Dashibodi ya mapato: Mwonekano mzuri wa takwimu zako za msingi

Tumia chati mpya tendanishi za utendaji na ripoti za mapato za kiotomatiki.
Na Airbnb tarehe 1 Mei 2024
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 1 Mei 2024

Kuelewa mapato yako kunaweza kukusaidia uendeshe biashara ya kukaribisha wageni yenye mafanikio zaidi. Ndiyo sababu tunaongeza vipengele vipya kwenye dashibodi ya mapato, tukichochewa na maoni ya Wenyeji.

  • Chati tendanishi kwa vidokezi vya kina. Angalia mapato yako kupitia mtazamo wa kila mwezi na kila mwaka, pamoja na kuchuja kulingana na tangazo na upate maelezo zaidi kuhusu miaka iliyopita na makadirio ya siku zijazo.
  • Ripoti za mapato katika kituo kipya muhimu. Pokea kiotomatiki ripoti za kila mwezi na za kila mwaka na uzipakue kama PDF. Ripoti hizo zinajumuisha mchanganuo kulingana na tangazo na njia ya kupokea malipo.

Fikia dashibodi ya mapato katika kichupo cha Menyu. Chagua Mapato ili kuifungua.

Haya ndiyo mambo yote utakayopata kwenye dashibodi ya mapato iliyoboreshwa.

Chati mpya tendanishi za mapato

Chati ya mapato iliyo kwenye sehemu ya juu ya dashibodi inaonyesha:

  • Kiasi ulichopata katika kila mwezi mmoja katika miezi sita iliyopita
  • Kiasi ambacho umepata kufikia sasa mwezi huu
  • Kiasi unachokadiriwa kupata katika kila mmoja wa miezi mitano ijayo kulingana na nafasi zilizowekwa zinazokaribia

Bofya kishale marudufu ili kupanua na kuingiliana na chati ya mapato. Mwonekano huu mpya unaonyesha mapato yako kulingana na mwezi au mwaka na kulingana na tangazo. Tumia kichujio ili kuchagua tangazo au matangazo ya kuonyesha.

Chini ya chati tendanishi ya mapato, takwimu za utendaji zitaonyeshwa:

  • Idadi ya nafasi zilizowekwa
  • Jumla ya usiku ambao uliwekewa nafasi
  • Kiwango cha ukaaji
  • Wastani wa urefu wa ukaaji

Takwimu hizi huhesabiwa kulingana na muda na matangazo unayotazama. Hujisasisha kiotomatiki wakati wowote unapoweka kichujio au kupakia upya dashibodi.

Ili kupata mchanganuo wa mapato yako tangu Januari 1 ya mwaka wa sasa, gusa Angalia muhtasari wa mapato karibu na chati. Unaonyesha mapato yako ghafi, jumla ya kiasi unachopata kabla ya makato yoyote. Kila makato yameorodheshwa kwenye mstari wake, ikifuatiwa na jumla ya malipo yako halisi.

Hivi ndivyo utakavyoona:

  • Mapato ghafi
  • Marekebisho
  • Ada ya huduma ya Mwenyeji
  • Kodi zilizozuiwa
  • Jumla ya malipo halisi

Miamala

Dashibodi inaangazia miamala yako inayokaribia na ya hivi karibuni. Fungua muamala wowote ili upate maelezo, ikiwemo:

  • Mchanganuo wa bei
  • Tarehe ilipolipwa au imeratibiwa kulipwa
  • Chaguo la kulipwa ndani ya dakika 30 kupitia huduma ya Malipo ya Haraka (nchini Marekani pekee)
  • Msimbo wa uwekaji nafasi uliounganishwa
  • Jina na picha ya mgeni

Fungua miamala yote inayokaribia au iliyolipwa kwa ajili ya mwonekano kamili. Kutoka hapo, unaweza:

  • Chuja miamala kulingana na tarehe, tangazo na njia ya kupokea malipo
  • Tafuta kiasi halisi cha malipo au msimbo wa uthibitishaji wa nafasi iliyowekwa
  • Unda ripoti mahususi katika mfumo wa mafaili ya CSV kwa kuchagua maelezo ambayo ungependa kujumuisha, kama vile njia ya kupokea malipo, tarehe ya kuweka nafasi na msimbo wa kuthibitisha nafasi iliyowekwa

Kituo kipya cha kuripoti mapato

Airbnb sasa inakutolea taarifa za kila mwezi na za kila mwaka kiotomatiki katika kituo kipya cha kuripoti. Unaweza kupata ripoti tangu mwaka ulipoanza kukaribisha wageni na kuzipakua au uzitume kwa barua pepe kama PDF.

Kila ripoti inaangazia maelezo ya mapato ya mwezi au mwaka huo, ikiwa ni pamoja na:

  • Mchanganuo wa mapato ghafi, marekebisho, ada ya huduma ya Mwenyeji, kodi zozote zilizozuiwa na jumla ya malipo halisi
  • Takwimu za utendaji, kama vile usiku uliowekewa nafasi na wastani wa muda wa kukaa
  • Mapato kulingana na tangazo na njia ya kupokea malipo
  • Mapato kwa kila mwezi wa mwaka uliochaguliwa (kwa ripoti za mwaka tu)

Mipangilio na hati

Bofya ikoni ya gia iliyo upande wa juu kulia mwa dashibodi ya mapato ili ufikie:

  • Mipangilio ya kupokea malipo, ambapo unaweza kutathmini au kuweka njia za kupokea malipo na kanuni za anwani ya kutuma malipo
  • Taarifa ya kodi, ambapo unaweza kudhibiti maelezo ya mlipa kodi na hati za kodi
  • Ripoti za mapato, ambayo ni njia nyingine ya kufikia taarifa katika kituo chako kipya cha kuripoti

Jaribu dashibodi ya mapato iliyoboreshwa leo unapojisajili kwenye Mpango wa Ufikiaji wa Mapema.

Huduma anayopata mtumiaji inaweza kutofautiana kulingana na mahali.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
1 Mei 2024
Ilikuwa na manufaa?