Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

    Boresha picha za tangazo lako

    Wapiga picha wawili wa kitaalamu wanaelezea njia tano za kufanya tangazo lako la Airbnb lieonekane.
    Na Airbnb tarehe 26 Jul 2022
    Inachukua dakika 7 kusoma
    Imesasishwa tarehe 26 Jul 2022

    Vidokezi

    • Chagua picha ya jalada inayozingatia haiba ya sehemu yako

    • Ondoa mparaganyo, piga picha kwa usawa wa macho na uweke picha yako vizuri kwenye fremu

    • Gundua mengi zaidi katika mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

      Je, unajua kuwa picha ni mojawapo ya visababishi vikuu vya kufanya uamuzi kwa wageni wanapochagua sehemu ya kukaa? Ubora wa picha zako pia unaweza kuathiri kuhusu mara ngapi wageni watarajiwa wanapata tangazo lako katika matokeo ya utafutaji, jambo ambalo linamaanisha kwamba picha za ubora wa juu ni muhimu kwa biashara yako ya kukaribisha wageni.

      Jeff na Candida ni wapiga picha wa kitaalamu na Wenyeji Bingwa ambao hutumia ubunifu wao ili kuvutia nafasi zaidi zinazowekwa kwenye makao yao ya jangwani, El Rancho, huko Joshua Tree, California. Siri yao ni kufanya sehemu yao ionekane kuwa nzuri katika picha kama ilivyo katika hali halisi.

      Hapa, wanandoa hao wanashiriki vidokezi vyao vya kitaalamu ili kuboresha picha za tangazo lako.

      1. Ondoa mparaganyo

      Unapopiga picha ya sehemu yako, hakikisha kudumisha unadhifu. "Wakati mwingine tunashangaa kuona watu wengi wakisahau kuondoa mparaganyo kwenye sehemu zao kabla ya kupiga picha," anasema Jeff. Tunajaribu kuondoa mparaganyo kwenye sehemu zetu za kuishi, kwa hivyo kupiga picha tunayotaka—bila vikengeusha fikira—kunakuwa rahisi zaidi.”

      Hata hivyo, hiyo haimaanishi kwamba sehemu yako isiwe kabisa na kitu chochote. "Ongeza kipengele kinachoashiria uwepo wa binadamu kwenye picha," anasema Candida, kama vile blanketi au safu ya vitabu. "Inafanya eneo hilo kuashiria ukaribisho zaidi.”

      2. Weka picha yako ya jalada kwenye fremu

      Picha ya jalada ya sehemu yako ndio kitu cha kwanza ambacho wasafiri hugundua katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo, kwa hivyo jaribu kufanya picha hiyo ivutie.

      “Fikiria kile kinachofanya sehemu yako iwe tofauti na nyinginezo. Je, nini kinafanya iwe ya kipekee? Je, unafikiri watu wataweza kujiwazia wakiwa hapa? Chunguza matangazo mengine ya Airbnb ili upate hamasa na ujue kile kinachofaa,” Candida anapendekeza.

      Hakikisha pia unapiga picha za maeneo yoyote ya kipekee ambayo yanaweza kuwavutia wageni watarajiwa, kama vile picha pana ya sehemu ya nje ya nyumba yako.

      3. Pata mwangaza wako

      "Siri ya kuwa na picha nzuri za tangazo ni mwangaza," Candida anasema. Haya ni mapendekezo kadhaa ya kuonyesha sehemu yako ikiwa na mwangaza unaofaa:

      • Angalia mwangaza wako. Fanya majaribio na uchunguze jinsi mwangaza wa asili unavyoonekana ndani na nje ya nyumba yako mchana kutwa.
      • Piga picha wakati wa jioni au alfajiri. Unapopiga picha ukiwa nje, piga picha baada tu ya jua kuchomoza au kabla ya jua kutua, huo ndio wakati bora. Mwangaza ni laini na si wa moja kwa moja na utaipa nyumba yako sura nzuri, yenye kuvutia.
      • Tumia mazingira ya asili. Ikiwa unapiga picha ndani ya nyumba, tafuta wakati wa mchana ambapo utapata mwangaza wa moja kwa moja na wa asili zaidi. Mwangaza bandia unapaswa kuwa suluhisho la mwisho kila wakati, kwani unaonekana kuwa mkali sana kwenye picha.
      • Zima mweko Kama ilivyo kwa mwangaza mwingine usiao wa asili, kutumia mweko kunaweza kuleta mwonekano mkali. Ikiwa sehemu unayopiga picha haina mwangaza wowote wa asili, washa taa ili kuunda mwonekano wa starehe.

      4. Tunga muundo wako

      Inapohusu ubora wa picha, muundo, vitu kama vile mwelekeo, ukubwa wa picha, mpangilio na ulinganifu, ni muhimu kama vile tu mada ya picha yako. Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kuzingatia wakati wa kubuni muundo wako:

      • Weka picha zako katikati ya fremu. Kumbuka kwamba Airbnb hupunguza picha ili zitoshee kwenye tangazo lako na katika matokeo ya utafutaji. Weka kitu kikuu unachokipiga picha katikati ya fremu ili kitu chochote muhimu kisikatwe. "Ikiwa una vitu vya kipekee ambavyo unavipenda nyumbani kwako, jaribu kuviweka katikati kwenye picha ili viweze kuonekana," anasema Jeff.
      • Piga picha kwenye usawa wa macho. Kupiga picha yako kwa pembe isiyoegemea upande wowote, bila kupotosha au kuelekeza juu au chini, huhakikisha kwamba picha iko sawa na inaruhusu wageni kupata uzoefu na kuihisi sehemu hiyo kana kwamba wapo hapo kihalisi.
      • Tumia kanuni ya theluthi. "Ukigawanya fremu yako katika theluthi, unaweza kuzitumia kama miongozo ya kupanga vitu katika muundo wako," Jeff anasema.
      • Jumuisha picha za aina mbalimbali. Picha pana ni bora kwa kuwasaidia watu kuelewa ukubwa wa chumba, ilhali picha za ukubwa wa wastani ni bora kwa kuzingatia vitu mahususi, kama vile televisheni au baiskeli ya mazoezi. Tenga picha zinazoonyesha mambo madogo madogo kwa ajili ya vitu vinavyoonyesha hulka yako.
      • Husianisha. Fikiria albamu ya picha zako kama ziara ya kuelekezwa na uwaonyeshe wageni watarajiwa jinsi vyumba vinavyohusiana kwenye picha.

      5. Onyesha sehemu yako

      Unapochagua nini cha kupiga picha na nini cha kuacha, jaribu kufikiria kama mgeni.

      "Ni muhimu kupanga na kuchagua picha mbalimbali zinazosimulia sehemu yako vizuri," anasema Candida. "Je, wageni wako watapenda nini kuhusu sehemu hiyo? Ni vitu gani vya kushangaza ambavyo wanaweza kuhitaji kujua? Unawezaje kuonyesha maelezo lakini bado uonyeshe kwa ujumla vile chumba kinavyoonekana?"

      Kumbuka kwamba sehemu ya kusimulia sehemu yako ni kuvuta picha mbali na kunasa mandhari ya eneo lako jirani. "Si lazima kila picha ihusu nyumba yako pekee," Jeff anabainisha. Kwa mfano, unaweza kujumuisha picha za njia ya matembezi iliyo karibu au mkahawa mzuri ulio karibu na sehemu yako.

      Muhimu zaidi, unaposhiriki sehemu yako na eneo jirani, tumia picha zenye ubora wa hali ya juu ili kuwasaidia wageni watarajiwa waone vile ukaaji wao utakavyokuwa na ikiwezekana, waweke nafasi kwenye eneo lako kwa ajili ya ukaaji watakaokumbuka.

      Taarifa iliyo katika makala hii inaweza kuwa imebadilika tangu kuchapishwa.


      Vidokezi

      • Chagua picha ya jalada inayozingatia haiba ya sehemu yako

      • Ondoa mparaganyo, piga picha kwa usawa wa macho na uweke picha yako vizuri kwenye fremu

      • Gundua mengi zaidi katika mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

        Airbnb
        26 Jul 2022
        Ilikuwa na manufaa?