Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

    Kuweka malengo ili kuboresha utendaji wa tangazo lako

    Jaribu nyenzo hizi za Airbnb na vidokezi vya Mwenyeji Bingwa ili kuboresha mikakati yako.
    Na Airbnb tarehe 25 Feb 2022
    Inachukua dakika 4 kusoma
    Imesasishwa tarehe 25 Feb 2022

    Vidokezi

    • Kutathmini historia yako, tathmini za wageni na mielekeo ya eneo lako kunaweza kukusaidia kujipanga kwa ajili ya mafanikio

    • Unaweza kufuatilia utendaji wa tangazo lako kutoka kwenye akaunti yako ya kukaribisha wageni

    • Baada ya kuweka malengo mapya, sasisha tangazo lako ili uyatimize

    Januari si mwezi pekee ambao unaweza kuamua kukuza biashara yako. Kuangalia maendeleo yako mara kwa mara—na kurekebisha mkakati wako kama inavyohitajika—ni kichocheo cha kuwa na mafanikio mwaka mzima.

    Nyenzo zako za kukaribisha wageni hufanya iwe rahisi kufuatilia utendaji wa tangazo lako, kujifunza kile kinachowafaa Wenyeji wengine na kuweka malengo ya kupata matokeo unayoyataka.

    Fuatilia utendaji wa tangazo lako

    Ni vigumu kujua kinachofaa bila kupima maendeleo yako. Ili kukusanya taarifa, tumia dashibodi yako ya kukaribisha wageni:

    • Tafakari kuhusu nafasi unazowekewa na mapato yako
    • Soma maoni kutoka kwenye tathmini za wageni
    • Chunguza mielekeo ya sasa ya usafiri wa ndani

    Sehemu ya Vidokezi ya dashibodi yako ya kukaribisha wageni hutoa takwimu za msingi, ikiwemo mapato yako ya kila mwezi, idadi ya usiku uliowekewa nafasi, tathmini za wageni na ukadiriaji wa jumla. Pia ni nyumbani kwa kituo cha Fursa, ambacho kinaonyesha mielekeo ya usafiri katika eneo la tangazo lako, kama vile ni aina gani ya sehemu za kukaa na vistawishi ambavyo wageni wanatafuta zaidi.

    Unapotafakari kuhusu nambari zako, fikiria iwapo mkakati wako wa kupanga bei na upatikanaji wa kalenda unatumia kikamilifu mielekeo ya sasa ya usafiri na misimu au vipindi vya idadi kubwa ya wasafiri katika eneo lako. Unaweza pia kutumia maoni kutoka kwa wageni wako.

    "Wasikilize wageni," anashauri Mwenyeji Bingwa Elaine wa Visiwa vya Balearic, Uhispania. “Wanaweza kukuambia mengi kuhusu kile kisicho bora. Kufanya maboresho kutasababisha uweze kuweka bei bora."

    Ili kuingia ndani zaidi kwenye data yako, jaribu kuwasha nyenzo zetu za kiweledi ili ufikie dashibodi yako ya utendaji. (Unaweza kurudi wakati wowote katika mipangilio ya akaunti yako.)

    Nyenzo hizi za kiweledi zinakuwezesha kufuatilia utendaji wako—kiwango cha ukaaji, bei ya wastani ya kila usiku, mionekano ya wageni na kadhalika—katika matangazo mengi katika mwaka uliopita. Unaweza pia kulinganisha metriki zako na matangazo yanayofanana na lako ili kukusaidia kutambua ni ipi kati ya mikakati yako ya kukaribisha wageni inayofaa zaidi.

    Kwa kusikitisha, stadi zangu za kutunza mahesabu ni duni ikilinganishwa na huduma yangu ya kukaribisha wageni! Lengo langu la mwaka huu ni kuboresha uhasibu wangu.
    Superhost John,
    Munnsville, New York

    Pata maelezo kuhusu kile kinachowafaa Wenyeji wengine

    Mara baada ya kutambua kile kinachoweza kukusaidia kuboresha utendaji wa tangazo lako, unaweza kujiuliza jinsi ya kufanya mabadiliko. Badala ya kuanza kutoka mwanzo, unaweza kujifunza kutokana na uzoefu wa Wenyeji wengine waliofanikiwa.

    Hapa katika Kituo cha Nyenzo, unaweza kupata vidokezi vya Mwenyeji Bingwa kuhusu mada kama vile kuunda mpango wa biashara na kuweka vistawishi ukiwa na pesa chache. Au uangalie mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni.

    Unaweza pia kujifunza kutoka kwa Wenyeji wengine kwa kutafuta machapisho yanayohusiana na mahitaji yako katika Kituo cha Jumuiya. Kwa mfano, hebu tuseme unatafuta njia tofauti za kusimamia fedha zako. Mwenyeji Bingwa Ann wa Jiji la New York anaelezea mbinu yake katika chapisho la jumuiya.

    "Lengo langu la kwanza ni kupata wastani wa mapato zaidi kwa siku kuliko matumizi kwa siku," Ann anaandika. "Ninaweka lahajedwali yenye kiasi jumla kinachobadilishwa mara kwa mara. Katika miaka miwili iliyopita mapato yangu yamezidi matumizi, kwa hivyo huo ni mwelekeo ninaotaka uendelee."

    Weka malengo yako ya kukupa mafanikio

    Hatua inayofuata ni kugeuza taarifa zote ulizokusanya kuwa malengo ya mwaka unaofuata. Fikiria kuhusu kile kinachostahili umakini zaidi na ni hatua gani unaweza kuchukua ili kuanzisha maendeleo yako.

    Kwa mfano, haya ni baadhi ya malengo ya kawaida na njia za kuyatimiza:

    1. Ongeza nafasi unazowekewa na mapato
    Kuhakikisha kwamba mkakati wako wa kupanga bei ni sahihi kunaweza kuhitaji majaribio kadhaa. Ili kutimiza malengo yako ya kifedha huku ukiwavutia wageni, fikiria kuweka ada ya mnyama kipenzi au kutoa punguzo kwa ajili ya sehemu za kukaa za muda mrefu.

    Kuhakikisha kwamba tangazo lako ni la kisasa kunaweza kusaidia sana katika kufikia mafanikio ya kukaribisha wageni. Ukiwa na uelewa wa mielekeo ya usafiri ya eneo lako wakati kuna uhitaji mkubwa zaidi wa usafiri, wasafiri wengi na wachache, panga upatikanaji wa kalenda yako.

    Unapojaribu kutafuta ni nini kinachokufaa zaidi, Mwenyeji Bingwa Andrew wa Berlin anapendekeza kuwa na subira na kuzingatia kuridhika kwa wageni: "Baadhi ya matangazo ya Airbnb yamewekewa nafasi mwaka mzima, lakini kwa kawaida huchukua mwaka mzima ili kutambua mienendo yako na kujenga sifa kutokana na tathmini."

    2. Pata tathmini bora za wageni
    Boresha maelezo ya tangazo lako ili kuweka matarajio wazi na kuonyesha vistawishi ambavyo wageni wanataka, kama vile Wi-Fi ya kasi ya juu na jiko lenye vifaa vya kutosha. Hakikisha kwamba unajumuisha picha zenye ubora wa juu ambazo zinaonyesha uzuri wa sehemu yako.

    "Picha kuu hubeba uzito zaidi wa kuuza tangazo," Andrew anasema. "Picha changamfu zenye rangi za kuvutia macho, zilizopogolewa ili kufanya kinachoangaziwa kionekane kikamilifu katika muundo mdogo, ni muhimu."

    Wageni wanajali sana usafi pia: Sehemu isiyo na doa inaweza kusababisha tathmini nzuri. Wape wageni uhakika kwa kushiriki kile unachofanya ili kufanya usafi na kutakasa eneo lako.

    3. Rahisisha utaratibu wako wa kukaribisha wageni
    Kupata njia bora zaidi za kushughulikia majukumu ya mara kwa mara kunaweza kufanya iwe rahisi kukaribisha wageni na kutimiza malengo yako. Jaribu kutumia majibu ya haraka na ujumbe ulioratibiwa ili kufanya mawasiliano yako na wageni yawe ya kiotomatiki.

    Mbinu nyingine za kuokoa muda ni pamoja na kurahisisha mchakato wako wa kuingia, kuboresha utaratibu wako wa kufanya usafi na kufafanua sheria za nyumba yako. "Sheria za nyumba hazipaswi kusomeka kama msamiati wa kisheria," anasema Mwenyeji Bingwa J Renato wa Rio de Janeiro. "Ikiwa ziko hivyo, hakuna atakayezisoma."

    Haijalishi malengo yako ya kukaribisha wageni ni gani, tuko hapa kukusaidia kuyatimiza na kufanya mwaka huu uwe bora zaidi kwako.

    Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    • Kutathmini historia yako, tathmini za wageni na mielekeo ya eneo lako kunaweza kukusaidia kujipanga kwa ajili ya mafanikio

    • Unaweza kufuatilia utendaji wa tangazo lako kutoka kwenye akaunti yako ya kukaribisha wageni

    • Baada ya kuweka malengo mapya, sasisha tangazo lako ili uyatimize

    Airbnb
    25 Feb 2022
    Ilikuwa na manufaa?