Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Je, mchakato wa kuweka nafasi wa Airbnb unafanya kazi vipi?

Pata maelezo kuhusu maulizo, maombi ya kuweka nafasi, Kuweka Nafasi Papo Hapo na kadhalika.
Na Airbnb tarehe 9 Feb 2021
video ya dakika 3
Imesasishwa tarehe 18 Ago 2022

Vidokezi

  • Wageni wanaweza kutuma maulizo ya kuweka nafasi ikiwa wana maswali kuhusu eneo lako

  • Unaweza kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo au kuhitaji maombi ya kuweka nafasi mwenyewe

  • Kuzoea kufanya ukaribishaji jumuishi wa wageni ni sehemu muhimu ya kuwa Mwenyeji mwenye ufanisi

Mchakato wa kuweka nafasi kwenye Airbnb umebuniwa kuwa rahisi na wa moja kwa moja. Lakini kama Mwenyeji mpya, unaweza kuwa na maswali kadhaa kuhusu jinsi mchakato huo unavyofanya kazi.

Mara baada ya kuelewa mchakato wa kupokea na kujibu maulizo ya kuweka nafasi, kuwasha au kuzima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, kufuatilia nafasi zilizowekwa na kupanga mapema ukitumia kalenda yako, utakuwa tayari kuwakaribisha wageni wako wa kwanza.

Kupokea maulizo ya kuweka nafasi

Baadhi ya wageni wanaweza kuwa na maswali, kwa mfano, kuhusu kuingia mapema au eneo lako mahususi. Wageni hawa wanaweza kukutumia maulizo ya kuweka nafasi kabla ya kuweka nafasi. Unapopata maulizo, kulingana na mipangilio yako, utapata barua pepe, arifa kwenye kikasha chako cha Airbnb au zote mbili.

Hata ikiwa unatumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, wageni wanaweza kukutumia maulizo ya kuweka nafasi kwanza ili wapate taarifa zaidi kabla ya kuweka nafasi. Utakuwa na saa 24 za kujibu ujumbe wao. Mara baada ya kujibu maswali yao, unaweza kutuma:

  • Idhini ya awali, ambayo inawaruhusu wageni kuweka nafasi kwenye sehemu yako ndani ya saa 24 bila hatua yoyote ya ziada kutoka kwako ikiwa umezima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo
  • Ofa maalumu, ambayo inakuwezesha kutoa punguzo (mara nyingi hutumika kwa ukaaji wa muda mrefu)
  • Arifa ya kukataa ikiwa huwezi kumkaribisha mgeni huyo, maadamu unafuata sera yetu ya kutobagua

Skrini ya maulizo ya kuweka nafasi ina machaguo matatu: toa idhini ya awali, ofa maalumu au kataa.
Ikiwa ungependa kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa, utahitaji kuwa na kiwango cha kutoa majibu cha asilimia 90 (pamoja na mambo mengine), kwa hivyo jaribu kuwajibu wageni ndani ya saa 24.

Jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi kwenye sehemu yako

Wageni ambao hawana maswali yoyote wanaweza kuweka nafasi kwenye sehemu ya kukaa kwa kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, ikiwa umekiwasha au kupitia ombi la kuweka nafasi, ikiwa umekizima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo.

  • Kuweka Nafasi Papo Hapo ni njia chaguo-msingi ya kuweka nafasi kwa matangazo yote. Ikiwa utatumia chaguo hili, wageni ambao wanakidhi matakwa yako yote na kukubali sheria za nyumba yako wataweza kuweka nafasi kwenye sehemu yako papo hapo kwa tarehe zozote zinazopatikana. Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo pia kinaashiria kwamba uko tayari kumkaribisha mtu yeyote anayekidhi vigezo vyako vya kuweka nafasi, sehemu muhimu ya kuwa Mwenyeji jumuishi.
  • Maombi ya kuweka nafasi hukupa saa 24 za kutathmini na kukubali au kukataa kila ombi la kuweka nafasi lililowasilishwa. Utaweza kufikia tathmini na wasifu wa wageni. Baadhi ya Wenyeji, hasa wale walio na sehemu za kipekee au ratiba zisizo thabiti, hupendelea maombi ya kuweka nafasi wenyewe.
Unapopokea ombi la kuweka nafasi, sogeza chini ili ufikie wasifu wa mgeni na tathmini za hivi karibuni.
Tunajaribu kujibu haraka iwezekanavyo na kujaribu kukubali maombi mengi kadiri tuwezavyo. Ni njia inayotegemeka ya kukuweka katika nafasi nzuri kwenye orodha ya utafutaji.
Superhosts Danielle and Eli,
Tannersville, New York

Kuhakikisha kwamba kalenda yako imesasishwa

Unaweza kurekebisha bei na mipangilio yako ili ukidhi uhitaji wa eneo lako kwa ajili ya nyakati tofauti za mwaka. Vidokezi vichache vya haraka vya kalenda:

Pata maelezo zaidi kuhusu mipangilio ya kalenda na kuweka nafasi

Mara baada ya kuelewa jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi kwenye sehemu yako na jinsi mchakato huo ulivyo, utakuwa tayari kukazia umakini kwenye hatua ya kufurahisha ya huduma ya kukaribisha wageni: kuwakaribisha wageni wako.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Wageni wanaweza kutuma maulizo ya kuweka nafasi ikiwa wana maswali kuhusu eneo lako

  • Unaweza kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo au kuhitaji maombi ya kuweka nafasi mwenyewe

  • Kuzoea kufanya ukaribishaji jumuishi wa wageni ni sehemu muhimu ya kuwa Mwenyeji mwenye ufanisi

Airbnb
9 Feb 2021
Ilikuwa na manufaa?