Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Kuweka na kuhariri vistawishi ni rahisi kuliko hapo awali

Tumeanzisha machaguo mapya ya vistawishi—na njia mpya za kuziweka kwenye tangazo lako.
Na Airbnb tarehe 7 Des 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 15 Jun 2021

Vidokezi

  • Tumeweka machaguo mapya 40 na zaidi ya vistawishi, ili wageni wajue cha kutarajia

  • Sasa unaweza kuwavutia wageni wanaotafuta vistawishi kama vile "mandhari nzuri" na "ufikiaji wa ufukwe," pamoja na maelezo kama vile aina ya kifaa cha kutengeneza kahawa unachotoa

  • Tumefanya pia iwe rahisi kuhariri maelezo ya tangazo lako kwa kutumia mpangilio mpya

Maelezo madogo ya tangazo, kuanzia aina ya kahawa ambayo mgeni anapewa hadi mandhari ambayo anaona kila asubuhi, yanaweza kuathari sana safari. Tunataka kukurahisishia kuwaambia wageni watarajiwa zaidi juu ya huduma maalum zinazotolewa na nafasi yako, kukusaidia kuweka matarajio na kutoa kukaa nyota tano. Ndiyo sababu tumeweka machaguo mapya ya vistawishi zaidi ya 40, pamoja na njia mpya za kuwa mahususi zaidi na kuhariri maelezo ya tangazo lako.

Wageni wanaweza kutafuta matangazo yaliyo na vistawishi mahususi, kwa hivyo vipengele hivi vipya vinakusaidia kuwavutia wageni bora kwa ajili ya mpangilio wako.

Onyesha chumba kilicho na uwezo wa kuona mandhari

Kipengele unachojivunia zaidi kinaweza kuwa eneo la msitu lililo nje ya dirisha la sebule yako au mandhari ya bahari kutoka kwenye chumba chako cha kuotea jua, kwa hivyo tumeweka "mwonekano wa mandhari nzuri" kwenye machaguo ya vistawishi. Sasa unaweza kuifanya nyumba yako ionekane, iwe ina mwonekano wa mlima, mwonekano wa ziwa au hata mwonekano wa sehemu ya ziwa. Wageni wataweza kupata matangazo yanayoonyesha mandhari wanazozipenda—na utaweza kuweka matarajio halisi ya jinsi mwonekano huo ulivyo.

Unaweza kuweka mandhari nzuri katika sehemu ya 'Maelezo ya Tangazo' ya Simamia Sehemu Yako. Chagua tu tangazo lako ili kuhariri.

Chagua kutoka miongoni mwa vistawishi vipya zaidi ya 40

Iwe sehemu yako inaonyesha jiko la nje, ukumbi au mashine ya kutengeneza maji ya matunda asubuhi,wageni wanataka kujua kuhusu hilo. Hapa kuna machaguo kadhaa ya vistawishi unavyoweza kuchagua:

  • Ufikiaji wa ufukwe
  • Ufikiaji wa risoti
  • Vifaa vya mazoezi
  • Kitanda cha bembea
  • Vifaa vya kusoma

Wageni wanapojua nini cha kutarajia wakati wa ukaaji wao, wanaweza kupanga mapema. Na kuweka matarajio ni muhimu: Tumejifunza kutoka kwa Wenyeji Bingwa wetu kwamba si lazima nyumba yako iwe kamilifu—lakini ni muhimu kuwaambia wageni hasa kile watakachopata watakapowasili.

Tumepanga katika makundi vistawishi maarufu zaidi ili kukusaidia kupata na kuvichagua kwa kuvitupia jicho. Kwa mfano, sasa unaweza kuonyesha kwamba eneo lako lina Wi-Fi, televisheni, sehemu mahususi ya kufanyia kazi, mashine ya kufua nguo, kiyoyozi na kadhalika—zote katika sehemu moja.

Tumeendelea kupanga makundi ya vistawishi kulingana na eneo ili uweze kuendelea kuchagua vistawishi vyako vyote vya jikoni mara moja, lakini tumeweka sehemu maarufu ya vistawishi ili kufanya iwe rahisi hata zaidi kuwaambia wageni kwamba una vipengele wanavyotafuta mara nyingi.

Wajulishe wageni wako mambo mahususi

Hapo awali kwenye Airbnb, ungeweza kutumia kipengele cha vistawishi ili kuwajulisha wageni kwamba unatoa sehemu mahususi ya kufanyia kazi au sehemu ya nje kama vile ukumbi. Lakini sasa unaweza kuwapa wageni watarajiwa maelezo hata zaidi. Kwa mfano, unaweza kuwasaidia wafanyakazi wa mbali kupata sehemu inayowafaa kwa kubainisha kwamba ina dawati, kompyuta, kiti cha ofisi, au meza na unaweza kuwajulisha wageni ikiwa ukumbi ni wa kujitegemea au ni wa pamoja.

Unaweza pia kutaja mambo mahususi kuhusu vistawishi kadhaa vingine, ikiwemo:

  • Huduma za utiririshaji na vifaa, ikiwemo Apple TV, Netflix, Disney+ na kadhalika
  • Mashine ya kutengeneza kahawa, iwe ni ya matone, Keurig au espresso
  • Nyama choma, kuanzia chaguo la mkaa hadi kuni
  • Kwa mfano, meko ya ndani, iwe ni ya umeme au ya kuni
  • Mifumo ya kupasha joto na baridi

Ikiwa vistawishi vinabadilika kwenye tangazo lako, sasa ni rahisi kwako kuvibadilisha haraka, ikikuruhusu uendelee kuzingatia kile unachofanya vizuri zaidi—kutoa ukaribishaji bora kwa wageni wako.

Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Tumeweka machaguo mapya 40 na zaidi ya vistawishi, ili wageni wajue cha kutarajia

  • Sasa unaweza kuwavutia wageni wanaotafuta vistawishi kama vile "mandhari nzuri" na "ufikiaji wa ufukwe," pamoja na maelezo kama vile aina ya kifaa cha kutengeneza kahawa unachotoa

  • Tumefanya pia iwe rahisi kuhariri maelezo ya tangazo lako kwa kutumia mpangilio mpya
Airbnb
7 Des 2020
Ilikuwa na manufaa?