Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji

Weka urefu wa safari yako, ilani ya mapema, muda wa maandalizi na kipindi cha upatikanaji.
Na Airbnb tarehe 9 Jan 2025
Imesasishwa tarehe 9 Jan 2025
Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji
Kwa kutumia kalenda yako
Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji

Mipangilio ya upatikanaji ya Airbnb inafanya iwe rahisi kudhibiti wakati gani na jinsi gani wageni wanaiwekea nafasi nyumba yako. Utaipata katika kalenda yako.

Mipangilio ya upatikanaji na nyenzo za kupanga bei mara nyingi hufanya kazi pamoja. Ikiwa unataka kutumia nyenzo fulani, kama vile kutoa mapunguzo ya kila mwezi, huenda ukalazimika kubadilisha upatikanaji wako, kama vile kuruhusu sehemu za kukaa za muda mrefu.

Kurekebisha urefu wa safari yako

Kubadilisha urefu wa safari yako kunaweza kufungua kalenda yako na kulisaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji. Hakikisha kwamba kima cha chini na cha juu cha urefu wa safari yako kinafuata sheria na kanuni za eneo lako.

  • Kima cha chini cha usiku: Kupunguza kima cha chini cha urefu wa safari yako huwavutia wageni wanaoweka nafasi ya ukaaji wa muda mfupi na husaidia kujaza nafasi kwenye kalenda yako. Una chaguo la kuweka kima mahususi cha chini cha safari yako kulingana na siku ya wiki.
  • Idadi ya juu ya usiku: Kuongeza kima cha juu cha urefu wa safari yako husaidia kuwavutia wageni wanaoweka nafasi ya ukaaji wa muda mrefu, jambo ambalo linapunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka. Unaweza pia kuruhusu maombi ya ukaaji wa muda mrefu kuliko kima chako cha juu. Utaweza kutathmini na kuidhinisha maombi haya.
  • Urefu mahususi wa safari: Kuweka urefu mahususi wa safari ambao ni mfupi kuliko urefu wa kima cha chini cha safari yako kwa tarehe fulani kunaweza kukusaidia kujaza nafasi kwenye kalenda yako.

Kusimamia upatikanaji wako

Unahitaji ilani ya muda gani kati ya uwekaji nafasi wa mgeni na kuwasili kwake? Je, ungependa kuruhusu wageni kuweka nafasi mapema kiasi gani? Weka upatikanaji wako ili uwekewe nafasi zinazokufaa. Usiku utapatikana kiotomatiki kulingana na mipangilio unayochagua. Hutahitaji kurekebisha kalenda yako mwenyewe.

  • Ilani ya mapema: Chagua ama siku hiyo hiyo, angalau siku 1, angalau siku 2, angalau siku 3 au angalau siku 7. Una chaguo la kuruhusu pia maombi ya siku hiyo hiyo, lakini utaweza kutathmini na kuidhinisha maombi haya.
  • Ilani ya mapema ya siku hiyo hiyo: Ukiruhusu wageni kuweka nafasi siku hiyo hiyo, unaweka muda wa mwisho ambao baada ya hapo hawawezi kuweka nafasi tena. Chagua saa yoyote kati ya saa 12:00 asubuhi na saa 6:00 usiku.
  • Wakati wa maandalizi: Chagua idadi ya usiku unaohitaji kuzuia kabla na baada ya kila nafasi iliyowekwa. Machaguo ni hakuna, usiku 1 kabla na baada ya kila nafasi iliyowekwa na usiku 2 kabla na baada ya kila nafasi iliyowekwa.
  • Kipindi cha upatikanaji: Kuongeza muda wa upatikanaji wako kunawawezesha wageni waweke nafasi mapema zaidi na kulisaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji. Chagua kati ya miezi 3, miezi 6, miezi 9, miezi 12 na miezi 24 kuanzia tarehe ya leo.
  • Mipangilio zaidi ya upatikanaji: Una chaguo la kuwazuia wageni kuingia au kutoka kwenye siku fulani za wiki. Hii inazuia kalenda yako dhidi ya wageni wanaowasili na kuondoka ikiwa unajua kwamba hupatikani kila wakati siku hizo. Unaweza kuchagua siku kadhaa za wiki lakini si kila siku, kwani hiyo itawazuia wageni kuweza kuweka nafasi kwenye nyumba yako.

Kuunganisha kalenda zako

Kuoanisha kalenda zako zote za kukaribisha wageni husaidia kuzuia wageni wengi kuweka nafasi kwenye tarehe hiyo hiyo. Muunganisho huu wa njia mbili husasisha kalenda zote mbili kiotomatiki usiku utakapokuwa umewekewa nafasi. Kuunganisha kalenda zako:

  • Weka kiungo cha kalenda ya Airbnb kilichotolewa kwenye tovuti nyingine.
  • Pata kiungo kinachoishia na .ics kutoka kwenye tovuti nyingine na ukiweke kwenye kalenda yako ya Airbnb.

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji
Kwa kutumia kalenda yako
Badilisha mipangilio yako ya upatikanaji
Airbnb
9 Jan 2025
Ilikuwa na manufaa?