Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi ya kupanua biashara yako na Matukio

  Wahudumu wanaweza kufanya zaidi kwa kuweka shughuli za kuhamasisha.
  Na Airbnb tarehe 17 Jan 2019
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 7 Jan 2022

  Vifungua kinywa vilivyotengenezewa nyumbani, ziara za matembezi, shughuli za kitongojini na kadhalika—Wenyeji Bingwa hufanya mengi zaidi ili kuwafanya wageni wahisi kukaribishwa. Kwa kweli, karibu asilimia 30* ya wenyeji wa nyumba wa Airbnb wamewapa wageni ziara na shughuli. Na baadhi ya wenyeji hata wamefanya huduma hizo kuwa rasmi kwa kuingia katika Matukio.

  Wafikirie Wenyeji Bingwa Patricia Ramos na Oscar Fernandez, waliokuwa miongoni mwa wenyeji wa kwanza wa Matukio nchini Kyuba. Wanandoa hao, ambao wote ni maprofesa wa uchumi katika Chuo Kikuu cha Havana, walianza kama wenyeji wa nyumba. Sasa, pia wanaandaa Matukio manne: jasura ya kitamaduni ya siku mbili huko Havana na maeneo ya vijijini; ziara ya nusu siku ya kutembea Havana halisi; safari ya siku nzima kwenda sehemu za mashambani za Kyuba ili kulima kahawa, kufuga wanyama na kuishi kwa kutegemea shamba; pamoja na mazungumzo ya saa mbili kuhusu uchumi na jamii ya Kyuba huku tukinywa vinywaji vya Kyuba au kinywaji cha chaguo la mtu. Aidha, "tumewahimiza marafiki kuandaa Matukio mengine 15," Oscar akasema.

  Patricia na Oscar walizungumza nasi kuhusu jinsi walivyouinua ujasiriamali wao kufikia kiwango kingine.

  Basi ulianzaje Matukio?
  Oscar: "Tulikuwa tukitumia saa mbili na kila mgeni wakati wa kuingia kwa sababu tulitaka kumwambia kila kitu tunachojua kuhusu Kyuba. Na tulifurahia sana kwa sababu tulihisi kama sisi ni maprofesa walio na mwanafunzi mpya wa aina tofauti.”

  Patricia: "Halafu watu wakaanza kutuandikia tathmini na wakaandika kuhusu [ziara zetu za kushtukiza]. Kwa hivyo Airbnb ilipozindua Matukio nchini Kyuba, tulisema, 'Kwa nini tusiunde Tukio kama ambavyo tayari tunafanya wakati wa kuingia?'”

  Tuambie kuhusu Tukio lako la kwanza, kwa kuwa Jasuria ya Kyuba Ni nini hufanya liwe la kipekee?
  Patricia: "Kwa sehemu kubwa, wageni wa kimataifa wanaokuja Kyuba wanatarajia kusikia kuhusu tumbaku, pombe aina ya rum na muziki wa salsa. Lakini tulichotaka kufanya ni kuwaonyesha wageni vitu zaidi: jinsi mfumo wa elimu, mfumo wa afya na masoko unavyofanya kazi; na jinsi watu wanavyoishi kwa mshahara mdogo sana. Tunafanya ziara ya kutembea jijini na kuwaonyesha maeneo ambayo si ya watalii, kama vile Coppelia, ambayo ni ufalme wa aisikirimu. Vijiko vitano vya aisikirimu vinagharimu takribani USD senti 25. Unasubiri kwa takribani dakika 30 na watu hushirikiana na hata kufanya mikutano wakati wanasubiri kwenye foleni—hicho ni kionjo cha jamii ya Kyuba. Tunawapeleka pia wageni wetu kwenye usafiri wa umma, jambo ambalo ni nadra sana [kwa watalii]. Mwisho wa siku, wanahisi kwamba wamefanya kitu kikubwa sana na wanaweza kuongea kuhusu jinsi Wakyuba wanavyoishi katika jamii ya ujamaa."

  Ni sehemu gani bora kuhusu kuwa mwenyeji wa Tukio?
  Oscar: “Ujuzi na ukwasi wa kitamaduni ni wa kushangaza. Kila wakati, unashiriki na wengine utamaduni wako. Bado sisi ni maprofesa katika chuo kikuu, kwa hivyo tunawahimiza wenzetu wadogo washirikiane nasi kuandaa Tukio. Tunahisi pia Airbnb imetengeneza ajira na kuboresha maisha. Kwa Tukio letu la "Maisha Vijijini", tunawapeleka wageni wetu kwenye eneo la mashambani ili wakutane na marafiki wa familia yetu ambao maisha yao yanategema shamba kwa kuvua na kupanda matunda na kahawa. Sasa, tunawaleta wageni hapo karibu mara tatu kwa wiki na sasa marafiki wetu ni wajasiriamali pia.”

  Je, kuna ushauri wowote kwa wenyeji wengine wanaofikiria kuunda Tukio?
  Patricia: "Ni kuhusu ikiwa una kitu cha kushiriki na wengine na iwapo kama kweli ungependa kukishiriki na wengine."

  Oscar: “Kwa sababu jambo kuu ni kuwa wazi kwa wageni. Lazima uwe mkweli na halisi, vinginevyo hutafanikiwa.”

  *Kulingana na utafiti wa ndani wa Airbnb wa zaidi ya wenyeji 100.

  Taarifa zilizo ndani ya makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Airbnb
  17 Jan 2019
  Ilikuwa na manufaa?