Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Kuweka mkakati wako wa kupanga bei

Rekebisha bei zako mara kwa mara na uzingatie uhitaji wa wageni na msimu.
Na Airbnb tarehe 4 Des 2025

Programu ya Airbnb hufanya iwe rahisi kusimamia bei na upatikanaji wako. Hivi ndivyo unavyoweza kutumia zana zako za kukaribisha wageni ili kukusaidia uwekewe nafasi zaidi na kusaidia malengo yako ya mapato.

Tathmini kalenda yako mara kwa mara

Wageni hutafuta Matukio ya Airbnb ambayo hutoa thamani kubwa. Fanya mazoea ya kutathmini upya kile unachotoza na ni mara ngapi unakaribisha wageni ili uendelee kuwa na ushindani. 

Unaweza kurekebisha mipangilio yako ya bei na upatikanaji moja kwa moja kwenye kalenda yako. Zingatia mambo haya.

  • Siku ya wiki: Fikiria kuweka bei tofauti kwa siku tofauti. Kwa mfano, unaweza kutaka kutoza kiasi kidogo kwa siku zenye shughuli chache ili kuwashawishi watu kuweka nafasi.
  • Wakati wa siku: Fikiria kuhusu nyakati bora za kuvutia wageni mbalimbali na kuweka upatikanaji. Kwa mfano, jioni za siku za wiki zinaweza kuwavutia wakazi ambao hufanya kazi wakati wa mchana na wanataka kuepuka wikendi zenye shughuli nyingi.
  • Mapunguzo ya kikundi: Unaweza kutoa bei zilizopunguzwa kwa kila mtu ili kuvutia vikundi vikubwa. Kwa mfano, unaweza kutoa punguzo la asilimia 10 kwa watu 2 hadi 3, punguzo la asilimia 20 kwa watu 4 hadi 5 au asilimia 30 kwa zaidi ya watu 6. 
  • Familia: Fikiria kuruhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 12 kushiriki bila malipo au kwa bei ya chini.
  • Nafasi zilizowekwa katika dakika za mwisho: Ikiwa tukio limewekewa nafasi kwa sehemu tu, jaribu kurekebisha bei yako ili ujaze nafasi zilizobaki. 
  • Ukubwa wa kikundi: Unaweza kurekebisha nafasi zako zilizo wazi ili kuepuka kuuza kupita kiasi ikiwa unatoa tukio lako kwenye tovuti nyingine.

Jitayarishe kwa nyakati zenye shughuli nyingi

Misimu yenye wageni wengi inaweza kusaidia biashara yako kukua. Panga kwa ajili ya uhitaji mkubwa wa wageni kwa kutumia vidokezi hivi vya bei.

  • Weka matukio: Toa tukio lako mara nyingi zaidi wakati hali ya hewa, sikukuu na matukio makubwa kama vile matamasha, sherehe na mashindano ya michezo huleta wageni zaidi katika eneo lako. 
  • Sasisha idadi ya wageni: Fikiria kuongeza idadi ya viti na urekebishe bei ili kusaidia kuwavutia wageni wa dakika za mwisho. Unaweza kufanya mabadiliko haya kwenye kichupo chako cha Leo.

Misimu yenye shughuli nyingi pia ni fursa nzuri ya kusasisha tangazo lako ili lionekane katika utafutaji. Fikiria kurekebisha kichwa na maelezo yako ili kuonyesha wakati wa mwaka au kuweka picha mpya. 

Panga kwa ajili ya nyakati zenye wageni wachache

Hizi ni njia za kusaidia tangazo lako lionekane wakati wa vipindi vyenye utulivu.

  • Weka mapunguzo: Hata mapunguzo madogo yanaweza kuboresha nafasi yako katika utafutaji. Fikiria kutoa bei za chini kwa punguzo kwa watakaowahi na kundi kubwa. Ikiwa punguzo lako ni zaidi ya asilimia 10 kutoka kwenye jumla ya bei, bei yako iliyopunguzwa itaonyeshwa karibu na bei yako ya awali, ambayo imepigwa kistari, katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wa tangazo lako.*
  • Fanya nafasi kwa ajili ya nyongeza za dakika za mwisho: Punguza muda wako wa mwisho kuweka nafasi ili wageni waweze kuweka nafasi siku hiyohiyo au siku moja kabla. Nusu ya nafasi zote zilizowekwa hufanyika chini ya wiki 1 kabla ya tukio kuanza.** Wageni kama vile wakazi na wageni walio na mipango inayoweza kubadilika huwa wanaweka nafasi baadaye kuliko kawaida wakati wa vipindi vyenye shughuli chache.

*Lazima iwe angalau USD 3 au sarafu sawa ya nchi husika kutoka kwenye jumla ya bei

**Kulingana na nafasi zilizowekwa za matukio kuanzia tarehe 13 Mei, 2025, hadi tarehe 20 Julai, 2025, katika miji 30 ulimwenguni kote

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
4 Des 2025
Ilikuwa na manufaa?