Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Kuandika maelezo ya tangazo yenye ufanisi

Wasaidie wageni wajione wapo katika sehemu yako.
Na Airbnb tarehe 18 Nov 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 28 Nov 2023

Kuandika maelezo ya kina kuhusu eneo lako ni mojawapo ya njia bora za kuweka matarajio na kuvutia uwekaji nafasi. Wajulishe wageni kile watakachopata watakapowasili.

Andika maelezo yako ya tangazo

Kuna zaidi ya nyumba milioni 7 kwenye Airbnb. Tumia sehemu ya Maelezo ya nyumba kuelezea mambo ya kipekee kuhusu nyumba yako.

  • Weka maelezo mafupi. Wageni mara nyingi wanasoma maelezo ya tangazo ili kuona vipengele muhimu. Ongoza kwa kutumia kile kilicho muhimu zaidi, na epuka kurudia taarifa zinazoonekana katika maeneo mengine ya tangazo lako, kama vile orodha yako kamili ya vistawishi.
  • Simulia kuhusu sehemu yako. Kuwa mahususi kuhusu huduma unayowapa wageni. Chumba cha kawaida katika sehemu ya biashara ya jiji kinaweza kuwa “sehemu inayofaa kwa ajili ya kuvinjari jiji.” Fleti ya ghorofa ya juu iliyozungukwa na miti inaweza "kuonekana kama uko kwenye nyumba ya kwenye mti."

  • Zingatia vipengele maalumu. Eleza kile ambacho kinatofautisha sehemu yako, kikiangazia vistawishi vikuu ambavyo wageni wanataka. Soma maelezo mengine ya tangazo na tathmini ili upate hamasa na upate maelezo kuhusu aina za taarifa ambazo wageni wanathamini.

  • Kuwa na uhalisia. Kusifia au kutia chumvi kunaweza kusababisha maudhi na tathmini mbaya. Kuwa mwangalifu kuhusu vipengele vya nyumba yako ambavyo vinaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya wageni, ikiwemo watu walio na matatizo ya kutembea au watoto.

Jaza sehemu nyingine zote

Tumia sehemu zilizobaki ili kuwasaidia wageni kuelewa jinsi ilivyo kukaa kwenye sehemu yako.

  • Nyumba yako. Andika maelezo ya jumla ya vyumba na sehemu zako, ukiweka mkazo kwenye maelezo ya kufurahisha lakini ya kweli ambayo wageni wanaweza kutaka kujua. Kwa mfano, "Ua wa nyuma umejengewa uzio, na kuna nafasi ya watoto na wanyama vipenzi kukimbiakimbia."
  • Ufikiaji wa wageni. Wajulishe wageni ni maeneo gani ya sehemu hiyo wanayoweza kutumia. Kwa mfano, "Wageni wanaweza kutumia baraza linaloshirikiwa na nyumba kuu."
  • Mwingiliano na wageni. Chagua mapendeleo yako ya mwingiliano wa ana kwa ana ili kuweka matarajio. Machaguo ni kuanzia kutumia muda na wageni hadi kuwasiliana kupitia programu.
  • Maelezo mengine ya kuzingatia. Jumuisha kitu kingine chochote ambacho ungependa wageni wajue ambacho hakijatangazwa mahali pengine. Kwa mfano, "Nyumba hiyo iko umbali wa kutembea kwa dakika 10 kutoka katikati ya jiji."

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
18 Nov 2020
Ilikuwa na manufaa?