Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Kurahisisha ada za huduma za Airbnb

Wenyeji wanaotumia programu ya usimamizi wa nyumba wanabadilisha kwenda ada moja.
Na Airbnb tarehe 22 Ago 2025
Imesasishwa tarehe 22 Ago 2025

Tunarahisisha muundo wetu wa ada ili kufanya iwe rahisi kwa wenyeji kuweka bei. Pata maelezo kuhusu kinachobadilika na jinsi ya kutobadilisha malipo unayotumiwa.

Jinsi ada za huduma zinavyofanya kazi

Leo, wenyeji na wageni kwa kawaida hulipa ada za huduma. Kwa sababu hiyo, unaweka bei moja lakini wageni wako hulipa bei ya juu ambayo inajumuisha ada yao ya huduma.

Tarehe 27 Oktoba, wenyeji ambao husimamia bei kwa kutumia usimamizi wa nyumba au programu ya usimamizi wa chaneli watabadilisha kwenda kwenye ada moja, ambapo wenyeji wanaweka bei ambayo wageni wnaiona na kulipa. Kujua kile ambacho wageni wako hulipa hufanya iwe rahisi kuweka bei yenye ushindani.

  • Ada ya kugawanya: Leo, ada ya mwenyeji ya asilimia 3 inakatwa kwenye bei yako ili kukokotoa malipo unayotumiwa.* Aidha, wageni hulipa ada ya huduma ya asilimia 14.1 hadi 16.5 pamoja na bei yako. Kwa mfano, ikiwa uliweka bei yako kuwa USD 100, unapata USD 97 na wageni wako wanalipa takribani USD 115.
  • Ada moja: Tarehe 27 Oktoba, ada ya huduma ya asilimia 15.5 itakatwa kwenye bei yako ili kukokotoa malipo unayotumiwa. Ada hii moja inategemea ada za wastani za huduma za Airbnb ulimwenguni, ambazo kwa sasa zimegawanywa kati ya wenyeji na wageni. Kwa mfano, ukirekebisha bei yako kuwa USD 115 ili kushughulikia ada moja, utajipatia USD 97.18 na wageni wako watalipa USD 115.

Katika mifano yote miwili, kile unachojipatia na kile ambacho wageni wako hulipa ni sawa.

Kutathmini bei zako

Fikiria iwapo ungependa kufanya mabadiliko yoyote kwenye bei zako ili kuzingatia muundo mpya wa ada.

  • Rekebisha bei zako: Unaweza kutaka kubadilisha bei zako ili udumishe malipo unayotumiwa na kiasi ambacho wageni wanalipa sawa na ilivyokuwa hapo awali. Kama ilivyoonyeshwa hapo juu, ukirekebisha bei yako kutoka USD 100 hadi USD 115, utajipatia USD 97.18 na wageni wako watalipa USD 115.
  • Weka bei zako sawa: Utajipatia mapato kidogo kwa kila usiku na wageni wako watalipa kiasi kidogo ikiwa hutarekebisha bei zako. Kwa mfano, ukiweka bei yako kuwa USD 100, utajipatia USD 84.50 baada ya ada ya asilimia 15.5 kuondolewa na wageni wako watalipa USD 100.

Ukirekebisha bei zako, fanya mabadiliko tarehe 27 Oktoba ukitumia programu yako ya usimamizi wa nyumba. Kisha hakikisha kwamba bei zako, ikiwemo mapunguzo na promosheni, zinaonekana sawa kwenye programu na tovuti unazotumia.

Ukiamua kufanya mabadiliko kabla ya tarehe 27 Oktoba, utahitaji kusasisha mwenyewe muundo wako wa ada kuwa ada moja ya huduma katika sehemu ya Malipo kwenye akaunti yako ya Airbnb.

Kile ambacho ada za huduma za Airbnb zinashughulikia

Ada za huduma husaidia kulipia gharama za bidhaa na huduma za Airbnb, ikiwemo uchakataji wa malipo, uuzaji na huduma kwa wateja. Kusasisha muundo wetu wa ada kuwa ada moja ni sehemu ya ahadi ya Airbnb ya kuboresha uwazi wa bei.

Pata maelezo zaidi kuhusu ada za huduma za Airbnb.

*Baadhi hulipa zaidi, ikiwemo baadhi ya wenyeji wenye matangazo nchini Italia na Brazili.

Ada za huduma ni asilimia ya bei yako ya kila usiku pamoja na ada zozote ulizoweka, kama vile ada ya usafi. 

Katika baadhi ya nchi na maeneo, kodi hujumuishwa kwenye jumla ya bei iliyoonyeshwa. Jumla ya bei ikiwemo kodi huonyeshwa siku zote kabla ya kulipa.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
22 Ago 2025
Ilikuwa na manufaa?