Nyenzo na vidokezi vya kukusaidia kupanga bei ya chumba chako
Unafuu ni mojawapo ya sababu kuu za wageni kuweka nafasi ya vyumba kwenye Airbnb. Zaidi ya asilimia 80 ya vyumba ulimwenguni kote mwaka 2022 vilikuwa chini ya USD 100 kwa usiku na bei wastani ya USD 67 kwa usiku.*
Siku zote una udhibiti wa bei unayoweka. Airbnb inatoa nyenzo unazoweza kutumia ili kuweka na kurekebisha bei yako.
Kulinganisha matangazo sawia yaliyo karibu
Kuelewa bei za wastani za matangazo kama hayo katika eneo lako kunaweza kuwa mahali pazuri pa kuanza kufikiria kuhusu cha kutoza.
Nenda kwenye kalenda yako ya kukaribisha wageni ili ulinganishe matangazo sawia yaliyo karibu. Chagua tarehe au tarehe kadhaa, kisha uguse au ubofye bei yako ya kila usiku. Chini yake, chagua Matangazo sawia ili upate ramani inayoonyesha bei za wastani za matangazo kama yako. Unaweza kuonyesha maeneo ambayo yamewekewa nafasi au ambayo hayajawekewa nafasi kwenye tarehe hizo.
Richard, ambaye anakaribisha wageni kwenye chumba karibu na sehemu ya biashara ya jiji la Toronto, aliamua kuanza "chini kidogo ya ushindani" ili kupata wageni haraka. Ilifanya kazi: Anasema miezi yake 3 ya kwanza iliwekewa nafasi karibu siku zote.
"Bei yangu bado iko chini kidogo, lakini ninajua ninapotaka kwenda," Richard anasema. "Ninafikiria kuhusu kuongeza bei yangu kwa nyongeza ndogo baada ya muda."
Kuzingatia mahali ulipo
Kufanya utafiti kidogo kuhusu mienendo ya usafiri katika eneo lako pia kunaweza kukusaidia kupanga bei ya eneo lako kwa ushindani. Wageni wa wikendi, wageni wa likizo za msimu, wafanyakazi wa muda mfupi na aina nyingine za wageni wanaweza kufasili "bei nafuu" kwa njia tofauti.
Reed, Mwenyeji Bingwa huko Philadelphia, alichunguza mandhari ya eneo alipoweka bei ya chumba chake cha kulala cha ghorofa ya tatu. Kwa sababu anaishi karibu na vyuo vikuu na hospitali, aliweka bei ya chumba chake kwa ajili ya wanafunzi na wanagenzi wanaotembelea eneo hilo wasiotaka kutumia pesa nyingi. "Tumekaribisha kundi la watu wanaofanya utafiti au mafunzo ya matibabu na walihitaji mahali pa kukaa kwa wiki kadhaa," anasema.
Kwa kuweka bei yake chini na kukubali ukaaji wa muda mrefu, Reed anasema ameweza kujaza kalenda yake na kulipa rehani yake kabla ya ratiba. "Nina usiku mwingi uliowekewa nafasi na idadi ndogo ya wageni wanaoingia," anasema. "Ninafanya kazi kwa busara badala ya kufanya kazi kwa nguvu."
Kuweka punguzo
Wageni wanaopenda ukaaji wa muda mrefu huwa wanatafuta sehemu zenye mapunguzo. Reed hutumia mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi ili kuwavutia wageni waweke nafasi. "Watu wengi ambao wamevutiwa na chumba chetu wanatafuta angalau wiki kadhaa," anasema.
Unaweza kujaribu mapunguzo anuwai kufaa hali tofauti. Utapata machaguo haya yanayopatikana kwenye kichupo cha Bei kwenye kalenda yako:
Promosheni ya tangazo jipya. Promosheni hii inatoa punguzo la asilimia 20 kwenye bei yako ya kila usiku kwenye nafasi 3 za kwanza unazowekewa. Kuiweka kunaweza kukusaidia kupata tathmini za wageni haraka na kujenga sifa yako kama mwenyeji.
Punguzo kwa watakaowahi. Punguzo hili linatumika kwenye nafasi zilizowekwa mapema. Unachagua urefu wa muda, kuanzia mwezi mmoja hadi miezi 24 kabla ya kuingia. Mapunguzo kwa watakaowahi yanaweza kusaidia kuwavutia wageni wanaopanga mapema.
Punguzo la dakika za mwisho. Punguzo hili linatumika kwenye nafasi zilizowekwa ndani ya muda mfupi. Unachagua muda mfupi kiasi gani, kuanzia siku moja hadi siku 28 kabla ya kuingia. Wageni wa vyumba mara nyingi wanakuwa wasafiri wa kujitegemea ambao wana urahisi wa kubadilika ukilinganisha na wenzi au familia kuweza kuweka nafasi muda mfupi kabla ya tarehe ya safari yao.
Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi. Mapunguzo ya kila wiki yanatumika kwa nafasi zilizowekwa za usiku 7 au zaidi na mapunguzo ya kila mwezi yanatumika kwa nafasi zilizowekwa za usiku 28 au zaidi. Hizi zinaweza kukusaidia kujaza kalenda yako kwa idadi ndogo ya wageni wanaoingia.
Hakikisha sikuzote umeweka muda wa chini na wa juu wa ukaaji unaofuata sheria na kanuni za eneo husika. Kuanzia hapo, unaweza kurekebisha muda wako wa juu wa ukaaji kuwa angalau usiku mwingi kama muda wa kukaa ambao ungependa kuwekea punguzo.
*Bei ya kila usiku ikiwemo ada na kodikuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba, 2022
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.