Je, chumba kwenye Airbnb ni nini?
Sehemu yako ya ziada inaweza kuwa njia ya kujipatia pesa na kukutana na watu. Ikiwa una chumba cha kulala cha ziada, unaweza kuweka tangazo na kukaribisha wageni kwenye nyumba yako.
"Ina faida sana na si tu kifedha," anasema Eric, Mwenyeji Bingwa huko Los Angeles. “Wageni wanakuja California kuwa na jasura yao wenyewe, lakini pia ni jasura nzuri kwetu, kwa sababu hatujui ni nani atakayekuwa upande wa pili wa mlango. Tunajifunza mengi kuhusu maeneo kote ulimwenguni."
Vyumba ni maarufu ulimwenguni kote, vina nafasi ya tatu katika uwekaji nafasi kati ya aina zote za sehemu za kukaa kwenye Airbnb.* Wageni wanaweza kupata na kuweka nafasi ya vyumba kwa kuchagua Chumba kwenye kichujio cha utafutaji.
Haya ndiyo mambo unayohitaji kujua ili uanze kukaribisha wageni kwenye chumba.
Je, ni nini kinachostahili kuwa chumba?
Akiwa na chumba, mgeni anapata chumba chake cha kulala cha kujitegemea katika nyumba ya mwenyeji, pamoja na ufikiaji wa maeneo ya pamoja ambayo anaweza kushiriki na wengine.
Ili kustahiki kuwa chumba, tangazo linahitaji kukidhi vigezo hivi vyote:
Mgeni ana chumba chake cha kulala cha kujitegemea kikiwa na mlango.
Mgeni anaweza kufikia bafu la kujitegemea au la pamoja.
Mgeni anaweza kufikia angalau sehemu moja ya pamoja, kama vile jiko, sebule, au ua wa nyuma.
Wenyeji wanatumia majina yao kwenye tangazo lao, badala ya majina ya biashara au majina mengine.
"Chumba" kinachaguliwa kama tangazo au aina ya chumba katika mipangilio ya tangazo la mwenyeji.
Chumba cha kujitegemea si chumba cha pamoja, hoteli, risoti, hema, gari la malazi, nyumba ya kujitegemea (kama vile nyumba isiyo na ghorofa ya ua wa nyuma) au aina nyingine yoyote ya nyumba iliyo kwenye orodha hii.
Ikiwa tangazo lako halikidhi vigezo hivi, chagua aina nyingine ya sehemu unapounda tangazo lako.
Kwa nini ukaribishe wageni kwenye chumba?
Vyumba vya ziada vinaweza kufanya mengi zaidi ya kukusanya vumbi au kuhifadhi vitu vya ziada. Faida za kutangaza sehemu hiyo zinajumuisha:
Kujipatia pesa. Mwaka 2022, wenyeji wa vyumba walijipatia zaidi ya USD bilioni 2.9 ulimwenguni kote na mapato ya wastani yalikuwa zaidi ya asilimia 20 kuanzia mwaka 2021.**
Kuhusiana na watu. Kushiriki nyumba yako, mapendeleo, utamaduni na vidokezi vya eneo husika kunaweza kusababisha mwingiliano wa maana na wasafiri.
Kutumia sehemu uliyonayo tayari. Chumba chako cha ziada kinaweza kuwapa wageni mahali pazuri pa kulala, bila kupata gharama nyingi za kuanza kukaribisha wageni kwenye nyumba nzima.
"Nina nyumba kubwa na ninaishi peke yangu na nina eneo na hali inayofaa ya kukaribisha wageni," anasema Ruth, mwenyeji jijini Perth, Australia. “Sikuhitaji kutumia gharama kubwa kununua vitanda, kurekebisha vyumba, kuhamisha samani au kitu kama hicho.”
*Kulingana na takwimu za kimataifa za Airbnb zilizokusanywa kati ya mwezi Mei 2022 na Machi 2023
**Mapato ya wastani kwa wenyeji wote wa vyumba ulimwenguni
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.