Kuwavutia wageni wako wa kwanza
Sasa kwa kuwa Tukio lako la Airbnb limechapishwa, unaweza kuzingatia kuwavutia wageni. Kuweka upatikanaji, kuweka bei yenye ushindani na kupata tathmini zako za kwanza za nyota 5 kunaweza kusaidia kujenga kasi.
Sasisha kalenda yako
Tangazo lako halitaonekana kwenye Airbnb hadi uweke upatikanaji. Sasisha kalenda yako mara moja ili wageni waweze kuweka nafasi. Amua ni mara ngapi utatoa shughuli hiyo kulingana na muda wake, upatikanaji wako na malengo yako ya biashara. Ikiwa una mwenyeji mwenza, amua ni wakati gani kila mmoja wenu ataandaa tukio.
Ili kuweka upatikanaji, chagua siku unayotaka kukaribisha wageni kisha ubofye Ratibu tukio. Chagua wakati, aina ya nafasi iliyowekwa, bei, ukubwa wa kikundi na maelezo mengine. Unaweza kuzuia muda kabla na baada ya shughuli kwa ajili ya kazi ya maandalizi au kufanya usafi.
Jaribu vidokezi hivi ili kusaidia tangazo lako lionekane.
- Fungua upatikanaji zaidi: Kadiri unavyoweka tarehe na nyakati zaidi, ndivyo unavyoweza kuwekewa nafasi zaidi. Wenyeji waliofanikiwa mara nyingi hutoa tukio mara 10 au zaidi kwa mwezi, ikiwemo angalau siku moja ya wikendi kwa wiki.
- Panga mapema: Wenyeji wengi huweka hadi miezi 3 ya upatikanaji ili kusaidia kuongeza uwezekano wao wa kuwekewa nafasi. Unaweza kuratibu tukio unalotoa kila siku hadi siku 60 kabla na tukio unalotoa kila wiki hadi wiki 52 mapema.
- Oanisha kalenda zako: Oanisha kalenda zako za biashara za Airbnb na Google ili kusaidia kufuatilia kila kitu katika sehemu moja na kuzuia kuweka nafasi mara mbili kimakosa. Kwa mfano, usiku unapowekewa nafasi kwenye kalenda moja, unazuiwa kiotomatiki kwenye kalenda nyingine.
- Tafuta fursa: Mara baada ya kuanza kukaribisha wageni, tambua nyakati zenye wageni wachache na zenye shughuli nyingi na uzingatie kurekebisha upatikanaji wako na bei ipasavyo. Kadiri unavyotoa upatikanaji zaidi sasa, ndivyo utakavyoweza kukidhi nyakati zenye uhitaji mkubwa.
Weka bei yenye ushindani
Kurekebisha bei yako kunaweza kukusaidia kuwekewa nafasi zako za kwanza na kujenga kasi. Kuna mambo 4 makuu ya kuzingatia.
- Gharama za uendeshaji: Hakikisha kwamba bei yako inashughulikia gharama zako.
- Mapato: Wakati mwingine kutoa bei ya chini kwa kila mtu kunaweza kuvutia wageni zaidi na kuongeza mapato yako. Kwa mfano:
- Wageni 4 walioweka nafasi kwa USD 75 kila mmoja = USD 300
- Wageni 8 wakiweka nafasi kwa USD60 kila mmoja = USD480
- Matukio yanayofanana: Tafuta shughuli kama zako kwenye Airbnb na tovuti nyinginezo ili kulinganisha bei za eneo husika na uone bei ipi ni ya ushindani. Kiwango cha wastani cha bei ya kimataifa kwa ajili ya Tukio la Airbnb ni USD 65 hadi USD 81.*
- Jumla ya bei: Bei yako lazima ijumuishe ada zote na bakshishi.
Kuweka punguzo ni njia nyingine ya kusaidia tangazo lako lionekane. Kuna mapunguzo 3 yanayopatikana katika mipangilio ya bei yako.
- Kwa muda mfupi: Wavutie wageni wako wa kwanza na tathmini za mapema kwa kutoa punguzo la asilimia 5 hadi asilimia 50 kwa siku 90.
- Watakaowahi: Toa punguzo la asilimia 20 kwa wageni wanaoweka nafasi zaidi ya wiki 2 mapema. Hii inawavutia wasafiri wanaopanga mapema na inakusaidia kujaza kalenda yako.
- Kikundi kikubwa: Unaweza kuweka bei zilizopunguzwa kwa kila mtu ili kuvutia vikundi vikubwa. Kwa mfano, unaweza kutoa punguzo la asilimia 10 kwa watu 2 hadi 3, punguzo la asilimia 20 kwa watu 4 hadi 5 na asilimia 30 kwa zaidi ya watu 6. Wageni wengi huweka nafasi ya tukio wakiwa na angalau mtu mwingine mmoja.*
Ikiwa punguzo lako ni zaidi ya asilimia 10 kutoka kwenye jumla ya bei yako, wageni wanaona bei iliyopunguzwa karibu na bei yako ya awali iliyopigwa kistari katika matokeo ya utafutaji na kwenye tangazo lako.** Ukiweka zaidi ya punguzo moja, mgeni hupata lolote ambalo husababisha uokoaji mkubwa zaidi wa pesa. Hawezi kupokea mapunguzo mengi kwenye nafasi ileile iliyowekwa.
Toa huduma ya kuweka nafasi za binafsi
Unaweza kutaka kutoa tukio lako kwa mgeni au kikundi mahususi kwa bei mahususi. Kwa mfano, kushiriki tukio lako na familia na marafiki kwa bei ya chini au bila malipo ni njia nzuri ya kupata tathmini zako za kwanza za nyota 5.
Ili kuunda tukio la faragha, chagua tarehe na saa kwenye kalenda yako, gusa Hariri kisha uweke mwonekano kuwa wa faragha. Nakili kiungo mahususi na ukishiriki na mgeni au kikundi mahususi. Wageni wanaojiunga na nafasi iliyowekwa pekee ndio wanaoweza kuandika tathmini.
*Kulingana na nafasi zilizowekwa za Matukio ya Airbnb kuanzia tarehe 13 Mei, 2025, hadi tarehe 20 Julai, 2025, katika miji 30 ulimwenguni kote
**Lazima iwe angalau USD 3 au sarafu sawa ya nchi husika kutoka kwenye jumla ya bei
Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
