Airbnb na Wenyeji wakazi wanachangia jumuiya huko Paris
Kutenga muda wa kuungana na watu ni muhimu kwa Emmanuel, Mwenyeji huko Paris kwa zaidi ya miaka 10. "Ninapenda kushirikiana na watu, hasa wale walio katika dhiki au walio wapweke," anasema. "Tunahitaji kutenga muda ili kuwafanya watu wajisikie wenye furaha. Ni sawa na kukaribisha wageni kwenye Airbnb unapomkaribisha mtu nyumbani kwako.”
Hiyo ndiyo sababu mojawapo kati ya nyingi ya Emmanuel kujitolea katika Shirika la Saint Vincent de Paul, shirika la miaka 190 lililoanzishwa huko Paris ambalo linawahudumia watu wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na watu wasio na makazi. Linaratibu mikusanyiko ya kila wiki ili kukutanisha watu pamoja , kama vile karakana za kushona na vifungua kinywa vya sehemu ya nje.
Kama mwanachama wa Klabu cha Wenyeji wa Paris, Emmanuel aliteua shirika la Saint Vincent de Paul kwa ajili ya mchango wa Mfuko wa Jumuiya ya Airbnb. Wanachama wa Kalabu cha Wenyeji wana fursa kila mwaka kusaidia jumuiya zao za mahali husika kupitia Mfuko wa Jamii. Aliamini shirika hilo lisilotengeneza faida lilikuwa mtaradhia sahihi kwa sababu lilikuwa na maadili sawa na Airbnb. "Airbnb ni jumuiya maalumu kwa sababu inathamini undugu kati ya watu," anasema.
Jinsi Vilabu vya Wenyeji vinavyoleta mabadiliko
Kwa sababu ya uteuzi wa Kilabu cha Wenyeji cha Paris, Shirika la Saint Vincent de Paul lilipokea mchango wa USD 50,000 kutoka kwenye Mfuko wa Jumuiya ya Airbnb. Mchango huu utafadhili maendeleo ya makazi ya wanawake pekee katika jiji hilo na mikusanyiko ya ziada ya jumuiya, kama vile viamsha kinya katika sehemu za nje.
Zaidi ya Vilabu 50 vya Wenyeji viliteua mashirika yasiyotengeneza faida kote ulimwenguni ili kupokea michango ya Mfuko wa Jumuiya ya Airbnb mwaka 2023. Uteuzi kwa ajili ya kupokea michango ya Mfuko wa Jumuiya mwaka 2024 sasa umefunguliwa. Ungana na Kilabu cha Wenyeji cha mahali ulipo ili kupata maelezo zaidi.
Information contained in this article may have changed since publication.

