Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Njia 10 za kutoa mchango wakati wa sikukuu na baada ya hapo

  Tenda mema kupitia mipango ya uhisani ya Airbnb na uhamasishwe na wenyeji wengine.
  Na Airbnb tarehe 13 Nov 2019
  Inachukua dakika 5 kusoma
  Imesasishwa tarehe 21 Apr 2021

  Vidokezi

  • Sikukuu ni wakati mzuri wa kuzingatia shukrani na utoaji

   • Kupitia Airbnb, wenyeji wanaweza kutoa sehemu zao kwa wenye uhitaji, watoe mchango wa sehemu ya nafasi zao zilizowekwa na kujaribu Tukio la Wajibu kwa Jamii

   • Pata maelezo kuhusu jinsi ambavyo wenyeji wengine wanaleta mabadiliko na utafute njia za kushiriki katika jumuiya yako mwenyewe

    Sikukuu ni wakati wa sherehe wa kuwa pamoja na familia na marafiki, lakini pia ni fursa nzuri ya kuzingatia shukrani na kutoa. Hujui uanzie wapi? Angalia baadhi ya mipango ya uhisani ya Airbnb na upate msukumo kwa kile ambacho wenyeji wenzako tayari wanafanya ili kusaidia kuufanya ulimwengu uwe mahali pazuri zaidi.

    1. Wakaribishe kwako wale wenye uhitaji

    Maelfu ya wenyeji wakarimu ulimwenguni kote wamejiunga na mpango wetu wa Open Homes, ambao unawaruhusu wenyeji kama wewe kutoa sehemu zao kwa watu wanaohitaji makazi ya muda. Iwe ni kuwasaidia wageni wanaosafiri kwa ajili ya matibabu, wakimbizi ambao wanaingia katika jiji jipya, manusura wa majanga ya asili, au wafanyakazi wa misaada ambao wanahitaji mahali pa kukaa, unaweza kuleta mabadiliko. Toa sehemu yako bila malipo

    2. Toa kidogo kila wakati unapokaribisha wageni

    Kwa kuzingatia roho ya Jumanne ya Ukarimu—siku ya kimataifa ya utoaji wa hisani inayotukia Jumanne baada ya siku ya Kutoa Shukrani nchini Marekani—fikiria kujiunga na mpango wetu mpya wa Michango, unaokuruhusu kutoa mchango wa sehemu ya nafasi zako zilizowekwa kwa mwaka mzima kwa mashirika yasiyotengeneza faida ambayo yanashirikiana na Open Homes.

    Jinsi inavyofanya kazi: Unaamua asilimia unayotaka ikatwe kiotomatiki kutoka kwenye kila malipo ili utoe mchango na asilimia 100 ya mchango wako unaenda kwa mashirika yasiyotengeneza faida ambayo hutumia fedha hizo kuwasaidia watu wenye uhitaji kupata makazi ya muda. Hivi sasa mpango huu unatolewa tu nchini Marekani, Meksiko, Uhispania, Japani, New Zealand, Thailand, Malaysia na Sri Lanka, lakini timu yetu inafanya kazi ili kuupanua mpango huu ufikie nchi zaidi hivi karibuni, kwa hivyo endelea kutarajia. Anza kutoa mchango

    3. Kuwa mgeni—kwa malengo mazuri

    Yasaidie mashirika yasiyotengeneza faida kwa kushiriki katika mojawapo ya Matukio ya Wajibu kwa Jamii takribani 700 ulimwenguni kote. Unaweza kugundua hifadhi ya kasuku huko Hawaii, ujisajili kwa ajili ya mafunzo ya sanaa ya nakshi huko Washington, DC, ziara ya matembezi ya watetezi wa mfumo jike huko London, jiunge na safari ya mtumbwi ya asubuhi na mapema huko Mexico City na kadhalika. Tunasamehe ada yetu ya huduma ya asilimia 20 kwa wenyeji wa mashirika yasiyotengeneza faida, kwa hivyo asilimia 100 ya kile unachotumia kwenye tukio kitaenda moja kwa moja kwa shirika hilo lisilotengeneza faida. Jisajili kwa ajili ya Tukio la Wajibu kwa Jamii

    4. Sambaza habari

    Ikiwa unajua shirika lisilotengeneza faida linaloweza kufaidika kutokana na kuandaa Tukio la Wajibu kwa Jamii, lielekeze hapa ili kupata maelezo zaidi kuhusu mpango huu.

    5. Ungana na wenyeji wengine ili kuleta mabadiliko

    Wajue wenyeji wengine katika jumuiya yako kwa kujiunga na kilabu cha wenyeji na kujitolea kama kundi kwa mwaka mzima. Hapa kuna yale ambayo baadhi ya vilabu vya wenyeji vimefanya hivi karibuni kama sehemu ya Wiki ya Kutenda Wema, mpango wa kujitolea wa kila mwaka wa Airbnb, wakati wenyeji, wafanyakazi na mashirika yasiyotengeneza faida hushirikiana ili kuzitumikia jumuiya:

    • Huko Seville, Uhispania, kilabu cha wenyeji kilikutana na shirikisho ambalo huwaunganisha wahamiaji na mashirika ya ndani kwa ajili ya misaada ya maendeleo na mipango ya usawa.
    • Kilabu cha wenyeji huko Cape Town kilifanya kazi na shirika la eneo husika ili kutengeneza mpango wa utekelezaji wa miezi sita ili kuendesha uanuwai na ujumuishaji katika jumuiya yao ya Airbnb.
    • Kama sehemu ya Siku ya Usafi Duniani 2019, kilabu cha wenyeji huko Naples, Italia, kilisafisha kitovu cha kihistoria cha jiji kama shughuli yao ya kwanza ya kujitolea.

    6. Zingatia dunia kwanza

    Kuanzia kusafisha fukwe hadi kukarabati fanicha, wenyeji ulimwenguni kote wanafanya sehemu yao katika kulinda mazingira:

    • Remba kwa vitu vilivyokarabatiwa: "Ninapenda kuchukua fanicha barabarani au kwenye soko la mtumba na kuzirekebisha." —Delphine, Paris
    • Punguza na utumie tena: Bryan huko Feltham, Uingereza, anashirikiana na Freecycle, "mfumo wa mtandaoni wa kuondoa vitu kwenye jalala kwa kuvitumia tena."
    • Acha plastiki: Wenyeji Perrine na Maxime kutoka Plouézec, Ufaransa, hutengeneza bidhaa zao wenyewe zinazoweza kutumika tena, kama vile karatasi za nta za kuhifadhia vitu badala ya kutumia mfuko wa plastiki. Celine kutoka Saumur, Ufaransa, hununua vitu kwa wingi na hubeba mifuko ya nguo, vyombo vinavyoweza kutumika tena na chupa akienda sokoni.
    • Okota takataka: Leticia kutoka Cancún, Meksiko, husafisha fukwe, kama anavyofanya Elena kutoka Palamós, Uhispania, ambaye anasema: “Kama sheria, kila ninapoenda kwenye mojawapo ya fukwe zetu, mimi huokota angalau vipande vitano vya takataka ninazopata: plastiki, vichungi vya sigara, nk. ”

    7. Isaidie jumuiya yako

    Pata msukumo kutoka kwa wenyeji hawa ambao wamejitolea kuzifanya jumuiya zao kuwa na nguvu na mahiri zaidi:

    • Zisaidie shule: "Tumetoa vitabu kwa ajli ya maktaba yao na vitafunio kwa watoto." —MariaEsperanza, Bogota, Kolombia
    • Hifadhi historia ya eneo husika: Linda na Richard hujitolea kwenye Jumuiya ya Uhifadhi ya San Antonio na kusaidia kuhifadhi majengo ya kihistoria, maeneo na desturi zinazohusiana na historia ya Texas.
    • Jisajili kwenye shirika la eneo husika: Till na Jutta kutoka Stuttgart, Ujerumani, hujitolea kwenye bodi ya ushirika ya eneo lao ya mvinyo, matunda na kilimo cha bustani.

    8. Kuwa mtetezi wa wanyama

    Wenyeji hawa huwasaidia wanyama vipenzi wetu:

    • Yasaidie makundi ya uokoaji wa wanyama: Federico kutoka Ronchi dei Legionari, Italia, anajitolea katika hifadhi. Wenyeji wa Ujerumani Sybille na Harry kutoka Hamburg na Ralf kutoka Inzell husaidia hifadhi kwa kutoa mchango wa vitu vilivyotumika kama vile taulo na mashuka.
    • Pigania haki zao: Alexandra kutoka Lincoln, Kanada, husaidia kuendesha kundi linaloendeleza haki za wanyama nchini Uhispania na hutafuta makao mapya kwa ajili ya mbwa waliotelekezwa.
    • Saidia spishi zilizo hatarini: "Ninasaidia kumtunza mmoja wa ndege adimu sana wa New Zealand kwa ajili ya Idara ya Uhifadhi: Ndege wetu aina ya Fairy Tern aliye katika hatari sana (idadi ya 35), kupitia elimu kwa umma, ufuatiliaji wa viota na kuwatega wanyama wawindaji wabaya." —Ria, Northland, New Zealand

    9. Toa msaada wa moja kwa moja

    Kuanzia kutoa mahitaji ya msingi hadi kujenga shule, wenyeji hawa wanaleta mabadiliko:

    • Kabidhi vitu vilivyotolewa mchango: Yuni na Erick kutoka Havana, Kyuba, wanatembelea vitongoji maskini wakiwa na wageni wa Airbnb ambao wameleta nguo, viatu, dawa, midoli na vitu muhimu vya kusambaza.
    • Saidia kupambana na njaa: Ana na Juan hujitolea kwenye Benki ya Chakula ya Barcelona nao wanasaidia kupanga kampeni ya kila mwaka ya kukusanya chakula wakati wa Krismasi.
    • Chukua nyundo: Marco kutoka Liguria, Italia, alijenga shule ya chekechea na husaidia kazi katika hospitali moja barani Afrika.

    10. Wasaidie watoto na wazee

    Angalia jinsi wenyeji hawa wanavyotoa ujuzi wao, huduma na wakati:

    • Mfundishe mtu kusoma na kuandika: "Kuna watoto wengi sana ambao hawana fursa ya kuendeleza ustadi wao wa lugha, kwa hivyo tunasaidia popote pale palipo na uhitaji."—Clara kutoka Pensacola, Florida
    • Tumia wakati pamoja na watoto wenye uhitaji: "Tunawatembelea mara nyingi iwezekanavyo, tunawapelekea midoli watoto wote, tunahakikisha wanaenda kwenye sinema na kupata chakula kizuri cha jioni na pia tunatoa mchango mdogo kwa malezi yao."—Gordon kutoka London, ambaye hutumia wakati katika makao ya watoto yatima walio na VVU huko Caracas, Venezuela
    • Mpe mtu lifti: "Ninawatembelea wagonjwa na wazee kila wiki na kutoa huduma za kusafiri kwa watu wasiotembea."—Monika, Vienna

    Tunatumaini masimulizi haya yatakuchochea uhusike katika jumuiya zako mwenyewe msimu huu wa sikukuu na baadaye—njoo na wageni wako pia!

    Taarifa iliyo katika makala hii inaweza kuwa imebadilika tangu kuchapishwa.

    Vidokezi

    • Sikukuu ni wakati mzuri wa kuzingatia shukrani na utoaji

     • Kupitia Airbnb, wenyeji wanaweza kutoa sehemu zao kwa wenye uhitaji, watoe mchango wa sehemu ya nafasi zao zilizowekwa na kujaribu Tukio la Wajibu kwa Jamii

     • Pata maelezo kuhusu jinsi ambavyo wenyeji wengine wanaleta mabadiliko na utafute njia za kushiriki katika jumuiya yako mwenyewe

      Airbnb
      13 Nov 2019
      Ilikuwa na manufaa?