Jinsi ya kuweka eneo lako

Kutoa anwani sahihi ni muhimu katika kuwavutia wageni.
Na Airbnb tarehe 5 Mei 2021
Inachukua dakika 1 kusoma
Imesasishwa tarehe 16 Nov 2022

Mahali pa eneo lako panaweza kuchangia pakubwa katika uamuzi wa wageni wa kukaa hapo. Kabla ya kuweka nafasi, wanaweza kuangalia jinsi ilivyo karibu na maeneo wanayopanga kutembelea wakati wa safari yao.

Kama Mwenyeji, unaweza kuchagua iwapo ungependa kutoa eneo la jumla au mahususi kwa ajili ya ramani iliyoonyeshwa katika matokeo ya utafutaji. Kwa vyovyote vile, wageni hawapokei anwani yako ya mtaa hadi nafasi waliyoweka ithibitishwe.

Jinsi ya kuweka eneo lako

1. Weka anwani yako ya mtaa. Anza kuandika na wakati anwani sahihi itajitokeza, ichague.

2. Thibitisha anwani yako. Fanya marekebisho yoyote yanayohitajika kwa usahihi, kama vile kuweka fleti au nambari ya chumba.

3. Hakikisha kwamba pini ipo mahali sahihi. Ikiwa pini haijawekwa ifaavyo, buruta ramani hadi pini ielekee mahali sahihi.

4. Chagua ramani. Tangazo lako litajumuisha ramani ya eneo la jumla la mahali pako isipokuwa utumie swichi ya kutogoa ili kuonyesha eneo lako mahususi.

  • Eneo la jumla: Ramani ya tangazo lako inaonyesha eneo linalolizunguka, ndani ya nusu maili (chini ya kilomita 1) ya anwani ya mtaa.
  • Eneo mahususi: Ramani ya tangazo lako inaonyesha pini kwenye njia panda iliyo karibu, lakini haionyeshi eneo hususa.
Hivi ndivyo eneo la jumla (kushoto) na mahususi (kulia) yanavyoainishwa katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb.
Na ikiwa una swali au ukipata matatizo yoyote, unaweza kuwasiliana nasi ili upate msaada.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
5 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?