Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

    Karibisha wageni ukiwa na uhakika kupitia sera na ulinzi wetu

    Kuanzia viwango vya wageni hadi AirCover kwa ajili ya Wenyeji, tuko hapa kukusaidia.
    Na Airbnb tarehe 20 Okt 2020
    Inachukua dakika 5 kusoma
    Imesasishwa tarehe 21 Jul 2023

    Vidokezi

    Wengi wenu mmetuambia jinsi mnavyopenda kushiriki sehemu yenu na kuungana na watu kutoka kote ulimwenguni. Bila shaka, hilo halingewezekana ikiwa hamngehisi kusaidiwa mnapokaribisha wageni

    Tunaelewa kwamba mnahitaji Airbnb iwasaidie katika nyakati nadra lakini za kusikitisha wakati mambo hayaendi kulingana na mpango. Ili kuwasaidia kukaribisha wageni mkiwa na uhakika, hizi hapa ni baadhi ya nyenzo, sera na vipengele tulivyonavyo.

    Ulinzi kamili kwa Wenyeji

    Katika Airbnb, ulinzi wetu wa kina wa Mwenyeji hututenga na hutusaidia kuweka jumuiya yetu salama.

    • AirCover kwa ajili ya Wenyeji: Tunajumuisha ulinzi kamili kwa kila Mwenyeji kwenye Airbnb. AirCover kwa ajili ya Wenyeji hutoa ulinzi kabla ya safari ili kusaidia kuhakikisha wageni wanaoweka nafasi wako jinsi wanavyodai kwenye uthibitisho wa utambulisho wa mgeni na husaidia kupunguza uwezekano wa sherehe zenye usumbufu na uharibifu wa nyumba kupitia teknolojia ya uchunguzi wa nafasi iliyowekwa. Pia inajumuisha USD milioni 1 ya bima ya dhima ya Mwenyeji na USD milioni 3 ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, pamoja na ulinzi wa kazi za sanaa, vitu vya thamani, magari yaliyoegeshwa, boti na magari mengine.
    • Sheria za msingi: Sheria za msingi kwa ajili ya wageni ni seti ya viwango vinavyoweza kutekelezwa ambavyo wageni wote wanapaswa kufuata. Sheria za msingi zinahitaji wageni waheshimu sehemu yako, wafuate sheria za nyumba yako, wawasiliane mara moja ikiwa matatizo yatatokea na waache nyumba yako katika hali ambayo haihitaji kufanyiwa usafi kupita kiasi.
    • Kughairi kwa Mwenyeji: Una haki ya kutathmini tathmini za mgeni na mtiririko wa ujumbe na kughairi nafasi iliyowekwa unayoamini kwamba itasababisha sherehe. Utaombwa uwasilishe ushahidi kwenye kituo cha Usaidizi wa Jumuiya. Ughairi wote lazima uambatane na sera yetu ya kutobagua.

    Nyenzo za kukupa udhibiti zaidi

    Sehemu ya kukaribisha wageni ni kuweka matarajio ili kusaidia kuzuia visa visitokee. Hivi ni vipengele vichache ambavyo tumeunda ili kukusaidia kuvutia wageni ambao wataweza kufaa sehemu yako:

    • Mipangilio ya kalenda na kuweka nafasi: Kuanzia idadi ya watu wanaoweza kukaa katika eneo lako, unawafahamisha wageni kile kinachokufaa. Chagua idadi ya usiku ambapo wageni wanaweza kukaa, wakati wa mapema zaidi ambapo wanaweza kuweka nafasi na muda unaohitaji kati ya ukaaji. Pata maelezo zaidi kuhusu kuchagua mipangilio yako ya kuweka nafasi
    • Sera za kughairi: Sera ya kughairi utakayochagua itaeleza kwa uwazi ilani ambayo wageni wako wanapaswa kutoa ikiwa wanataka kughairi nafasi waliyoweka na kurejeshewa fedha zote. Pata maelezo zaidi kuhusu kuchagua sera ya kughairi
    • Sheria za nyumba: Sheria za kawaida za nyumba yako, kama vile kutovuta sigara, kutotumia sigara za kielektroniki au kutoruhusu wanyama vipenzi, zinaweza kufanywa ziwe mahususi na huwasaidia wageni kuelewa matarajio yako ili waweze kuamua endapo sehemu yako inawafaa. Sheria za nyumba yako zinaonyeshwa katika sehemu nne: kwenye ukurasa wa tangazo lako, kwenye skrini ya uthibitishaji wageni wanapoweka nafasi kwenye sehemu yako na kwenye barua pepe ya Fungasha Mabegi Yako na Mwongozo wa Kuwasili ambao wageni hupokea kabla ya safari yao. Ukiwa na sheria za msingi kwa ajili ya wageni, chochote unachoweka katika sheria za kawaida za nyumba yako kinaweza kutekelezwa.
    • Nyenzo za majibu: Ikiwa una shaka na ombi la safari, unaweza kuchagua kulikataa mradi tu unafuata sera yetu ya kutobagua.

    Usaidizi wa jumuiya kwa Wenyeji

    Hata viwango na mipangilio hii ikiwekwa, kuna visa nadra ambapo mambo hayaendi kama inavyotarajiwa. Katika nyakati hizo, kuna njia kadhaa ambazo unaweza kupata usaidizi kutoka kwa Airbnb:

    • Mawasiliano ya moja kwa moja: Usaidizi wa mtandaoni wa Airbnb ndiyo njia ya haraka zaidi ya kupata msaada unaohitaji kwa matatizo yasiyo ya dharura kama vile kusasisha kalenda yako au kurekebisha bei yako.
    • Usaidizi mahususi wa Wenyeji Bingwa: Ikiwa wewe ni Mwenyeji Bingwa, utaunganishwa kwa urahisi na mfanyakazi mtaalamu katika huduma kwa wateja wakati wowote unapoomba msaada.
    • Nambari ya simu ya dharura ya eneo husika: Tunajua kwamba wageni wanaosafiri katika nchi wasizofahamu huenda wasijue jinsi ya kuwasiliana na huduma za dharura za eneo husika, kwa hivyo tumezindua kitufe cha kupiga simu ya dharura cha ndani ya programu. Kitufe hiki hutoa muunganisho wa moja kwa moja kwa mamlaka ya kutekeleza sheria na huduma za dharura za eneo husika wakati wa nafasi amilifu iliyowekwa.
    • Nambari ya simu ya usaidizi wa dharura: Ikiwa uko nchini Marekani na unakumbana na jambo la dharura linalohusiana na usalama au ulinzi wako wakati wa nafasi amilifu iliyowekwa, unaweza kuunganishwa kwa haraka na mtaalamu kwa ajili ya msaada kupitia programu yetu.

    Ni muhimu tukuze uaminifu ili jumuiya ya Airbnb istawi—na tunatumaini kwamba ulinzi na vipengele hivi vitatusaidia kutimiza jambo hilo. Kama kawaida, asante kwa kuwa Mwenyeji.

    AirCover kwa ajili ya Wenyeji ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Wenyeji,bima ya dhima ya Mwenyejina bima ya dhima ya Matukio haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini Japani, ambapo Bima ya Mwenyeji ya Japani na Bima ya Ulinzi ya Tukio ya Japani zinatumika au Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel LLC. Kwa Wenyeji waliotoa huduma ya sehemu za kukaa au matukio nchini China Bara, Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China unatumika. Kumbuka kwamba vikomo vyote vya ulinzi vinaonyeshwa kwa USD.

    Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio inadhaminiwa na watoa bima wengine. Ikiwa unakaribisha wageni nchini Uingereza, sera za bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio zinatolewa na Zurich Insurance Company Ltd. na zinapangwa na kutekelezwa bila gharama ya ziada kwa Wenyeji wa Uingereza na Airbnb UK Services Limited, mwakilishi aliyeteuliwa wa Aon UK Limited, ambao wameidhinishwa na kudhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha. Nambari ya usajili ya Aon katika FCA ni 310451. Unaweza kuangalia hii kwa kutembelea Rejesta ya Huduma za Fedha au kuwasiliana na FCA kwa 0800 111 6768. Sera za dhima ya Mwenyeji na dhima ya Matukio ya Wenyeji ndani ya AirCover ya kwa ajili ya Wenyeji inadhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Fedha. Bidhaa na huduma zilizosalia si huduma zinazodhibitiwa zilizopangwa na Airbnb UK Services Limited. FPAFF407LC

    Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si bima na hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji. Chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, utarejeshewa fedha kwa ajili ya uharibifu fulani uliosababishwa na wageni kwenye nyumba na mali yako ikiwa mgeni hatalipia uharibifu huo. Kwa matangazo katika Jimbo la Washington, majukumu ya mikataba ya Airbnb chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji yanalindwa na sera ya bima iliyonunuliwa na Airbnb. Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na sheria, masharti na vighairi.

    Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    Airbnb
    20 Okt 2020
    Ilikuwa na manufaa?