Sasa unaweza kutumia Airbnb zaidi ya Airbnb
Mwaka 2007 tulikuwa na wazo: Itakuwaje ikiwa tutabuni njia ya watu kuweka nafasi ya nyumba kwa urahisi kama wanavyoweza kuweka nafasi ya hoteli? Tangu wakati huo, Airbnb imezidi wageni bilioni 2 waliowasili na kubadilisha jinsi watu wanavyosafiri. Lakini safari nzuri ni zaidi ya nyumba unamokaa. Ndiyo sababu tunakuletea:
- Huduma kwenye Airbnb – Huduma za ajabu za kufanya ukaaji wa mgeni uwe maalumu zaidi.
- Matukio ya Airbnb – Vinjari jiji ukiwa na wakazi ambao wanalijua vyema.
- Programu mpya ya Airbnb – Programu iliyoundwa upya ambayo inafanya iwe rahisi kwa wenyeji kusimamia nyumba, huduma au tukio lao na kwa wageni kuweka nafasi, hayo yote katika sehemu moja.
“Miaka kumi na saba iliyopita, tulibadilisha jinsi watu wanavyosafiri. Zaidi ya wageni bilioni 2 baadaye, Airbnb ina maana sawa na sehemu ya kukaa,” alisema Brian Chesky, mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Airbnb. “Kupitia uzinduzi wa huduma na matukio, tunabadilisha usafiri tena. Sasa unaweza kutumia Airbnb zaidi ya Airbnb.”
Huduma kwenye Airbnb
Mara nyingi watu huchagua hoteli kwa sababu ya huduma wanazotoa, kama vile huduma ya chumba, ufikiaji wa chumba cha mazoezi au miadi kwenye spa. Kuanzia leo, wageni wanaweza kupata huduma moja kwa moja kwenye Airbnb yao.
Tunakuletea Huduma kwenye Airbnb, huduma za kuaminika ili kufanya ukaaji uwe maalumu zaidi. Tunazindua aina 10 katika miji mahususi, huku huduma zinazotolewa na maeneo mapya yakiwekwa mara kwa mara kwenye programu ya Airbnb. Aina 10 za kwanza ni:
- Wapishi – Milo inayoandaliwa kwenye nyumba inayoweza kufanywa kuwa mahususi kikamilifu kutoka kwa wapishi wataalamu.
- Upigaji picha – Vipindi vya kupiga picha mahususi kutoka kwa wapiga picha wazoefu.
- Usingaji – Usingaji wa kurejesha usawa wa mwili ikiwemo usingaji wa Kiswidi, usingaji wa kina kwenye nyama na usingaji wa kupunguza mkazo kutoka kwa wataalamu wazoefu.
- Huduma za spa – Utunzaji wa uso, mikwaruzo midogo kwenye ngozi, skrabu za mwili na huduma nyinginezo, zinazotolewa na wataalamu wa urembo wa uso.
- Mazoezi ya viungo kwa mtu binafsi – Yoga, mazoezi ya viungo ya kuimarisha nguvu, HIIT na kadhalika, yanayoongozwa na wakufunzi wa mazoezi ya viungo, ikiwemo wataalamu maarufu wa mazoezi ya viungo na wanariadha wa mashindano ya dunia.
- Mitindo ya nywele – Unyoaji wa nywele wa kitaalamu, mitindo ya ukaushaji nywele na kadhalika kutoka kwa wanamitindo wazoefu.
- Upodoaji – Upodoaji kwa ajili ya kila siku au matukio maalumu kutoka kwa wapodoaji bingwa wataalamu.
- Huduma za kucha – Utunzaji wa kucha za mikono na miguu kutoka kwa wataalamu wazoefu wa kucha.
- Vyakula vilivyoandaliwa – Vyakula vilivyo tayari kuliwa vilivyoandaliwa na wapishi wataalamu.
- Kuandaa chakula – Huduma kamili ya kuandaa chakula yenye menyu mahususi, mapambo na vifaa, pamoja na mpangilio na kufanya usafi.
Huduma za Airbnb zinakaguliwa kwa ajili ya ubora, kwa kuzingatia vigezo kama vile maarifa, elimu, sifa na kadhalika. Wenyeji wa huduma wana uzoefu wa miaka mingi na wamekamilisha mchakato wa uthibitishaji wa utambulisho wa Airbnb. Wengi ni maarufu katika nyanja zao, ikiwemo wapishi kutoka migahawa yenye nyota ya Michelin, wapiga picha walioshinda tuzo na wakufunzi bingwa.
Huduma za Airbnb zinapatikana kwa karibu kila bei na huduma nyingi zinajumuisha ofa ya kuingia iliyo chini ya USD 50. Ukiwa na huduma za aina yoyote ya safari, unaweza kupata kila kitu kuanzia chakula kilichoandaliwa cha bei nafuu hadi mazoezi ya kila siku na mkufunzi mashuhuri.
Huduma zinaweza kufanyika kwenye nyumba, biashara ya mwenyeji wa huduma au sehemu ya umma. Ikiwa unakaribisha wageni kwenye nyumba, huduma zinaruhusiwa kiotomatiki. Hii ni njia moja ya kuwaonyesha wageni kwamba umewekeza katika kufanya ukaaji wao uwe wa kipekee zaidi.
Unaweza kuamua kutoruhusu huduma kwenye nyumba yako. Wasiliana na Airbnb Usaidizi ili kubainisha huduma zozote ambazo huruhusu na watasasisha sheria za nyumba yako.
Kuanzia leo, wataalamu wazoefu wanaweza kuwa mwenyeji wa huduma. Ni njia mpya ya kushiriki utaalamu wako na kukuza biashara yako.
Matukio ya Airbnb
Mojawapo ya sababu kuu za watu kuweka nafasi ya sehemu ya Airbnb ni kwa sababu wanaweza kuishi kama mkazi. Lakini ni vigumu kupata mambo bora ya kufanya ukiwa mahali ambapo hufahamu. Mara nyingi unaishia kwenye kikundi kikubwa, ukimfuata mwelekezaji wa watalii aliye na megafoni, ukifanya shughuli ambazo unahisi kana kwamba ni za kawaida tu. Itakuwaje ikiwa kungekuwa na njia halisi zaidi ya kupata uzoefu wa jiji?
Leo, tunakuletea Matukio ya Airbnb yaliyobuniwa upya kabisa, yanayoandaliwa na wakazi wanaolijua jiji lao vyema. Tunazindua matukio katika miji mbalimbali kote ulimwenguni na kuongeza zaidi kila siku. Wageni wanaweza kugundua sehemu bora za jiji kupitia matukio kama vile:
- Matukio ya alamaardhi, majumba ya makumbusho na kitamaduni – Ingia katika ulimwengu wa urejeshaji wa Notre-Dame kupitia macho ya msanifu majengo kutoka kwenye timu yake ya urejeshaji.
- Ziara ya vyakula, mafunzo ya upishi na matukio ya kula chakula – Pata ustadi wa sanaa ya kutengeneza ramen na mpishi kutoka mgahawa uliopewa tuzo ya Michelin Bib Gourmand.
- Matukio ya nje, michezo ya maji na wanyama wa mwituni – Panda farasi kupitia maeneo matakatifu ya Inca na mandhari ya kushangaza ya Andes na mtaalamu mkazi wa utamaduni na anthropolojia ya Andes.
- Matukio ya ziara za kwenye makumbusho ya sanaa, karakana za sanaa na ununuzi – Pata mavazi mapya kwenye kabati la nguo kupitia kipindi cha binafsi cha mitindo kutoka kwa mshauri wa mitindo wa Hollywood.
- Matukio ya mazoezi, siha na urembo – Ingia ulingoni ili upate uzoefu halisi wa mafunzo ya lucha libre ukiwa na mtaalamu wa mieleka wa Meksiko.
Matukio ya Airbnb yanakaguliwa kwa ajili ya ubora, kwa kuzingatia maarifa, sifa na uhalisi na mchakato huu unaendelea. Tunatathmini matukio mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba yanafikia viwango vyetu.
Mawasilisho sasa yamefunguliwa kwa ajili ya Matukio ya Airbnb. Ikiwa unajua jiji lako kwa undani na unatoa shughuli ya kipekee ambayo haipatikani mahali pengine popote, wasilisha wazo lako la kuandaa tukio.
Programu mpya kabisa
Tumeunda upya programu kwa ajili ya wenyeji ili kujumuisha kila kitu unachohitaji ili kusimamia nyumba, huduma au tukio lako:
- Anza Kutumia Airbnb – Nyenzo iliyorahisishwa ya kuunda tangazo hufanya iwe rahisi kuwasilisha huduma au tukio kwenye Airbnb.
- Kichupo cha leo – Kichupo kipya cha usimamizi wa nafasi zilizowekwa kinachojumuisha nyumba, huduma na matukio kinakusaidia kutoa ukarimu wa kipekee.
- Kalenda – Kalenda iliyoundwa upya kwa ajili ya nyumba, huduma na matukio inajumuisha mtazamo mpya wa kila siku na ratiba ya kila saa na ujumuishaji wa wakati halisi kupitia Kalenda ya Google.
- Kichupo cha matangazo – Nyenzo mpya za usimamizi wa tangazo kwa ajili ya huduma na matukio hufanya iwe rahisi kurekebisha kila kipengele cha tangazo lako, kuanzia eneo hadi bei.
Ikiwa unakaribisha wageni kwenye nyumba, pata ufikiaji wa mapema sasa ili uanze kutumia zana zako mpya za kukaribisha wageni.
Huduma hazipatikani katika maeneo yote, ikiwemo Brazili na Puerto Rico.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.