Jinsi ya kupinga tathmini za kulipiza kisasi
Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Airbnb 2022 Toleo la Novemba. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu toleo letu la hivi karibuni.
Tunajua Wenyeji mara nyingi huwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa tathmini ya kulipiza kisasi. Hizi ni tathmini za kibaguzi ambazo wageni wanaweza kuziweka baada ya kuripoti kwamba wamekiuka mojawapo ya sheria za nyumba yako, wameharibu nyumba yako au wamefanya ukiukaji mwingine mkubwa wa sera.
Mfumo wetu wa tathmini unakuwezesha kupinga tathmini unazoamini kuwa za kulipiza kisasi.
Ulinzi dhidi ya tathmini za kulipiza kisasi
Unapaswa kujisikia huru kukaribisha wageni bila kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuandikiwa tathmini ya kulipiza kisasi. Unaweza kupinga tathmini ya kulipiza kisasi,bila kujali ilichapishwa lini, kutoka kwa wageni ambao wanakiuka sera kwa kiwango kikubwa, kama vile:
Kuharibu nyumba yako
Kuzidisha muda wa kukaa
Kukiuka sheria za kawaida za nyumba yako
Kuwa na sherehe au hafla isiyoidhinishwa kwenye sehemu yako
Kupinga tathmini hakumaanishi kwamba lazima itaondolewa. Unapopinga tathmini, tutakuomba utoe ushahidi, kama vile picha au uzi wa ujumbe wa mazungumzo kati yako na wageni.
Ushahidi wako utahitaji kuonyesha kwamba ukiukaji mkubwa wa sera ulitokea. Lazima iwe wazi kwamba kutoa ripoti kuhusu ukiukaji wa sera kwa Airbnb na/au mgeni huenda kulisababisha tathmini ya kulipiza kisasi.
Ni wazo nzuri kudumisha mawasiliano yako yote na wageni kwenye kikasha chako cha Airbnb, ili timu yetu ya huduma kwa wateja iweze kutathmini ushahidi wowote kwa urahisi. Kumbuka kwamba ni Wenyeji wakuu na wageni pekee ndio wanaoweza kupinga tathmini.
Pata taarifa zaidi kuhusu sera yetu ya tathmini
Jinsi sera hiyo inavyofanya kazi
Hebu tuseme mgeni anavuta sigara nyumbani kwako, kinyume cha sheria za nyumba yako. Unamwambia mgeni wako kwamba umekuta mabaki ya sigara sebuleni na unawasilisha ombi la kufidiwa ili uweze kufanya usafi wa kina. Kwa kujibu, mgeni wako anakataa kulipa kisha anaandika tathmini ya hasira. Unaweza kupinga tathmini hii na tutachunguza ili kubaini ikiwa inastahiki kuondolewa.
Wenyeji wametuambia kwamba sera yetu iliyosasishwa kuhusu tathmini za kulipiza kisasi imewasaidia kukaribisha wageni kwa kujiamini. Mwenyeji Leanne anasema tathmini ya kulipiza kisasi kwenye tangazo lake "ilitathminiwa mara moja na kuondolewa nilipotuma ombi. Nilihisi kweli kwamba Airbnb ilikuwa upande wangu.”
Mwenyeji Daniel pia "nilishughulikia tathmini niliyoiona kuwa isiyo ya haki," anasema. "Ninaweza kusema kwamba [Airbnb Usaidizi] ilisaidia sana kushughulikia ombi langu."