Mwongozo wa mwenyeji wa kusaidia utalii endelevu

Saidia wageni wako kuwa wasafiri wenye kutunza mazingira kwa vidokezi hivi.
Na Airbnb tarehe 21 Apr 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 3 Apr 2025

Vidokezi

  • Warahisishie wageni kutumia usafiri wa umma kwa kujumuisha njia maarufu na taarifa ya nauli katika kitabu chako cha mwongozo

  • Angazia maswala ya mazingira ya eneo husika ambayo yanaweza kuathiri ukaaji wa wageni wako, kama vile moto wa misituni au mafuriko

  • Pendekeza biashara unazopenda katika eneo lako na masoko ya wakulima

Sehemu ya kuwa mwenyeji endelevu ni kukaribisha wageni wako kujiunga pia. Kwa sababu uendelevu unaweza kuwa ni jambo jipya kwao, ni muhimu kuelezea njia wanazoweza kuleta mabadiliko.

Ili kukusaidia katika kuwaelimisha wageni wako juu ya safari endelevu kwa mazingira, tumekusanya vidokezi kutoka kwenye jumuiya yetu ya ulimwengu ya Wenyeji na kufanya kazi na Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa, mtetezi mwenye mamlaka wa mazingira ya ulimwengu na Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni, shirika linaloongoza kwa uhifadhi.

Endelea kuoma ili ujue ni jinsi gani unaweza kukuza safari rafiki kwa mazingira.

Wasaidie wageni kufahamu jinsi ya kutumia usafiri wa umma

Safari fupi za gari zinawajibika kwa robo tatu* ya uzalishaji wa hewa chafu, kwa hivyo kuhamasisha wageni wako kutumia usafiri wa umma kunaweza kuleta matokeo makubwa.

Kwa kuwa kutembelea maeneo mapya kunaweza kuwa changamoto kwa wasafiri, wasaidie wageni kwa kuweka taarifa kuhusu basi, gari moshi za chini ya ardhi, au taarifa za gari moshi kwenye kitabu chako cha mwongozo, ikiwemo na makisio ya nauli na njia bora za kufikia sehemu maarufu za eneo husika na uwanja wa ndege. Unaweza pia kutoa baiskeli kwa wageni, au kupendekeza biashara ambapo wanaweza kukodisha.

Toa vyombo vinavyoweza kutumika tena

Vifaa vya plastiki hutengeneza taka nyingi na mara nyingi haziwezi kurejelezwa. Kwa sababu bidhaa za plastiki zina hatari sana kwa dunia, ni muhimu kuepuka kuzinunua pale inapowezekana.

Ili kuwakatisha tamaa wageni wasinunue vitu vya plastiki wakati wa ukaaji wao, Mwenyeji Bingwa Tiffany huko Hollywood Beach, California, hutoa vitu vinavyoweza kutumika tena kama vikombe na chupa za maji kwa wageni watumie. Huko Chiang Mai, Thailand, Mwenyeji Bingwa Nutth pia huwajulisha wageni mahali pa kujaza chupa za maji wanapokuwa katika kuzunguka mitaani.

Sahani zinazoweza kutumika tena, vyombo vya fedha na vyombo vya kuhifadhia chakula pia vinaweza kuwaruhusu wageni wako kufurahia chakula cha nje wakati wakipunguza uharibifu

Sifu biashara za eneo husika, ambazo ni rafiki kwa mazingira

Tumia mwongozo wako wa nyumba au kitabu cha mwongozo kuwaambia wageni kuhusu mkahawa wako endelevu uupendao, soko la wakulima, au duka linalouza bidhaa kutoka eneo husika na endelevu. Ikiwa kuna mazao ya msimu katika eneo lako, ongelea hilo pia. "Tuna mapendekezo mengi katika kitabu chetu cha mwongozo kuhusu mikahawa ya kupendeza ambayo inashiriki maadili yetu endelevu," anasema Mwenyeji Bingwa Anna anayeishi huko Pembrokeshire, Wales.

Unaweza hata kutoa kidokezi cha bidhaa za eneo husika ambazo pengine wageni wangependa kuangalia au kuchukua nyumbani kama ukumbusho. Huko Tasmania, Australia, Mwenyeji Bingwa Merrydith huacha asali iliyotengenezwa kwa mikono na sabuni ya lavenda kwa wageni watumie au kuchukua nyumbani.

Waelimishe wageni juu ya njia za kusafiri kwa uwajibikaji

Katika sheria zako za nyumba au mwongozo wa nyumba, unaweza kuomba wageni wapunguze upotevu, waoge kwa muda mfupi, kunywa maji ya bomba yaliyochujwa na kuweka thermostati katika viwango vilivyowekwa mapema. Unaweza pia kuweka maelezo kwenye sehemu yako ili kuwakumbusha wageni kuzima taa kabla hawajaondoka na kufunga maji wanapopiga mswaki.

Mwenyeji Bingwa Omar wa Mexico City huunda video ambazo wageni wanaweza kuzifikia kutoka kwenye msimbo wa QR zinazoelezea mchakato wa kurejeleza katika vyumba vyake na athari mbaya za plastiki ya matumizi ya wakati mmoja.

Sio tu kwamba mazoea haya yanaweza kuokoa pesa, pia yanaweza kuvutia wageni ambao wanajaribu kufanya safari endelevu.

Wajulishe wageni kuhusu maswala ya mazingira ya eneo husika

Jumuiya kote ulimwenguni zinaathiriwa na shida za mazingira kama moto wa misituni, mafuriko na hali ya hewa inayobadilika kupita kiasi. Kwa kutaja maswala ya eneo husika katika mwongozo wako wa nyumba, unaweza kuwaelimisha wageni wako juu ya jinsi ya kuwa wasafiri wenye kuwajibika—na uwajulishe hatari ambazo hawawezi kupata nyumbani, kama uchafuzi wa hewa au ukame.

Kwa mfano, katika maeneo yenye ubora duni wa hewa, ni bora kuepuka shughuli za nje katika siku za uchafuzi mkubwa wa mazingira au kushiriki katika shughuli zinazoongeza uchafuzi wa mazingira, kama vile kuendesha gari, kuchoma nyama, au kuwasha fataki.

Angazia jinsi tangazo lako lilivyo rafiki kwa mazingira

Kwa kusisitiza hatua unazochukua katika maelezo ya tangazo lako na mwongozo wako wa nyumba, unaweza kuwajulisha wageni watarajiwa unajali mazingira.

Ikiwa unawapa wageni vitu kama sabuni ya mikono inayoweza kuvundishwa na bakteria au chupa za maji zinazoweza kutumika tena, kumbuka kuonyesha hilo katika tangazo lako pia.

Kuingiza mawazo haya katika utaratibu wako wa kukaribisha wageni kunaweza kusaidia kuleta matokeo kwenye dunia—na kuruhusu wageni kupata uzoefu wa maisha kama wakazi. Tunajua kuwa kufuata mazoea endelevu huchukua muda, kwa hivyo tunakusanya nyenzo zaidi ili kukusaidia njiani.

KIFUATACHO:Jifunze jinsi Mwenyeji Bingwa mmoja anakuwa endelevu zaidi

*Kutoka kwenye chapisho la Mfuko wa Wanyamapori Ulimwenguni linaloitwa
60 Actions for the Planet , lililochapishwa tarehe 5 Machi, 2021

Taarifa iliyo katika makala hii inaweza kuwa imebadilika tangu kuchapishwa.

Vidokezi

  • Warahisishie wageni kutumia usafiri wa umma kwa kujumuisha njia maarufu na taarifa ya nauli katika kitabu chako cha mwongozo

  • Angazia maswala ya mazingira ya eneo husika ambayo yanaweza kuathiri ukaaji wa wageni wako, kama vile moto wa misituni au mafuriko

  • Pendekeza biashara unazopenda katika eneo lako na masoko ya wakulima

Airbnb
21 Apr 2021
Ilikuwa na manufaa?