Muhtasari na hoja kuu

Tathmini kile ulichojifunza na upate hatua zinazofuata za kuanza kama Balozi Mwenyeji Bingwa.
Na Airbnb tarehe 30 Nov 2023
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 30 Nov 2023

Kwa kutathmini makala na video katika mfululizo huu wa mafunzo, uko kwenye njia nzuri ya kuwasaidia wengine kama Balozi Mwenyeji Bingwa. Huu hapa ni muhtasari wa kile tulichojifunza, pamoja na vikumbusho vya hatua za kuchukua ili tuweze kukuunganisha na Mwenyeji wako mpya wa kwanza.

Jinsi mpango unavyofanya kazi

  • Tutakuunganisha na Wenyeji watarajiwa na wapya kulingana na lugha, eneo na aina ya sehemu.
  • Utajibu maswali yake na kushiriki vidokezi na nyenzo za Airbnb.
  • Kila mara Mwenyeji mpya uliyemsaidia anapokamilisha ukaaji wake wa kwanza, utapokea zawadi.

Jinsi ya kutumia dashibodi yako

  • Dashibodi ni mahali ambapo utasimamia maingiliano na Wenyeji wapya.
  • Vichujio hukusaidia kupanga kikasha chako na kuwaweka Wenyeji kwenye vikundi kulingana na maendeleo yao.
  • Unaweza kuweka upatikanaji wako kuwa "Mtandaoni sasa" ili kuonyesha kwamba unapatikana mara moja au usitishe uonanishaji mpya wakati una watu wa kutosha wa kusaidia.
  • Tazama video hii ili kuona ziara ya kina ya dashibodi ya Balozi Mwenyeji Bingwa

Jinsi ya kuwasiliana na Wenyeji wapya

  • Mikutanisho mipya inaonekana kwenye dashibodi yako.
  • Bofya kwenye picha ya wasifu ya mtu ili kupata maelezo yake na uanzishe mawasiliano.
  • Kuunda ujumbe ulioratibiwa hufanya mawasiliano ya awali yawe rahisi, lakini ni wazo zuri kuyafanya yawe mahususi.
  • Unaweza kuanzisha simu ya Zoom ukitumia nyenzo zako za kutuma ujumbe kwenye kikasha
  • Fuatilia maendeleo ya Wenyeji wapya kwenye dashibodi yako na utoe usaidizi kulingana na uhitaji.

Vidokezi vya kutoa usaidizi bora

  • Wenyeji wapya watafurahia kusikia kutoka kwako ndani ya saa 24.
  • Ukichagua mpangilio wa “Mtandaoni sasa”, unaashiria kwamba unapatikana ili kupiga gumzo la moja kwa moja, kwa hivyo uwe tayari kushiriki.
  • Kuwapa wengine masimulizi ya kile unachotamani laiti ungejua ulipoanza kukaribisha wageni kunaweza kuleta mabadiliko makubwa.
  • Kutumia maneno ya kirafiki kwenye ujumbe wako kunaweza kusaidia mawasiliano yako kwenda vizuri.
  • Kukubali tofauti zenu huku ukitafuta mambo mnayokubaliana kunaweza kusaidia kujenga imani na wengine.
  • Kuuliza maswali kuhusu mahitaji na malengo ya kila mtu ya kukaribisha wageni hukusaidia kuelewa njia bora ya kuwasaidia.
  • Fikiria njia mbalimbali za kushughulikia wasiwasi na kusaidia kufungua vizuizi kulingana na mambo uliyopitia mwenyewe.
  • Unaweza kutoa mapendekezo wakati wowote kulingana na mambo uliyopitia.
  • Jisikie huru kujitolea kutathmini matangazo mapya kabla ya kuchapishwa.

Mahali pa kupata nyenzo za Airbnb

Ni nini kinachofuata?

Kumbuka kutathmini hatua zifuatazo ambazo zinapatikana kwako:

Umefaulu, sasa wewe ni Balozi Mwenyeji Bingwa rasmi. Hongera kwa kukamilisha mfululizo huu wa mafunzo na karibu kwenye mpango! Ikiwa una maswali au wasiwasi wowote, tafadhali usisite kuwasiliana na msimamizi wako wa jumuiya au wasiliana na ambassadors@airbnb.com.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
30 Nov 2023
Ilikuwa na manufaa?