Weka maelezo ambayo wageni watayapenda

Mkurugenzi wa zamani wa ubunifu anashiriki vidokezi vyake bora vya kupamba.
Na Airbnb tarehe 13 Apr 2021
Inachukua dakika 6 kusoma
Imesasishwa tarehe 18 Apr 2022

Vidokezi

  • Kuunda tukio la kukumbukwa kwa ajili ya wageni wako huanza kwa kubuni kwa uangalifu sehemu yako

  • Vidokezi vya kitaalamu vinajumuisha kuweka mwonekano wa sehemu yako, kuunda kona nzuri na kufanya ubunifu wako uwe mahususi

  • Zawadi na vistawishi vidogo vya eneo husika vinaweza kusaidia kuboresha ukaaji wa wageni

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

Wageni wanapoingia kwenye The Beach Lodge huko Hollywood Beach, California, mara moja wanamfahamu Tiffany Caliva-Talledo. Umakinifu wake na mapenzi yake ya ubunifu huhisiwa kwenye machaguo yake yote ya mapambo, rangi, maumbile na kila pambo mahususi. Kama mkurugenzi wa zamani wa ubunifu, daima amekuwa akizingatia mambo ya kina. Hapa, anashiriki siri zake za mafanikio kwenye Airbnb.

The Beach Lodge inazinduliwa

"Kabla ya kukarabati The Beach Lodge, ilikuwa nyumba yenye sura mbaya ya kijani kibichi. Watu waliiita ‘Maficho ya Mihadarati' na walikuwa wakikimbia walipopitia hapo! Majirani walidhani tuna wazimu kwa kuinunua, lakini niliona jambo la kipekee kuihusu—nilifikiria kwamba tukiweza kuikarabati, watu wangekuja. Nimeionyesha upendo mwingi sana—nami nadhani wageni watarudi kwa sababu hiyo hiyo."

Vidokezi 7 vya Tiffany vya kufanya zaidi ya ulivyotarajiwa

Tengeneza mandhari
"Kuunda matukio yasiyosahaulika kila wakati huanza kwa kuweka mtazamo unaofaa. Mimi huwaambia wateja wangu kwamba, wakati wanabuni sehemu, waanze na hisia badala ya mandhari. Unataka wageni wako wahisi nini wanapoingia kwenye nyumba yako—starehe, furaha, utulivu? Kwa ajili ya The Beach Lodge, badala ya kufuata mandhari halisi ya ufukweni, nilifikiria kwa jumla kuhusu rangi, maumbile na vipengele: vielelezo vinavyoingiliana na hali ya hewa, maumbile yanayoshabihi mchanga na mimea mingi ya kuonyesha hisia ya mandhari ya nje."

Ubunifu ukiwa na uhaba wa pesa
"Si lazima mapambo yawe ya bei ghali! Masoko ya mitumba na maduka ya mitumba yamejaa vitu vyenye thamani vya bei nafuu na bidhaa za kipekee ambazo zina historia ndefu. Unahitaji tu kuwa na bidii ya kutafuta. Ninavutiwa hasa na vitu vinavyowakilisha utamaduni wangu wa Ufilipino na Asia. Vitu unavyochagua kwa ajili ya sehemu yako vinapaswa kuwa na historia fulani na kwa pamoja vitasaidia kusimulia hadithi kubwa ya nyumba yako.”

Kuwa mdadisi
"Ushauri mwingine ninaoshiriki na wateja wangu ni kujipa ruhusa ya kuwa mdadisi. Badilisha mapambo. Jaribu mambo mapya. Fanya mambo upya kila msimu. Ni njia bora ya kugundua kile kinachofaa kwa kile unachojaribu kufikia na kile ambacho hakifai. Fikiria kuhusu sehemu yako kama mtu mwenye changamoto na tabia zake mwenyewe. Kama wewe, inapaswa kukukua, kubadilika na kuboreka ili ifae zaidi kwa ajili ya muda wa sasa."

Tengeneza maeneo ya likizo ndogo
"Ninapenda kucheza na sehemu na mandhari kwa njia zisizotarajiwa. Kidokezi kimoja ninachopendekeza ni kutengeneza maeneo ya likizo ndogo kwenye nyumba yako, maeneo madogo ya likizo fupi ambapo wageni wanaweza kujizamisha kwenye kitabu. Ninaweza kuweka mablanketi, mito na mchoro kwenye kona ili ziweze kuwavutia kabisa watu. Fikiria jinsi unavyoweza kutengeneza kona hizi ndogo zenye kuvutia kila mahali."

Fikiria kuhusu sehemu yako kama mtu mwenye changamoto na tabia zake mwenyewe.
Tiffany,
Hollywood Beach, California

Ifanye iwe mahususi
"Ikiwezekana, saidia kufanya ukaaji wa wageni wako uwe mahususi kwa kuwapa vitu maalumu vya ziada. Kwa mfano, mtu akisema kwamba anasherehekea siku ya kuzaliwa, mimi humwekea keki ndogo kutoka kwenye maduka niyapendayo ya kuoka mikate katika eneo langu. Ikiwa ni wala mboga, mimi hutengeneza orodha ya migahawa ya eneo langu. Ikiwa ni familia yenye watoto, mimi hubadilisha mito na mashuka ili kuweka yale yanayodumu zaidi. Mazingatio haya ya umakinifu huwavutia sana wageni. Utaona mambo hayo yakionyeshwa katika tathmini zako na nafasi zinazowekwa zinazorudiwa."

Wapatie zawadi
"Ninapendekeza uwape wageni kitu cha kumbukumbu au cha kubeba wanapowasili kama ishara ndogo inayowaonyesha kwamba wao ni wa pekee na wamekaribishwa, kama vile kadi za zawadi kwa biashara zilizo karibu au kadi za posta kutoka kwa wasanii wa eneo husika."

"Ili kupanua wazo hilo hata zaidi, wageni wanaweza kununua vitu kutoka The Beach Lodge moja kwa moja, ikiwemo majoho na mashuka yanayozingatia mazingira pamoja na vitu vya kale au kutoka kwenye duka la mtandaoni nililotengeneza. Nimekuwa pia nikionyesha bidhaa zinazomilikiwa na wanawake na za wenyeji, ambazo ni muhimu kwangu. Sichukui faida zozote. Ninafanya yote haya ili kuwaunganisha watu na bidhaa hizi. Ina maana kubwa kwangu kuliko tu kuwa likizo.”

Vaa kofia yako ya mkurugenzi wa meli ya abiria
"Tuliita nyumba yetu The Beach Lodge kwa sababu, kwa maoni yetu, nyumba ya kukutania ni sehemu maridadi ya watu kukutania. Ninaijaza michezo ya bao, mikeka ya yoga, kazi za ufundi, sanaa, jiko la kuchomea nyama, taulo za ufukweni, baiskeli, vitabu vya kujizamisha wakati wa kusoma na santuri. Usafiri unahusu kupanua upeo wako na shughuli hizi zinaweza kuwasaidia watu kuunda kumbukumbu na njia mpya katika maisha yao. Fikiria vistawishi vinavyoweza kusaidia kuboresha uzoefu wake wa jumla."

Kumbuka kwamba yote ni kuhusu vipengele, vipengele, vipengele! Kupitia mapambo haya ya umakinifu, wageni watahisi kikweli umakinifu ulioweka kwenye sehemu yako nao wataendelea kurudi.

Vidokezi

  • Kuunda tukio la kukumbukwa kwa ajili ya wageni wako huanza kwa kubuni kwa uangalifu sehemu yako

  • Vidokezi vya kitaalamu vinajumuisha kuweka mwonekano wa sehemu yako, kuunda kona nzuri na kufanya ubunifu wako uwe mahususi

  • Zawadi na vistawishi vidogo vya eneo husika vinaweza kusaidia kuboresha ukaaji wa wageni

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni
Airbnb
13 Apr 2021
Ilikuwa na manufaa?