Kusaidia wageni kusafiri kama wakazi
Airbnb ilianza kama njia ya bei nafuu kwa wasafiri kukaa katika nyumba ya mtu mwingine. Wazo hilo lilianza kutekelezwa kadiri wenyeji wengi zaidi walivyotoa sehemu mbalimbali ulimwenguni na kuchangamana na wageni.
Vyumba husherehekea utamaduni huu: Ni nzuri kwa wageni ambao wanapendelea faragha kidogo, lakini bado wanataka kukutana na mtu mpya na kujionea eneo hilo kama mkazi. Wakiwa na chumba, wageni wana chumba chao cha kulala katika nyumba, pamoja na ufikiaji wa sehemu ambazo zinaweza kutumiwa pamoja na wengine.
Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kuwasaidia wageni wajisikie huru kuweka nafasi na kukaa nawe.
Kushiriki maeneo unayoyapenda katika eneo husika
Unaweza kuwasaidia wageni wajue eneo lako kwa kuunda kitabu cha mwongozo cha tangazo lako. Hii ni njia rahisi ya kuwapa wageni mapendekezo.
Wenyeji wengi pia hutoa mapendekezo ana kwa ana. Reed, ambaye anakaribisha wageni kwenye chumba jijini Philadelphia pamoja na mke wake, mara nyingi huwaalika wageni wajiunge nao kwenye chakula cha jioni cha Jumapili. Anazungumzia "maeneo ya kupendeza ambayo si ya kitamaduni," kama vile mgahawa wa kitongoji ulio na kuta za vitabu.
Wakati mwingine Reed huwaalika wageni kucheza dansi ya salsa, mojawapo ya burudani anazozipenda. "Tumeenda na wageni kadhaa kwenye eneo la Kilatini ili tuliwashe kidogo," anasema. Baadhi ya wageni, anaongeza, "ni kama watoto wetu sasa."
Kuwafanya wageni wajisikie wakiwa nyumbani
Wageni wanaweza kuweka nafasi ya chumba chako kwa sababu wasifu wako wa mwenyeji huunda hali ya kufahamiana, ambayo inaweza kuwasaidia wageni wajisikie huru kukaa na wewe.
Nicola, ambaye anakaribisha wageni kwenye chumba jijini Fitzroy, Australia, anasema kwamba anathamini tamaduni na mapishi mapya. Amegundua kuwa baadhi ya wageni wanapenda "kubarizi na kuhisi kana kwamba wana nyumba hapa."
Yeye na kaka yake, mpishi maarufu jijini Melbourne, wakati mwingine wanajitolea kupika chakula na wageni. "Tuna jiko la kibiashara, hivyo wanaweza kuandaa tambi au mikate ya panini," anasema.
Kikundi kimoja kilijisikia huru sana kiasi kwamba walifanya yoga kwenye sebule ya Nicola. "Lilikuwa jambo zuri sana kiasi kwamba walifurahia sana sehemu hiyo," anasema. Kwa kutambua nia yao ya kufanya mazoezi, Nicola aliwapeleka kwenye bustani iliyo karibu, ambapo walitumia alasiri kupanda miti na kuzungumza kuhusu maeneo mengine ya kuvinjari.
Kukumbatia yasiyotarajiwa
Fikiria kuhusu jinsi ambavyo ungependa kuingiliana na wageni na uwajulishe kile unachopendelea. Ikiwa uko tayari kuchangamana, uwazi wako unaweza kusababisha uhusiano wa maana.
Garth, Mwenyeji jijini Auckland, New Zealand, anasema kukaribisha wageni kunamruhusu kutumia muda mwingi na watu wa tamaduni nyingine bila kusafiri. Aliwaza, "Hebu tuwalete watu kwangu."
Mojawapo ya tukio la kukumbukwa zaidi la Garth kama mwenyeji lilitokea kwa wageni waliotoka Ufaransa. Mama alimuuliza ikiwa mwanawe angeweza kumtazama akitengeneza vitu kwenye gereji yake. "Alidhani kila kitu nilichokuwa nikifanya kilikuwa kizuri," Garth anasema.
Kwa hivyo Garth alibuni mradi ambao wangeweza kufanya pamoja. "Tulitengeneza boti ndogo na tukaipaka rangi," anasema. "Ilikuwa nzuri sana, kwa sababu hakuzungumza Kiingereza, lakini tulikuwa na lugha hii ya pamoja."
Unaweza kupata hadithi na vidokezi zaidi vya kukaribisha wageni kwa kujiunga na Kilabu cha Wenyeji cha mahali ulipo. Vilabu hivi vinaendeshwa na wenyeji na vinatoa mikutano ya ana kwa ana na ya mtandaoni, usaidizi unaoendelea na habari kuhusu Airbnb na huduma zake.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.