Kukusaidia kuwa Mwenyeji endelevu zaidi

Jifunze kuhusu kukaribisha wageni kwa uendelevu katika taarifa ya Aprili ya Bodi ya Ushauri ya Wenyeji.
Na Airbnb tarehe 21 Apr 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 28 Apr 2021

Vidokezi

  • Jifunze jinsi Airbnb na Bodi ya Ushauri ya Wenyeji inavyosaidia Wenyeji kuwa waendelevu zaidi

  • Anna Jones wa Bodi ya Ushauri pia anaeleza kwa nini anajali sana mazingira

  • Pata taarifa kwa wakati kuhusu maendeleo ya Bodi ya Ushauri ya mwenyeji katika mwaka 2021

Kila mwezi tunashiriki sasisho mpya kutoka Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na kukusaidia kuwajua wanachama wa bodi.

Habari kila mtu,

Mimi ni Anna Jones, mwanachama wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na mwezeshaji wa kamati ya uendelevu. Tumekuwa tukikutana na viongozi wa Airbnb kwa miezi michache iliyopita ili kuchunguza jinsi tunavyoweza kuwasaidia Wenyeji kutunza mazingira zaidi.

Katika kusherehekea Siku ya Ardhi mnamo tarehe 22 Aprili, ninafurahi kukushirikisha zaidi kuhusu kile tumekuwa tukifanya!

Kusaidia jumuiya yetu kuwa endelevu zaidi

Inaeleweka kuwa, Wenyeji hawajui pa kuanzia ili kuanza kuwa waendelevu zaidi. Kuna taarifa nyingi huko nje na unaweza mara nyingi kuhisi kuzidiwa!

Nilipojiunga na Bodi ya Ushauri, mojawapo ya malengo yangu ilikuwa kufanya uendelevu uonekane rahisi zaidi kwa wenyeji. Ninaamini kabisa kwamba kwa kusaidiana na kusherehekeana, tunaweza kuunda mabadiliko mazuri!

Hivi ndivyo tunavyofanya kazi na Airbnb kuhusu jambo hili:

  • Kuanzisha mfululizo wa elimu ya uendelevu: Airbnb ilifanya kazi kwa karibu na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, bingwa wa ulimwengu wa mazingira, Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni, shirika linaloongoza la uhifadhi, na Bodi ya Ushauri ya Wenyeji kuunda maudhui ya elimu kwa ajili ya Wenyeji . Hii ni pamoja na makala mpya kama vile mwongozo kwa wanaoanza kujifunza kuhusu jinsi ya kuwa mwenyeji mwendelevu na vidokezi vya kukuza utalii endelevu pamoja na wageni wako. Tutakua tunapanua mfululizo huo kwa mwaka mzima, kwa hivyo endelea kufuatilia ili kupata njia zaidi za kutunza mazingira!
  • Ikishiriki jinsi wenyeji wengine wanavyoleta mabadiliko: Kuwa mwendelevu kunaweza kuwa tofauti sana kulingana na mahali unapoishi na kile unachoweza kupata. Kuonyesha njia mbalimbali ambazo wenyeji wanaweza kuwa waendelevu katika maeneo na sehemu tofauti, tutaangazia Wenyeji ambao wanatunza mazingira kutoka sehemu mbalimbali umwenguni. Wa kwanza ni Mwenyeji Bingwa Tiffany, ambaye ana nyumba ya kulala wageni ya ufukweni huko Hollywood Beach, California.
  • Kuchunguza ushirika wa nishati mbadala: Ili kusaidia kufanya nishati mbadala kupatikana kwa Wenyeji, Airbnb inachunguza ushirikiano na kampuni zinazohimiza kutunza mazingira katika jamii zilizochaguliwa. Airbnb itazindua mpango wa majaribio huko Marekani hivi karibuni, na ikiwa wenyeji watauona kuwa unafaa, tutafanya kazi ya kupanua ofa kama hizo kwa jumuiya ya Wenyeji ulimwengu kote.

Ninafurahi kuwafahamisha kuwa huu ni mwanzo tu! Kamati ya uendelevu ina hamu ya kutafuta njia mpya za kuwasaidia Wenyeji kuyajali mazingira zaidi- na kuokoa pesa pia! Tutashiriki zaidi kuhusu mada hii katika mwaka mzima.

Kwa nini ninajali sana kuhusu mazingira

Kuishi karibu na bahari huko Pembrokeshire, Wales, kuliamsha shauku mpya na kunipa msukumo wa kuunda maisha endelevu zaidi. Nimefurahia kuweza kusaidia Wenyeji wengine kuanza safari hii. Hapa kuna mengi zaidi kunihusu:

Mnamo mwaka 2017, mimi na familia yangu tulikuwa tukitafuta mabadiliko katika mtindo wa maisha, na tulitaka sana kuweka tangazo kwenye Airbnb. Halafu shamba hili zuri la zamani lilikuja kwenye soko, na tukalipenda. Majengo yote yanaenda nyuma mpaka mwaka 1650, kwa hivyo kuna haiba kama hiyo na hali ya utulivu hapa.

Sio tu mazingira mazuri na ukanda wa pwani hapa. Watu wanatia hamasa sana - kuna uhusiano kati ya ardhi na kile wanachofanya. Inaambukiza! Jumuiya yetu ni sehemu muhimu ya uzoefu wa wageni-kutoka sabuni zetu zilizotengenezwa kienyeji hadi sanaa ya hapa ambayo inajaza kuta!

Tuna matangazo mawili. Mama yangu na mimi hufanya mabadiliko yote na ubunifu. Baba yangu hufanya matengenezo yote. Kila kitu ni chetu sisi sote na ni juhudi ya timu. Unajisikia kuhusika sana kutoka ndani kabisa, na shauku ya mahali tunapoishi inazidi kuongezeka.

Niliweka pamoja mpango wetu wa uendelevu, ambao upo katika maelezo ya tangazo letu. Yamechapishwa pia katika nyumba za shambani ili watu waweze kuyasoma na kujifunza kuhusu kile tunachofanya. Tunalima hata miti yetu endelevu ili kupata kuni za majiko yetu!

Nilikuwa mmoja wa waanzilishi wa Bodi ya Jumuiya ya Airbnb ya Uingereza, ambayo ilianza mnamo 2019, na ninaongoza mipango endelevu ya kukaribisha wageni pamoja na wenyeji kadhaa wa Uingereza na timu ya Airbnb.

Imekuwa safari ya maajabu kuwa karibu na mazingira. Nimeelewa misimu na mwenendo wa bahari, na hiyo inaonekana katika kila kitu tunachofanya hapa.

Watu wengi hujitambua wenyewe na kutambua mazingira wanapokaa hapa- wakati mwingine huwa najisikia kama Cupid kwa sababu wageni wanapenda Pembrokeshire na wanaendelea kurudi!

Bodi ya Ushauri ya Wenyeji itarudi tena mwezi ujao na sasisho zaidi kutoka kwenye mikutano yetu ya bodi. Kwa wakati huu, natumaini utapata msaada kutoka kwa mfululizo mpya wa makala ya uendelevu ya !

Kongole! (Au kama tunavyosema hapa Wales, 'Iechyd da!')

Anna Jones

Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika toka zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Jifunze jinsi Airbnb na Bodi ya Ushauri ya Wenyeji inavyosaidia Wenyeji kuwa waendelevu zaidi

  • Anna Jones wa Bodi ya Ushauri pia anaeleza kwa nini anajali sana mazingira

  • Pata taarifa kwa wakati kuhusu maendeleo ya Bodi ya Ushauri ya mwenyeji katika mwaka 2021
Airbnb
21 Apr 2021
Ilikuwa na manufaa?