Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Tunakuletea kichupo cha Leo, kituo chako cha kukaribisha wageni

Utapata nyenzo na kazi muhimu mara tu unapofungua Airbnb.
Na Airbnb tarehe 17 Mei 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 1 Jun 2022

Vidokezi

  • Kichupo cha Leo kinakusaidia kusimamia utaratibu wako wa kila siku wa kukaribisha wageni

  • Inakupa ufikiaji wa haraka wa majukumu na taarifa muhimu kutoka kwenye kifaa chochote

Kadiri unavyozidi kuwekewa nafasi, ndivyo majukumu yako ya kukaribisha wageni yanavyoweza kuongezeka. Kichupo cha Leo—skrini ya kwanza inayoonekana unapobadilisha kwenda kukaribisha wageni kwenye programu au tovuti ya Airbnb—kimeundwa ili kukusaidia kuokoa muda kwenye majukumu ya kila siku.

Kutoka kwenye kichupo cha Leo, unaweza kusimamia maombi ya kuweka nafasi au nafasi zilizowekwa na kupata kwa urahisi nyenzo zaidi za kufanikisha mambo. Unaweza pia kupata nyenzo nyinginezo, ikiwemo habari za hivi karibuni na vidokezi kutoka kwa Airbnb.

Nyenzo muhimu

Iwe unafikia unatumia cha Leo kutoka kwenye simu ya mkononi au kompyuta, skrini hii inawasilisha taarifa hiyo hiyo muhimu unayohitaji ili uendelee kumakinikia utaratibu wako wa kukaribisha wageni. Hapa utapata:

  • Arifa zinazozingatia muda, kama vile maombi amilifu ya kuweka nafasi au hatua unazopaswa kutekeleza

  • Nafasi za wageni zilizowekwa, za sasa na zinazokaribia

  • Hatua zinazofuata, ikiwa ni pamoja na hatua mahususi unazoweza kuchukua ili kusaidia kuongeza mvuto wa tangazo lako na kunufaika na mielekeo ya kuweka nafasi

  • Vidokezi na habari za hivi karibuni kuhusu
  • kukaribisha wageni kutoka Airbnb zinazohusiana na vipengele na nyenzo mpya, matukio maalumu na mabadiliko kwenye sera ambayo yanaweza kukuathiri

Vipengele vinavyofaa simu ya mkononi

Kuwajibu wageni haraka ni muhimu katika mafanikio ya huduma ya kukaribisha wageni, hiyo ndiyo sababu Wenyeji wengi wanajibu kwa urahisi kwa kutumia simu zao mahiri. Kwenye matoleo yote ya programu ya simu ya mkononi, kichupo cha Leo kinakuelekeza kwenye taarifa muhimu kwa mbofyo mmoja tu.

Kwenye sehemu ya chini ya skrini yako, utapata vitufe vya:

  • Kichupo cha Leo, ambacho kinakurudisha haraka kwenye sehemu ya juu ya skrini

  • Kikasha, ambapo unaweza kusoma, kutuma na kuratibu ujumbe, au kuwasiliana nasi kwa ajili ya usaidizi

  • Kalenda, ambapo unaweza kusasisha mipangilio yako ya bei na upatikanaji hasa unapowasha kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Vidokezi, ambavyo vinajumuisha data kuhusu utendaji wako, mielekeo ya kuweka nafasi na fursa za kujipatia mapato zaidi

  • Menyu, ambapo unaweza kwenda moja kwa moja kwenye tangazo lako na kupata viungo vya nyenzo za kukaribisha wageni, jukwaa letu la jumuiya na kadhalika

Vipengele vinavyofaa kompyuta ya mezani

Kichupo cha Leo ni kile kile kwenye tovuti na kwenye programu, isipokuwa kwa Wenyeji walio na tangazo zaidi ya moja. Ikiwa una matangazo mengi, unaweza kufikia nyenzo zetu za ukaribishaji wageni wa kiweledi kupitia kitufe cha Menyu kwenye tovuti pekee. Vipengele hivi vinajumuisha historia yako ya miamala na takwimu kama vile mapato.

Hata ratiba yako iwe na shughuli nyingi kiasi gani, unaweza kutegemea kichupo cha Leo ili kukusaidia kuzingatia kile ambacho ni muhimu zaidi katika utaratibu wako wa kukaribisha wageni.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Kichupo cha Leo kinakusaidia kusimamia utaratibu wako wa kila siku wa kukaribisha wageni

  • Inakupa ufikiaji wa haraka wa majukumu na taarifa muhimu kutoka kwenye kifaa chochote

Airbnb
17 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?