidia wageni kuamua ikiwa watajisikia vizuri na salama wakishiriki sehemu yako:
Maelezo ya tangazo. Tumia sehemu hii kuelezea mambo ya kipekee kuhusu nyumba yako. Chagua kila kistawishi unachotoa, na ubainishe maelezo kama vile sehemu ambazo wageni wanaweza kufikia, iwe wanyama vipenzi wanaishi kwenye nyumba na jinsi kitongoji chako kilivyo.
Picha na maelezo mafupi. Onyesha wazi maeneo yote ambayo wageni wanaweza kufikia, ikiwemo njia za kuingia na sehemu za maegesho. Angazia chochote kinachowasaidia wageni kuamua iwapo Chumba chako kinakidhi mahitaji yao ya usafiri.
Vyumba na sehemu za kulala. Wajulishe wageni ikiwa bafu ni la kujitegemea au la pamoja, ikiwa kuna kufuli kwenye mlango wa chumba cha kulala, na nani mwingine atakayekuwa kwenye nyumba wakati wa ukaaji wao.
Sheria za nyumba. Kuwa wazi kuhusu kile ambacho ni muhimu kwako, kama vile ikiwa una saa za utulivu au kuruhusu wageni kuleta wanyama vipenzi, ili kusaidia kupunguza kutoelewana. Wageni wanatarajiwa kufuata sheria zako na wanaweza kuondolewa kwenye Airbnb ikiwa watasababisha matatizo.
Kuna njia nyingine za kivitendo ambazo unaweza kuwasaidia wageni wote wajisikie wamekaribishwa. Daniel, mshiriki wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji nchini Uhispania, anaandika katika wasifu wake: "Milango ya nyumba yangu iko wazi kwa kila mtu."
Unachopaswa kujumuisha katika Chumba chako
Unda sehemu yenye starehe, isiyo na mparaganyo yenye nafasi kwa ajili ya vitu binafsi vya mgeni wako. Fikiria kuhusu vitu vyote unavyohitaji unaposafiri, kisha jaribu kuvijumuisha.
Wenyeji wa vyumba wanasema kwamba kuweka huduma maalumu kunaweza kumsaidia kila mtu ajisikie huru na kusababisha tathmini nzuri. Haya yanajumuisha:
Hifadhi ya chakula. Weka nafasi mahususi katika friji na stoo ya chakula na uweke alama kwa ajili ya wageni, au weka friji ndogo na stoo ya chakula ndani au karibu na chumba cha kulala cha mgeni wako.
Kikapu cha vinywaji. Maji, kahawa, na chai pamoja na vikombe na birika la umeme katika Chumba ni rahisi na huwafaa wageni ambao wanapendelea kukaa peke yao.
Kuzuia kelele. Plagi za masikio, malapa, au feni au mashine ya kelele nyeupe zinaweza kupunguza kelele zisizohitajika.
Makufuli. Wageni wanatarajia kuwa na uwezo wa kufunga mlango wa chumba cha kulala. Ikiwa Chumba chako hakina kufuli, fikiria kuliweka.
"Kufuli la chumba cha kulala hufanya iwe rahisi kwa kila mtu kupata usingizi mzuri wa usiku na kufurahia usingizi kikamilifu," anasema Dandara, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji ambaye anakaribisha wageni kwenye Chumba huko Maceió, Brazili.
Waombe wageni waandike tathmini na watumie maoni yao kufanya mabadiliko. Sasisha tangazo lako wakati wowote unapofanya hivyo.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.