Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Mchakato wa kutoka ambao ni wazi na rahisi

  Elezea matarajio yako, kuanzia kufanya usafi hadi kufunga.
  Na Airbnb tarehe 9 Mac 2020
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 1 Jul 2021

  Vidokezi

  • Taja wazi kuhusu wakati wa kutoka na usisitize umuhimu wa kutoka kwa wakati

  • Toa maelekezo yoyote ya kufunga, pamoja na mahali pa kuacha ufunguo

  • Waambie wageni ni kiasi gani cha kusafisha, kuanzia kuosha vyombo hadi kutoa shuka kutoka kitandani

  • Tuma ukumbusho wa wakati wa malipo na maelekezo yoyote siku moja kabla

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuwafurahisha wageni wako wa kwanza

  Kwa baadhi ya wenyeji, kutoka kunamaanisha kuwaomba wageni kufunga mlango na kufurahia safari yao ya kurudi nyumbani. Wenyeji wengine huacha maelekezo ya kina ya kufanya usafi. Bila kujali mtindo wako wa kukaribisha wageni, kuhakikisha matarajio yako kwa ajili ya kutoka kwa wageni yanawasilishwa wazi ni muhimu kwao ili kumaliza ukaaji wao kwa njia nzuri.

  Hivi ni vidokezi vya mchakato wa kutoka bila mafadhaiko:

  Kuwa wazi kabisa kuhusu wakati wa kutoka

  Kuchelewa kutoka kunaharibu ratiba yako na kunaweza kuingiliana na nafasi uliyowekewa inayofuata, hasa ikiwa una nafasi zilizowekwa zinazofuatana. Hakikisha wageni wanajua ni wakati gani wanahitaji kutoka na usisitize umuhimu kwa kuelezea sababu yake.

  Kidokezi cha Mwenyeji: Joh kutoka San Francisco anatumia mbinu mahiri: "Ninawaambia wageni kwamba msafishaji atafika saa 5:00 asubuhi ili kuandaa fleti kwa ajili ya wageni watakaofuata, kwa hivyo wanaelewa kwa nini ni muhimu kuondoka kwa wakati."

   Shiriki maelekezo yoyote ya usafi

   Wenyeji wana matarajio tofauti sana kuhusu kufanya usafi—baadhi yao wanataka wageni waoshe vyombo vyao na kujifulia nguo, ilhali wengine wanapendelea kufanya usafi wao wenyewe au kumkabidhi msafishaji wao (na wanaweza kutumia ada ya usafi* ili kulipia huduma hii). Bila kujali mbinu yako, elezea waziwazi. Na ufikirie kujumuisha taarifa hii kwenye mwongozo wako wa nyumba. Wenyeji wengi pia huacha vifaa vya kufanyia usafi ili iwe rahisi kwa wageni kudumisha usafi wakati wote wa ukaaji wao.

   Ubunifu wa mwenyeji: Chelsea na Kevin kutoka Chicago waligundua njia ya ubunifu ya kushiriki mahitaji yao ya usafi. "Kwa msaada wa mbwa wetu mzuri, nimeunda mwongozo wenye picha wa kutoka kwa ajili ya wageni wetu. Hadi sasa umependwa na wengi! Ya kijinga, ya kucheza, ya kufurahisha na zaidi ya yote, ni ngumu kupuuza!"

   Waambie wageni jinsi ya kufunga

   Wageni wanaweza kuchanganyikiwa kuhusu jinsi ya kufunga sehemu yako. Acha maelekezo ya wazi wazi kwa ajili yao. Je, madirisha yanahitaji kufungwa? Milango fulani inahitaji kufungwa? Je, vipi kuhusu kuzima thermostati au viyoyozi? Na ikiwa kuna ufunguo, wageni watahitaji kujua wapi wauache. Kwa mara nyingine tena, mwongozo wako wa nyumba ni eneo zuri la kutoa maelezo haya.

   Tuma kumbusho

   Hata kama umetoa maelekezo ya kutoka kwenye tangazo lako na/au katika mwongozo wako wa nyumba, ni wazo zuri kuelezea mambo wanayopaswa kufanya siku moja kabla. Huenda wageni wamekuwa wakifurahia ukaaji wao na labda hawakufikiria kuangalia maelezo ya kutoka hadi asubuhi ya kuondoka kwao. Kwa kuelezea matarajio yako siku moja kabla—iwe ni ana kwa ana au kwa arafa, barua pepe au ujumbe wa Airbnb—wageni wana uwezekano mkubwa wa kufuata maelekezo yako na kuondoka kwa wakati.

   Ninawaambia wageni kwamba msafishaji atafika saa 5:00 asubuhi, kwa hivyo wanaelewa kwa nini ni muhimu kuondoka kwa wakati.
   Joh,
   San Francisco

   Ukiweza, fanya mengi zaidi

   Siku za kusafiri zinaweza kuwafadhaisha wageni. Fikiria njia ambazo unaweza kusaidia kupunguza wasiwasi wowote. Baadhi ya wenyeji hujitolea kusaidia katika mipango ya uwanja wa ndege. Wengine hutoa sehemu kwa ajili ya wageni kuacha mifuko yao kwa saa chache wakati wanatalii jiji. Matendo haya hakika si ya kawaida na hakuna mgeni atakayeyatarajia. Lakini ikiwa unaweza kufanya zaidi ya unavyotarajiwa, ni njia nyingine zaidi ambayo unaweza kuwafurahisha wageni wako.

   Mchakato wao wa kutoka ukiwa shwari, wageni watakumbuka raha zote walizokuwa nazo kwenye sehemu yako badala ya mafadhaiko ya kuifunga na utakuwa tayari kwa nafasi ijayo uliyowekewa!

   *Ukiondoa Wenyeji wanaotoa huduma ya malazi huko China Bara. Pata maelezo zaidi

   Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

   Vidokezi

   • Taja wazi kuhusu wakati wa kutoka na usisitize umuhimu wa kutoka kwa wakati

   • Toa maelekezo yoyote ya kufunga, pamoja na mahali pa kuacha ufunguo

   • Waambie wageni ni kiasi gani cha kusafisha, kuanzia kuosha vyombo hadi kutoa shuka kutoka kitandani

   • Tuma ukumbusho wa wakati wa malipo na maelekezo yoyote siku moja kabla

   • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuwafurahisha wageni wako wa kwanza
   Airbnb
   9 Mac 2020
   Ilikuwa na manufaa?