Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Jinsi ya kumaliza kutangaza sehemu yako

Unaweza kumaliza tangazo uliloshughulikia hapo awali au kuanza jingine jipya.
Na Airbnb tarehe 14 Okt 2021
Imesasishwa tarehe 14 Okt 2021

Karibu tena! Katika hatua hii unaweza kuchagua kati ya kumaliza tangazo uliloanza tayari, kuunda tangazo jipya na kurudufisha sehemu fulani za tangazo lililopo.

1. Maliza tangazo lako
Matangazo yoyote ambayo tayari umeanza yameorodheshwa hapa—utapata yale uliyoshughulikia mwanzoni yametangulizwa. Ikiwa una zaidi ya matangazo matatu yanayoendelea, bofya Onyesha yote ili kupanua orodha. Mara baada ya kuchagua tangazo unalotaka kushughulikia, utaanzia mahali ulipoachia na unaweza kurudi wakati wowote ili kutathmini na kuhariri maelezo yoyote uliyoweka.

2. Unda tangazo jipya
Ili kuanza tangazo jipya, bofya tu + na tutakuongoza kwenye kila hatua.

3. Rudufisha tangazo lililopo
Unaweza kuokoa wakati wa kuunda tangazo jipya kwa kutumia maelezo kutoka kwenye tangazo lililopo. Hii inafaa zaidi kwa Wenyeji ambao wanatangaza sehemu zinazofanana, kama vile vyumba kadhaa vya kujitegemea katika nyumba moja. Utakuwa na chaguo la kutumia picha zilezile au kuweka nyingine mpya.

Kuanzia mwanzo hadi mwisho, unaweza kutangaza sehemu yako katika hatua 10 kuu:

  1. Chagua aina ya sehemu unayopangia kukaribisha wageni
  2. Elezea zaidi kuhusu aina ya nyumba yako
  3. Fafanua iwapo wageni watakaa kwenye eneo hilo peke yao
  4. Weka mahali ulipo
  5. Tambulisha idadi ya wageni ambao ungependa kuwakaribisha
  6. Tangaza vistawishi vya sehemu yako
  7. Weka na upange picha zako
  8. Lipe eneo lako jina
  9. Elezea eneo lako
  10. Weka bei yako ya kila usiku

Unaweza kufanya mabadiliko kwenye tangazo lako wakati wowote baada ya kulichapisha. Utaweza pia kuboresha jinsi unavyotaka kukaribisha wageni—kila kitu kuanzia kusasisha kalenda yako na kutathmini sera yako ya kughairi hadi kuweka sheria za nyumba yako.

Airbnb
14 Okt 2021
Ilikuwa na manufaa?