Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Mwongozo wa mwanagenzi kwa ukaribishaji endelevu wa wageni

Vidokezi hivi vinaweza kukusaidia kupunguza athari ya mazingira ya tangazo lako.
Na Airbnb tarehe 21 Apr 2021

Vidokezi

  • Kuwekeza katika vifaa vinavyotumia nishati kidogo kunaweza kukufanya uokoe pesa

  • Kubadilisha na kutumia vitu muhimu vya nyumbani vinavyoendeleza uendelevu kama vile vitambaa vya kufanyia usafi vinavyoweza kuoshwa kunaweza kupunguza athari zako kwa mazingira

  • Kuweka vifaa vyenye mtiririko wa chini kunaweza kusaidia kuhifadhi maji

Kuwa Mwenyeji anayewajibika kwa mazingira si jambo zuri kwa sayari pekee, bali pia ni zuri kwa biashara yako ya kukaribisha wageni. Mwaka 2019, idadi ya sehemu za kukaa katika nyumba zinazotunza mazingira iliongezeka kwa asilimia 141* ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Ili kukusaidia kuwa Mwenyeji endelevu zaidi, tulishirikiana kwa karibu na United Nations Environment Programme, mamlaka inayoongoza kimataifa ya mazingira katika Umoja wa Mataifa na World Wildlife Fund, shirika linaloongoza duniani katika uhifadhi, kwa ufahamu wa kitaalamu. Pia tulikusanya ushauri kutoka kwa Wenyeji kote ulimwenguni ambao walichukua hatua rahisi lakini zenye matokeo ili kuleta mabadiliko.

Soma zaidi ili ugundue jinsi unavyoweza kuunda sehemu ya kukaa endelevu zaidi kwa ajili ya wageni wako.

Tekeleza maboresho ya kutumia nishati kidogo

Kufanya sehemu yako iwe inayotumia nishati kidogo zaidi kunaweza kupunguza kiasi cha rasilimali unazotumia, kupunguza gharama zako na kupunguza kiasi cha hewa ya ukaa unayozalisha. Haya ni baadhi ya mawazo ya kuhifadhi nishati:

  • Wakumbushe wageni wachomoe vifaa kwenye soketi wakati havitumiki: Hadi asilimia 50** ya nishati inayotumiwa na simu za mkononi hutoka kwenye chaja ambazo zimechomekwa kwenye soketi wakati hazitumiki.
  • Rekebisha hita yako ya maji: Ingawa hali-joto ya kawaida ya hita ya maji ni nyuzi 140 Farenhaiti (nyuzi 60 Selsiasi), kuishusha hadi nyuzi 120-130 Farenhaiti (nyuzi 48-54 Selsiasi) kunaweza kusaidia kuokoa nishati.
  • Angalia balbu zako za taa: Kutumia wati ya chini kabisa kunaweza kutoa joto kidogo na kupunguza matumizi yako ya nishati baada ya muda. Balbu za umeme zinazookoa nishati, kama vile CFL na LED, pia hutumia nishati kidogo na hudumu kwa muda mrefu** kuliko machaguo ya balbu za kawaida.
  • Linda sehemu yako dhidi ya hali mbaya ya hewa: Weka mikanda ya kuzuia hali mbaya ya hewa kwenye milango na ufunike madirisha kwa mipira ili kusaidia kuokoa gharama za kupasha joto na kupoza.
  • Nunua virekebisha-joto mahiri vyenye vidhibiti vya kiotomatiki: Virekebisha-joto vinavyowezeshwa na Wi-Fi vinaweza kukuruhusu kudhibiti hali-joto kulingana na kuwasili na kuondoka kwa wageni. 
  • Tathmini vifaa vyako: Wakati wa kununua vifaa vipya, chagua vifaa vyenye ukadiriaji wa juu wa kutumia nishati kidogo.

Chagua vitu muhimu vya nyumbani vinavyoendeleza uendelevu

Vifaa vya kufanya usafi vinavyoweza kutumika tena na bidhaa zinazoweza kujazwa tena ni fursa nzuri kwa watu wengi kupunguza athari zao za kimazingira. Zingatia vidokezi hivi vya kutunza mazingira:

  • Ondoa vifaa vya kufanyia usafi vya kutumika mara moja: Mwenyeji Bingwa Anna wa Pembrokeshire, Wales, huweka sifongo zinazoweza kuoshwa na kutumika tena na vitambaa vya kufanyia usafi vyenye nyuzinyuzi ndogo jikoni badala ya taulo za karatasi za kutumika mara moja na kutupwa.
  • Tumia bidhaa za karatasi zilizotumika tena: Kwa bidhaa zozote za karatasi unazotoa, kama vile tishu za uso au karatasi ya choo, chagua karatasi iliyotumika tena kwa asilimia 100 ili kutunza mazingira zaidi.
  • Punguza kemikali kali: Nunua sabuni ya kuoshea vyombo, sabuni ya kufulia na vifaa vya usafi wa mwili ambavyo havina sumu au vyenye kiwango cha chini cha sumu, vya asilia au vinavyoweza kuoza. Jijini Bordeaux, Ufaransa, Mwenyeji Bingwa Pascale hupata bidhaa za kuogea na za mwili kutoka kwenye maduka ya eneo husika.
  • Badilisha utumie nguo za asili: Wakati wa kubadilisha mashuka na taulo, kuchagua nguo za kikaboni kunaweza kukusaidia kuepuka dawa za kuua wadudu na sumu nyingine ambazo ni hatari kwa watu na mifumo ya ikolojia. 

Hifadhi maji

Kwa sababu maji safi ni rasilimali chache, ni muhimu kuzingatia ni kiasi gani cha maji wewe na wageni wako mnatumia, hasa kwa kuwa mgogoro wa tabianchi unachangia ukame zaidi. Hizi hapa ni baadhi ya njia zenye manufaa za kuhifadhi maji:

  • Acha vikumbusho kwa ajili ya wageni: Kupunguza muda wa kuoga kwa dakika moja kunaweza kuokoa zaidi ya galoni** moja ya maji kila dakika. Mwenyeji Bingwa Antonella jijini Milan, Italia, anaweka maelezo karibu na mifereji ya maji ili kuwahimiza wageni kufunga mifereji wanapopiga mswaki. Unaweza pia kuwahimiza wageni kuoga kwa muda mfupi.
  • Angalia uvujaji: Kukagua mara kwa mara maeneo karibu na vyoo, sinki, mabeseni na vifaa vinavyotumia maji kunaweza kukusaidia kugundua uvujaji. Mita janja ya maji inaweza kufuatilia kiasi cha maji unayotumia na kukujulisha ikiwa kuna shughuli isiyo ya kawaida, kwa mfano, ikiwa utasahau kufunga mfereji wa maji wa jikoni au iwapo kuna uvujaji kwenye mashine ya kuosha vyombo.
  • Tumia mipangilio na vifaa vinavyofaa: Mashine za kufulia na mashine za kuosha vyombo hutumia maji mengi. Ikiwa sehemu yako inayo, wahimize wageni watumie mipangilio ya kuosha haraka au ya kuhifadhi mazingira. Na wakati wa kubadilisha mashine, chagua mashine inayotumia nishati kidogo ambayo hutumia maji kidogo.
  • Weka vifaa vya mtiririko wa chini: Unaweza pia kuleta mabadiliko kwa kuweka mifereji yenye mtiririko wa chini na vyoo vya mtiririko wa chini au vyoo vya kupiga maji mara mbili. Huko Tasmania, Australia, Mwenyeji Bingwa Merrydith ana bomba maalumu la mvua ambalo hupunguza mtiririko wa maji huku bado ukipata shinikizo la juu.

*Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb za ukuaji wa mwaka kwa mwaka wa kuwasili kwa wageni kwenye nyumba ikiwemo maneno mahususi (kutunza mazingira, ikolojia, n.k.) katika vichwa na maelezo ya matangazo kuanzia mwezi Agosti 2018 hadi Agosti 2019

**Kutoka kwenye Vitendo 60 vya Dunia vya World Wildlife Fund, vilivyochapishwa tarehe 5 Machi, 2021

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Kuwekeza katika vifaa vinavyotumia nishati kidogo kunaweza kukufanya uokoe pesa

  • Kubadilisha na kutumia vitu muhimu vya nyumbani vinavyoendeleza uendelevu kama vile vitambaa vya kufanyia usafi vinavyoweza kuoshwa kunaweza kupunguza athari zako kwa mazingira

  • Kuweka vifaa vyenye mtiririko wa chini kunaweza kusaidia kuhifadhi maji

Airbnb
21 Apr 2021
Ilikuwa na manufaa?