Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Jaribu nyenzo zetu za kupanga bei

Dhibiti bei yako kwa kutumia mapunguzo, promosheni na bei mahususi.
Na Airbnb tarehe 9 Jan 2025
Imesasishwa tarehe 9 Jan 2025
Jaribu nyenzo zetu za kupanga bei
Kwa kutumia kalenda yako
Jaribu nyenzo zetu za kupanga bei

Nyenzo za kupanga bei za Airbnb hufanya iwe rahisi kwako kurekebisha bei yako. Utaipata katika kalenda yako.

Nyenzo za kupanga bei na mipangilio ya upatikanaji mara nyingi hufanya kazi pamoja. Ikiwa unataka kutumia nyenzo fulani, kama vile kutoa mapunguzo ya kila mwezi, huenda ukalazimika kubadilisha upatikanaji wako, kama vile kuruhusu sehemu za kukaa za muda mrefu.

Kurekebisha bei yako

Kutathmini na kurekebisha bei yako mara kwa mara kunaweza kukusaidia kutimiza malengo yako ya mapato.

Unaweza kuhariri bei yako ya msingi wakati wowote kwenye kalenda ya tangazo lako. Unapobofya nambari ili kuibadilisha, utaona bei ya wageni kabla ya kodi na kile unachopata baada ya ada ya huduma ya mwenyeji.

Una njia nyingine mbili za kuboresha bei yako ya msingi.

  • Bei mahususi ya wikendi: Una chaguo la kuweka bei tofauti kwa usiku wa Ijumaa na Jumamosi. Kubadilisha bei yako kulingana na usiku kunaweza kusaidia kuongeza nafasi zinazowekwa.
  • Upangaji Bei Kiotomatiki: Washa nyenzo hii wakati wowote ili urekebishe bei yako kulingana na uhitaji wa eneo lako. Inatumia mamia ya vigezo kuhusu tangazo lako, eneo lako na tabia ya wageni. Unaweza pia kuweka bei zako za chini na za juu za kila usiku.

Kutoa punguzo na promosheni

Kuondoa asilimia fulani kwenye bei yako ya msingi kwa aina fulani ya nafasi zilizowekwa ni njia nyingine ya kuwavutia wageni. Kuna mapunguzo manne yanayopatikana kwenye kalenda ya tangazo lako.

  • Kila wiki: Mapunguzo kwa ajili ya ukaaji wa usiku saba au zaidi yanaweza kusaidia kuboresha nafasi yako kwenye matokeo ya utafutaji, kujaza nafasi kwenye kalenda yako na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka. Wageni wanaona wito maalumu kwa mapunguzo ya kila wiki ya asilimia 10 au zaidi. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya ile yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.
  • Kila mwezi: Unaweza pia kutoa punguzo kwa ajili ya ukaaji wa usiku 28 au zaidi. Hii inaweza kuongeza muda wa wastani wa kukaa katika matangazo yako yote na kupunguza idadi ya wageni wanaotoka. Wageni wanaona wito huo huo maalumu kwa mapunguzo ya kila mwezi ya asilimia 10 au zaidi.
  • Watakaowahi: Mapunguzo kwa nafasi zilizowekwa mwezi 1 hadi 24 kabla ya kuingia yanaweza kukusaidia uwavutie wageni wanaopanga mapema. Kwa mapunguzo kwa watakaowahi ya asilimia 3 au zaidi, wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo.
  • Dakika za mwisho: Mapunguzo kwa nafasi zilizowekwa siku 1 hadi 28 kabla ya kuingia yanaweza kusaidia kujaza kalenda yako na kuongeza mapato yako. Kwa mapunguzo ya asilimia 10 au zaidi kwenye bei yako ya wastani ya siku 60, wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo.

Kuweka mapunguzo ya muda mfupi kunaweza kukusaidia kuwekewa nafasi zaidi bila kubadilisha bei yako ya msingi. Kulingana na ustahiki wako, unaweza kuona hadi aina mbili za promosheni.

  • Promosheni ya tangazo jipya: Toa punguzo la asilimia 20 kwenye nafasi zako tatu zijazo zitakazowekwa kwenye tangazo jipya ili kukusaidia kupata wageni wako wa kwanza na tathmini.
  • Promosheni mahususi: Chagua tarehe zako na punguzo ambalo ungependa kutoa. Baadhi ya matakwa yanatumika, ikiwemo kwamba tangazo lako lazima liwe na angalau nafasi tatu zilizowekwa na angalau moja katika mwaka uliopita na tarehe unazochagua zinahitaji kuwa zimepatikana kwa angalau siku 28. Wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo unapotoa punguzo la asilimia 15 au zaidi.

Kuweka ada za hiari

Unaweza kuweka aina tatu za ada kwenye bei yako. Kumbuka kwamba ada huongeza bei yako ya jumla na zinaweza kuwazuia wageni wasiweke nafasi na hivyo kupunguza mapato yako.

  • Ada ya usafi: Hii ni ada ya mara moja ambayo inaongeza jumla ya bei ya ukaaji na inaonekana kama tozo tofauti wakati wa kulipa. Una chaguo la kuweka ada ya chini ya usafi kwa ukaaji ambao ni usiku mmoja hadi mbili.
  • Ada ya mnyama kipenzi: Una chaguo la kutoza ada hii kwa kila mnyama kipenzi, kwa kila usiku au kwa kila ukaaji. Huwezi kumtoza mgeni ada ya mnyama kipenzi kwa ajili ya Mnyama wa Huduma na wageni hawahitajiki kufichua uwepo wa Mnyama wa Huduma kabla ya kuweka nafasi. Pata maelezo zaidi kuhusu Sera ya Ufikiaji ya Airbnb.
  • Ada ya mgeni wa ziada: Unaweza kutoza ada ya usiku kwa kila mgeni zaidi ya idadi fulani. Kwa mfano, unaweza kuwaruhusu wageni sita wakae kwa bei yako ya kila usiku, lakini utoze USD 10 ya ziada kwa kila usiku kwa kila mgeni wa ziada hadi kiwango cha juu cha idadi yako ya wageni.

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Jaribu nyenzo zetu za kupanga bei
Kwa kutumia kalenda yako
Jaribu nyenzo zetu za kupanga bei
Airbnb
9 Jan 2025
Ilikuwa na manufaa?